Tuesday 31 January 2012

Vikao vingi utekelezaji Zero

Kikao cha kamati ya pamoja ya serekali ya Muungano wa Tanzania na Serekali ya Zanzibar kimekutana chine ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Mohd Gharib Bilali.
Kikao hicho kilicho husisha Mawaziri,makatibu Wakuu,Watendaji wa Serekali Wakiwemo pia Wataalamu Kilifanyika kwenye ukumbi wa Blue Ubungo Plaza Mjini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kikao hicho walikubaliana kuthibitisha kumbu kumbu za kikao cha Kamati ya pamoja ya SMT na SNZ cha Tarehe 2 Juni mwaka 2010 kilichokutana Bwawani Mjini Zanzibar.
Halkazalika Wajumbe hao walipitia Taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na Kikao hicho ambayo ni ushiriki Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki, Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia,Uvuvi katika ukanda wa Bahari kuu na Ushirikiano wa Zanzibar katika Tasisi za nje.
Tarifa nyingine ni ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika tasisi za Muungano, Mgawanyo wa mapato na faida yatokanayo na Bank kuu , Malalamiko ya wafanya biashara kutozwa kodi mara mbili waingizapo pidhaa zao Tanzania Bara,usajili wa vyombo vya moto, likiwepo pia ongezeka la gharama za Umeme wa Tanesco kwenda ZECO uharamia na utekaji nyara meli.
Katika majadiliano hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Dr Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazo husika kutowa maelezo ndani ya kipindi cha miezi mine utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia.
Mapema mwana sheria mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Othmani Masoud Othman Taratibu zote na Baraka kuhusu swala hilo zimeshachukuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Mapindizi na Baraza la Wawakilishi na kuliwakilisha Serekali ya Muungano kwa hatuwa za kisheria.
Naye makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisisitiza hoja ya kuwa na ratiba malum ya vikao pamoja na kupunguza urasimu wa utekelezaji wa mamuzi yanayofikiwa katika vikao hivyo vya pamoja.
Balozi Seif alisema itapunguza kero zilizopo na hatimae kuamsha ari ya kuimarisha Muungano kwa pande zote mpili.
Nirahisishieni kazi ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wake wako Solidarity na hakuna mjumbe wa CCM wala CUF katika swala lolote linalohusu Muungano,alisisitiza Balozi Seif.
Katika kikao hicho upande wa wajumbe wa Serekali ya Muungano uliongozwa na Waziri mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda wakati ule wa Zanzibar uliongozwa na makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif Ali Iddi.

Wananchi watakiwa kuwa makini kutetea maslahi ya Zanzibar

Na Khadija Khamis
Mjumbe wa Baraza la Katiba Zanzibar na Mwanasheria wa kujitegemea Ali Saleh amewashauri Wananchi wa Zanzibar kuwa makini katika kuwasilisha maoni yao ya kutetea maslahi ya Zanzibar na sio kuburuzwa na Wanasiasa ambao wanajali zaidi maslahi yao.
Ushauri huo ameutoa wakati alipokuwa katika mdahalo wa kujadili dhana nzima ya marekebisho ya Katiba na Wananchi wa Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mjumbe huyo alisema kuwa ndani ya mjadala wa Katiba kuna mambo mengi ya kujadiliwa lakini kwa upande wa Zanzibar la muhimu zaidi ni kujadili kero za Muungano kwani hii ndio nafasi pekee ya kuwakilisha mambo yanayowayima fursa Wazanzibar.
Akifafanua zaidi alisema kuwa suala la Muungano ndio muhimu kwa Wazanzibari kwa sababu limewaunganisha na sehemu ya pili ya Muungano ambapo kuwekwa sawa kwake kutaleta mabadiliko makubwa ya Kisiasa na Kiuchumi kwa Zanzibar
Alieleza kuwa kila siku jamii inazungumzia kero za Muungano jambo ambalo si sahihi kwani Muungano si kero ila Katiba iliyopo ina upungufu mengi ambayo yamepelekea kushindwa kukidhi haja kwa wakati na matumaini ya watu wa pande mbili za muungano huo.
Hata hiyo alisema pindipo Wazanzibari watakaa pamoja na kujadili kwa kina Katiba iliyopo kutawezesha mapungufu yaliyomo kuonekana jambo litakalowapelekea kufanya maamuzi bora zaidi wakati wa kupiga kura za maoni utapofika
Kwa upande wa Wananchi waliohudhuria kongamano hilo walisema kuwa umefika wakati wa kujenga mustakabali mpya wa mashirikiano ya pamoja na kuondoa itikadi za vyama kwa lengo la kujenga heshima ya Nchi ya Zanzibar.
“Tushikamane Wazanzibar tusipokuwa pamoja Zanzibar inakwenda zake lazima tuwe na msimamo mmoja bila kujali itikadi za vyama vyetu”alisema mmoja wa wananchi hao
Pia waliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwashughulikie katika kuwapatia vitambulisho vya Mzazibar Mkaazi ili kuweza kupata haki zao bila ya usumbufu.
Aidha walitoa wito kwa Serikali kuzidisha juhudi za kutoa elimu sahihi kwa Wananchi wa Zanzibar juu ya dhana ya marekebisho ya Katiba mpya ili wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba wawe na uelewa mpana.

