Friday 11 November 2011

DK SHEIN ZIARANI FALME ZA KIARABU UAE

Friday, November 11, 2011

Na Rajab Mkasaba, Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameondoka nchini jana kuelekea Falme za Kiarabu kwa ziara ya wiki moja.

Katika ziara Dk. Shein amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman na waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui.


Wengine alioambatana nao ni Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahadhi Juma Maalim, Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa na Uwekezaji Balozi Mohammed Ramia, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar, Salum Khamis Nassor pamoja na watendaji wengine wa serikali.

Akiwa nchini humo, Dk. Shein anatarajia kukutana na viongozi mbali mbali pamoja na wafanyabiashara, wenye viwanda na wawekezaji.

Miongoni mwa viongozi atakaokutana nao ni kiongozi wa Ras-Al-Khaiman Sheikh Saud bin Saqr Al-Qasimi, kiongozi wa Sharjah Sheikh Sultan Mohammed Al-Qasimi na viongozi wengineo.

Aidha, Dk. Shein atatembelea maeneo mbali mbali ya viwanda, bandari pamoja na maeneo ya kihistoria.
 
Chanzo: ZanziNews

No comments:

Post a Comment