Tuesday 8 November 2011

Kunyonyesha kunapunguza hatari ya kupata shinikizo wa damu - blood pressure


Na Mwenyekiti

NEW YORK (Reuters Health) – Mama ambao wananyonyesha kwa kipindi ambacho kimeshauriwa inaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa msukumo wa damu baadae.
Utafiti umegunduwa kuwa kunyonyesha sio kuwa inamfaidisha mototo tu bali pia na mama.
Kwa ujumla wataalamu wanasisitiza kuwa motto anyonyeshwe maziwa ya mama tu kwa muda wa miezi sita ya mwanzo baadae unaweza kumpa pamoja na maziwa ya ngombe ya kawaida mpaka afike mwaka mmoja.
Maziwa ya mama yanamsaidia mototo dhidi ya maradhi mengi kama  kuharisha (diarrhea) na mengineyo. Lakini pia kuna ushahidi unaoonyesha kuwa kunyonyesha kunamsaidia pia mama kujikinga na baadhi ya maradhi tofauti.
Utafiti umeonesha kuwa kunyonyesha kunapunguza hatari ya kupata kisukari (diabetes), wingi wa mafuta (high cholesterol) na maradhi ya moyo katika siku za baadae.
ADB

SOURCE: American Journal of Epidemiology, online October 12, 2011.

No comments:

Post a Comment