Saturday 12 November 2011

UJUMBE WA WAFANAYBIASHARA KUTOKA SINGAPORE WAWASILI ZANZIBAR

Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Singapore ukiongozwa na Waziri wa Biashara na Viwanda umewasili Zanzibar leo asubuhi kwa ziara ya siku moja.

Kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ujumbe huo ulipokelewa na Naibu Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar Thuweiba Kisaasi , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Viwanda na Wakulima Zanzibar Mbarouk Omar pamoja na maofisa mbali mbali katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar.

Kwa mujibu wa Ratiba iliotolewa na Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar , Ujumbe huo mchana huu utakuwa na mazungumzo na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd hukoOfisini kwake Vuga.

Usiku Kwenye Hoteli ya Serena iliopo Mjini Zanzibar Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore ataelezea juu ya hali ya Biashara nchini mwao na baadae kutatolewa maelezo juu ya nafasi za Vitega Uchumi viliopo Hapa Zanzibar.

Aidha Kamisheni ya Utalii Zanzibar nayo itapata nafasi kuelezea juu ya nafasi ziliopo Zanzibar katika mambo ya utalii na baadae kuwa na Chakula cha Usiku pamoja na kuwa na mazungumzo na Wafanya biashara wa Zanzibar na Wanasiasa.

Ujumbe huo Wawafanyabiashara kutoka Singapore ukiongozwa naWaziri wa Biashara na Viwanda unatarajiwa kuondoka Zanzibar hapo kesho asubuhi.i:

Na Mwenyekiti
Kwa kweli inabidi viongozi wetu inapokuja misafara kama hii tujifunze kutoka kwao, kwani Singapore ni moja ya mfano mizuri ambao mazingira na population vinashabihiana sana na Zanzibar, ila sisi tumeizidi kidogo kwani Singapore haina resource ya aina yoyote zaidi ya uchumi wake unategemea biashara tu,
Kwa mfano Singapore haina mafuta ila ni msafirishaji mkubwa wa mafuta, huwa inanunuwa mafuta ghafi (crude), na baadae husafisha na kuuza mafuta halisi.
Singapore ikiwa na per capital income kuishinda nchi kubwa kama Marekani na nchi nyengine,
Singapore imepiga hatuwa kubwa baada ya kujitowa kwenye shirikisho la Malaysia mara tu baada ya uhuru, hii iliipa nafasi kubwa zaidi ya kutumia uwezo wa watu wake katika kujiendeleza kiuchumi.
Kwa upande wa vita dhidi ya madawa ya kulevya, nakumbuka mwaka jana pia ulikuja ujumbe wa Singapore na kutowa ushuhuda wao wa jinsi gani waliweza kupambana na madawa ya kulevya na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, walisema kuwa mambo mawili makubwa ndiyo yaliyofanikisha hilo:
Kwanza ni uzalendo wa watu wake vikiwemo vikosi vya usalama, kwani uaminifu ni wa hali ya ju katika kutekeleza majukumu yao na
Pili kikubwa zaidi ni kuwepo adhabu ya kifo kwa yoyote ambae atapatikana na kosa la kuingiza madawa ya kulevya.
Nategemea Serikali yetu itachukuwa mazuri kama haya kutoka singapore!!!!!!!
ADB

No comments:

Post a Comment