Friday 11 November 2011
MLANGO ULE ULE ZANZIBAR ILIPITITISHWA KUJITOA JUMUIYA YA KIISLAMU (IOC) NDIO HUO HUO WA KUINGILIA FIFA:
Na Ramadhan Ali
Zanzibar ikiwa ni Nchi ya Kiislamu, ilishurutishwa Enzi za Utawala wa Rais Mwinyi na Dr.Salmin,miaka ya 1990, kujitoa kutoka Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (IOC) kwa kuwa swali la uwanachama ni la Muungano- swali la siasa ya nje ya Tanzania.
Jaribio jengine la Zanzibar au Zanzibar Football Association (ZFA) kujiunga na International Federation of Football Associations (FIFA) lilikataliwa mwaka huu. Hoja : eti "Zanzibar si nchi" na hivyo haina " Mamlaka " (Sovereignity) kukubalika kuwa Mwanachama wa FIFA kinyume na England,Wales,Scotland na Ireland ya Kaskazini.(Special status)eti kwa kuwa England ndie mama wa dimba-mother of football.
Lakini, ikiwa kujiunga nchi ya kiislamu ya Zanzibar- (Mecca ya Afrika Mashariki ) katika Jumuiya ya Kiislamu, ni mwiko kwasababu Zanzibar haina Mamlaka hayo na imejiingiza IOC kwa mlango wa nyuma, WAKATI sasa UMEWADIA kwa WAZIRI WA MICHEZO wa Zanzibar Bw.Jihad, Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar na Uongozi wa ZFA kuvaa njuga na kuanza KUHOJI Tanzania-bara ilijiunga vipi na FIFA;Halmashauri Kuu ya Olimpik Ulimwenguni (IOC) kupitia Tanzania Olimpic Committee (TOC),Shirika la Mabondia Ulimwenguni na Mashirika mengine ya KIMATAIFA wakati "MIMICHEZO" au "SPOTI" si swali la MUUNGANO kama wenzao Tanzania-bara walivyohoji uwanachama wa Zanzibar katika IOC ?.
JE,MASHIRIKA YA SPOTI YA PANDE HIZO MBILI YALIKAA PAMOJA NA KUOMBA UWANACHAMA KWA UBIA ?
Alao katika Shirikisho la dimba Ulimwenguni FIFA, hali haioneshi kuwa hivyo.Laiti ingelikuwa hivyo, ZFA isinge hanikiza kupiga hodi mlangoni mwa FIFA kuomba uwanachama wake pekee. Mabaraza 2 ya Taifa ya Spoti ya pande hizo mbili sasa yanapaswa kuitisha kikao kujadili NANI mwenye MAMLAKA hasa ya KUIWAKILISHA TANZANIA KIHALALI katika Mashirika ya Spoti ya Kimataifa mfano wa FIFA,IOC na World Boxing Federation, nikitaja Mashirika machache tu ya Kimataifa wakati SPOTI si swali la Muungano.
Wakati muwafaka kutafuta UFUMBUZI wa MEDANI YA SPOTI kwa Nchi mbili za Tanzania ni huu -sasa inapojadailiwa KATIBA MPYA.
Dimba linapaswa kwanza kuchezwa nyumbani Dar-es-salaam na Zanzibar kabla kukimbilia Zurich-Makao Makuu ya FIFA , Cairo-Makao Makuu ya CAF-Shirikisho la Kabumbu la Afrika au Lausane,Uswisi,Makao Makuu ya Kamati ya Olimpik Ulimwenguni. Pande hizo 2 zikae kutatua kero hii nyengine ya Muungano.
Katika Vikao hivyo vya serikali hizo mbili na Mabaraza 2 ya Michezo ya Kitaifa,kuna KITANDAWILI kinachobidi kufumbuliwa:
ILIKUAJE Tanganyika kwa kutumia KAWA la Tanzania , inaendelea kubeba BENDERA ya Tanzania medani za Kimataifa ilihali SPOTI si SWALI LA MUUNGANO ?
Hapa Serikali ya SMZ,ZFA na Baraza la Michezo la Zanzibar, ina turufu nzito ya kuwafanya ndugu zao wa Tanzania-bara kuridhia kukaa pamoja nao tena kwa nia safi kuchanganya upya karata na kuamua :
1.Ama kuacha Spoti kuendelea kuwa swali si la Muungano na kila moja isake uwanachama wake ulimwenguni au
2. kubadili Katiba /Hati ya Muungano na kulijumuisha katika Orodha ya Maswali ya Muungano na kuwa na timu moja.