Sunday 29 January 2012

Subject: WHEN ZANZIBAR WAS FOOLED, 25 APRIL, 1964

Extracts from Free Zanzibar Voice March/April, 1986
It is customary in many countries of the world to play practical but harmless jokes on one's friends on the 1st of April.  Our neighbour Nyerere chose the 25th of April for his gigantic hoax on Zanzibar.
On the fateful day Abedi Amani Karume, of Zanzibar and Julius Nyerere, of Tanganyika signed a piece of paper - Article of Union -   (appendixed below) which sold away for good the freedom and sovereignty of our ancient country and people. That was a tragic event not only for Zanzibar, but also for Tanganyika as well as for the whole region of East and Central Africa.  Freedom, like Peace, is indivisible. When freedom is destroyed in the farthest corner of the world the freedom of the whole world is threatened.   How much so when catastrophe of un-imaginable magnitude; for Nyerere it was a fulfillment of a dream.
GOVERNMENT NOTICE NO. 243 PUBLISHED ON 1/5/64. THE ACTS OF UNION OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR.
NOTICE: It is hereby notified that the following law was made by the Revolution Council of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, on twenty-fifth day of April 1964.
THE SCHEDULE: ARTICLE OF UNION BETWEEN THE REPUBLIC OF TANGANYIKA AND THE PEOPLE'S REPUBLIC OF ZANZIBAR
WHEREAS the Government of the Republic of Tanganyika and of the People's  Republic of Zanzibar, being mindful of the long association of the peoples  of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of  furthering that association and strengthening these ties and of furthering  the unity of African peoples, have met and considered the union of the  Republic of Tanganyika with the People's Republic of Zanzibar.
AND WHEREAS the Government of the Republic of Tanganyika and of the People's  Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in  one sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter  contained: -
It is therefore, AGREED between the Government of the Republic of Tanganyika and of the People's Republic of Zanzibar as follows: -
(i) The Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.
(ii) During the period from the commencement of the union until the Constitution for the United Republic (hereafter referred to as the interim period) the united Republic shall be governed in accordance with the provisions of Articles (iii) and (iv).
(iii) During the interim period the Constitution of the United Republic  shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for: -
a. a separate legislature and executive in and for Zanzibar as from time to  time constituted in accordance with the existing law of Zanzibar and having  exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to  the Parliament and Executive of the United Republic;
b. the offices of two Vice-Presidents one of whom (being a person normally   resident in Zanzibar) shall be the head of the aforesaid executive in and for Zanzibar and shall be the principal assistant of the President of the  United Republic in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar;
c. the representation of Zanzibar in the Parliament of the United Republic;
d. such other matters as may be expedient or desirable to give effect to the United Republic and to these Articles.
(iv) There shall be reserved to the Parliament and Executive of the United Republic the following matters:
a. The Constitution and Government of the United Republic;
b. External Affairs;
c. Defence;
d. Police;
e. Emergency Powers;
f. Citizenship;
g. Immigration;
h. External trade and borrowing;
i. The Public service of the United Republic;
j. Income tax, corporation tax, customs and excise;
k. Harbours, civil aviation, posts and telegraphs; and the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the United Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.
(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject:-
a. to any provision made hereafter by competent legislature;
b. to such provision as may be made by order of the President of the United Republic for the extension to Zanzibar of any law relating to any of the matters set out in Article (iv), and the revocation of any corresponding law of Zanzibar;
c. to such amendment as may be expedient or desirable to give effect to the union and to these Articles.