Zanzibar ishikilie TANZANIA-BARA iache kupepea BENDERA ya Tanzania katika medani za Kimataifa ilhali swali la spoti si la Muungano.
Tanzania ni Muungano wa Nchi 2 na hakuna Upande wenye haki kulitumia jina hilo kwa masilahi ya Upande mmoja tu katika maswali yasio ya Muungano.
Ni hapa inapostahiku kuhoji TANZANIA katika FIFA/IOC/WBF na kadhalika, inamuakilisha nani-Tanganyika au Zanzibar ?
Nani katoa Mamlaka au Idhini ya Uwaklilishi huo ?
JE,MASHIRIKA HAYO YA KIMATAIFA YALIFICHWA KUWA SPOTI SI SWALI LA MUUNGANO AU YALIZIBWA MACHO KUSUDI?
KWANINI FIFA ILIPOUKATAA UWANACHAMA WA ZFA HAIKUHOJI UWANACHAMA WA TFF CHINI YA MISINGI SPOTI SI SWALI LA MUUNGANO ?
KWANINI UOGOZI WA ZFA HAUKOHOJI UWANACHAMA WA TFF AU HAIKUA DIPLOMASIA MURWA?
IKIWA NI HIVYO,
MBONA WENZAO WALIHOJI UWANACHAMA WA ZANZIBAR KATIKA IOC-JUMUIYA YA KIISLAMU NA KUIVUA NGUO ZANZIBAR HADHARANI ITOKE ? KWANINI MARAIS WAO WALIFEDHEHESHWA :MZEE MWINYI NA KOMANDOO ? JE, WALIOWADHIRI Hawakujua Diplomasia au kutambua ukweli kuwa 99% ya Wazanzibari ni waislamu nawangefaidika kimisaada ?
Ikija ikadhihirika kuwa Mashirika ya Spoti ya Tanzania-bara yameingia katika Vyama na Jumuiya za Kimataifa kinyemela kama ilivyoingia Zanzibar katika Jumuiya ya Kiislamu miaka ya 1990 mlango wa nyuma na kulazimishwa ITOKE, Tanzania inabidi kUSIMAMISHWA UWANACHAMA WAKE hadi kwanza swali la UHALALI wa UWAKILISHI WAKE liempatiwa ufumbuzi na pande zote mbili baada ya kuamua hadhi (Status ) ya michezo katika Muungano.
Kwahivyo, MLANGO ULE ULE ZANZIBAR ILIOTOLEWA NJE YA JUMUIYA YA NCHI ZA KIISLAMU (IOC), NDIO UWE ULE ULE ZFA WA KUINGILIA FIFA .
Ama sivyo, pande zote 2 za Tanzania, zifunge virago na zikae nje ya FIFA/ Kamati ya Olimpik Ulimwenguni (IOC) na Mashirika mengine ya Kimataifa kama zilivyokaa nje ya Jumuiya ya Kiislamu (IOC) zote mbili tangu enzi za Utawala wa Rais Mwinyi na Dr.Salmin pale KIBIRITI kilipotikiswa huko Dodoma.
Wakati kukaa nje ya Jumuiya ya Kiislamu hakutawakera baadhi ya Watanzania-bara wasiowaislamu ,kukaa nje ya FIFA , CAF ,Michezo ya Olimpik (IOC) kutawakereketa wote bila ya kuchagua dini au madhehebu na hivyo, watatafuta haraka UFUMBUZI kukitegua KITANDAWILI-TEGA.Ufumbuzi huo uje tena kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2014 na Michezo ya OLimpik Brazil,2016.
Mpira sasa uko langoni mwenu Wazanzibari muucheza. Wenzetu wameshatia goli langoni mwa FIFA/IOC/World Boxing Federation na Mashirika mengine ya Kimataifa.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ramadhan Ali is the Author of "Africa at the Olympics, "The Rise of African Football,1984" and "African football Stars in the Bundesliga,2002"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
It is high time now kwa wazanzibari kusema enough is enough kwa so called Muungano. kila kitu kina wezekana kinachotakiwa ni kujipanga tu na kujua tunataka nini. kwa nini sisi wazanzibari tumekuwa wanyonge sana kiasi hichi wanachoaamua watanganyika sisi twakubali tu why tunaogopa kusema, viongozi wetu munatupeleka wapi. nadhani sasa hivi sio wakati wa kutegemea viongozi ni wakati sasa kwa wananchi wote wanaoipenda zanzibar kujitolea kwa nguvu zao zote kuipigani zanzibar kutoka katika mikono ya kidhalimu ya mkoloni Tanganyika. Tukiamua tunaweza ....
ReplyDelete