(vi)  a. The first President of the United Republic shall be Mwalimu JULIUS K. NYERERE and he shall carry on the     Government of the United Republic in accordance with the provision of these Articles and with the assistance of the Vice President aforesaid and of such other ministers and officers as he may appoint from Tanganyika and Zanzibar and their respective public services.
b. The first Vice President from Zanzibar to be appointed in accordance with the modifications provided for in Article (iii) shall be Sheikh ABEID KARUME.
(vii) The President of the United Republic in agreement with the Vice-President who is   head of the Executive in Zanzibar shall:-
a. Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the United Republic.
b. Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such members as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the United Republic.
(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the People's Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the United Republic and of Zanzibar in accordance therewith.
IN WITNESS WHEREOF Julius K. Nyerere, the President of Republic of Tanganyika, and Abeid Karume, the President of the People's Republic of Zanzibar, have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April 1964.   (Unquote).
The above document was the beginning to an end of the State of Zanzibar. In 1956 Nyerere with the convenience of the British administration in Tanganyika and Zanzibar and under its full blessings came to Zanzibar to complete his establishing of the Afro-Shirazi.  Eight years later -1964 - the evil seeds that Nyerere planted bore its monstrous fruit. Zanzibar was swallowed and digested to become part and percale of a new-fanged nation called Tanzania. At that moment the State of Zanzibar ceased to exist, it has even been wipped out from the world map.  Nothing but Tanzania.
Hoax Turned Sour
The hoax that Nyerere played on Zanzibar has turned sour, not only in respect of the delude islanders, but also in respect of Tanganyikans. The annexation called union has become a millstone round the neck of all Tanzanians.  It has become a tremendous liability. Poverty, disease, ignorance, humiliation and contempt have become the hallmark of the so called union since its inauguration on 25th April, 1964. The international press has at times caricatured Nyerere as a python who has swallowed a goat but incapable of completely digesting it or vomiting it. Only few years after the union Nyerere in obvious despair stated publicly, and his speech was broadcast live: - "This union with Zanzibar has brought us nothing but Balaa! Balaa!! Trouble! Trouble!!". It is known that his aides would often privately advise him to dissolve the monstrous union, but having crossed the Rubicon there could be no turning back with a man who fancied himself a reincarnation of his Roman namesake, Julius Caesar, whose Shakespearean play he has translated in Swahili. He had his pride to think about.  How else would he leave his mark in history?
It is true that Zanzibar has been dominated, conquered and subjugated.  In this lop-sided union between a mouse and a cat nothing is shared equally except backwardness, squalor and the impoverished Tanzania shilling, which on free market is worth 1/20 on its next door counterpart if anything so dramatically demonstrates the deterioration of the Tanzania union since its inception twenty years ago Nyerere's currency does it remarkably well.
However, history or not, truth cannot be distorted forever, and one cannot deceive all the people all the time. Tyrants, stooges, renegades, hypocrites and cowards may flourish for a time, but sooner or later, the truth be unveiled and culprits will see themselves in their complete nudity.
This is not the first time that Zanzibar has undergone the painful experience of being subjected to foreign rule.  Just as we were able to shake off the oppressive Portuguese rule, and the imperialism of Britain we should not shirk our duty in ridding the country from any tyranny.  No physical pleasure can well and truly allay the pangs of conscience for duty not done. We owe it to ourselves, and we owe it to our fathers and mothers that begot us, and our children and the children of our children yet unborn, to liberate the land of our ancestors from oppression and from alien domination. Above it we owe to our Maker to fulfill the mission for which He created us and fashioned us to fit the task to which we were assigned.
Grand-child". But we say: It is not too late. And it is better late than never. Instead of leaving your beloveds and live abroad as a refugee, it is a high time now that we unite as one Umma for the liberation of our mother-land and save our people from being completely wiped out by hunger, disease, ignorance and the imposition of foreign cultures and values which are calculated to destroy the very bases on which our nation is built.
Muhimu, sisi Wazanzibari umoja na ujirani ndio azimio letu tangu kale.  Vile vile, tunaamini katika nyoyo zetu kuwa binadamu amezaliwa huru na anatakiwa aishi huru, kwa hivyo basi, haturidhii kuona yoyote yule ananyimwa uhuru wake na kutawaliwa kwa njia yoyote ile.  Kutokana na imani hii  ndio tunaposema kwa sauti kuu kuwa tunataka Udola wa Zanzibar urejee na tuishi na ndugu zetu Tanganyika kwa ujirani na mafahamiano kama hapo zamani. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atupe kila la kheri na atuepushe na kila la shari – Amin.
Wa Billah Tawfiq
Farouk Abdulla Amour

Saturday 28 January 2012

Tuiache Zanzibar Iende kwa amani

Inocent Nganyagwa
 NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.
Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.
Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.
Kimsingi, Zanzibar in mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.
Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena.
Inashangaza kuwa kwa miaka sasa Zanzibar imekuwa ikipaza sauti kuwa hairidhiki na jinsi Muungano unavyoendeshwa. Lakini, wahusika walichokifanya, na ambacho wamekuwa wakiendelea kusisitiza kukifanya, ni kiini macho walichokipa jina la kutatua kero za Muungano.
Kinachowafanya waonekane kuwa ni majuha ni kuwa kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakiendelea na kiini macho hicho cha kutatua kero za Muungano lakini badala ya kwisha, kero zimekuwa zikiongezeka.
Ajabu ni kuwa wanaonekana kuwa hawaoni kuwa kero zinaongezeka badala ya kupungua licha ya juhudi zao za kushughulikia kero za Muungano.
Kwangu mimi, ilichokifanya Zanzibar mpaka hivi sasa ni njia za kuonyesha kistaarabu kuwa hairidhishwi na Muungano kwa sababu Wazanzibari wanaamini kuwa hauzingatii masilahi ya Zanzibar. Na walichokifanya wahusika ni kutumia nguvu kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kujiamulia mambo yao.
Walianza kudai kwa maneno tu, wakaonekana hawana hoja, wakakataliwa. Kwa kuwa walidhamiria kuendelea kudai kile wanachoamini kuwa ni haki yao, wakaanza kufanya baadhi ya vitu kwa vitendo.
Wakabadilisha sheria kadhaa ambazo kimsingi zinakiuka kabisa makubaliano ya Muungano kama ilivyopo sasa. Walipoona upande wa pili haujashtuka, wakaamua kubadili na Katiba kabisa. Lakini, inaonekana bado wahusika hawaelewi hawa jamaa wanataka nini.
Kitakachotokea sasa, sidhani kama ni kosa la Wazanzibari kwa sababu kama ni onyo walishalitoa na wakadharauliwa.
Upo msemo kuwa paka akibanwa kwenye kona, anaweza kugeuka kuwa chui. Hilo ndilo litakalotokea kwa Zanzibar. Kwa sababu imebanwa sana katika azima yake ya kutaka Muungano ambao una masilahi kwake, sasa itageuka kuwa mbogo kweli kweli. Na dalalili zimeanza kuonekana.
Zipo chockochoko za chini kwa chini ambazo zinawahusisha watu wa kawaida tu hivi sasa. Wapo watu wenye asili ya Tanzania Bara huko Zanzibar ambao wameanza kunyanyaswa na watu wa kawaida tu wa Zanzibar.
Kwa maelezo yanayotolewa, inaonyesha kuwa hilo ni suala la uhalifu wa kawaida tu ambao hata Tanzania bara upo, ingawa haulekezwi kwa Wazanzibari.
Lakini kwa wanaotaka kukiita kitu kwa jina lake halisi wanaelewa fika kuwa chokochoko hizi zina uhusiano ya kutoridhishwa kwa Zanzibari katika masuala ya Muungano. Wahusika hawataki kulikubali hilo lakini hiyo haibadilishi ukweli wa suala hilo.
Kwa kuwa tumeamua kuficha maradhi, tusubiri kifo kituumbue. Naamini kuwa Zanzibar haitachoka wala kuacha kudai haki zake ndani ya Muungano. Na kwa jinsi mambo yalivyo, wahusika wataendelea kukataa kutekeleza matakwa hayo.
Kwa kuwa suala hili limeshafika kwenye ngazi ya wananchi, ambao wameamka baada ya kuona kuna viongozi wao wengi tu ambao wana mawazo kama yao, tusitarajie kuwa litakwisha hivi hivi.
Nadhani wahusika wana hofu ya kuvunjika kwa muungano. Lakini wafahamu kuwa kuvunjika huko kwa Muungano kunaweza kuwa ndio suluhisho la kujenga Muungano mwingine utakaokuwa imara kwa sababu utajengwa chini ya maridhiano ya pande mbili zikikubaliana kuungana.
Lakini, kuna uwezekano mwingine kuwa ni kweli Zanzibar inabanwa sana kiuchumi ndani ya muungano na hivyo kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuisaidia ikajitanua. Itaisaidia pia Tanganyika iwapo itakuwa na jirani tajiri.
Kuendelea kulazimisha Muungano huu kutatuletea maafa hapo baadaye. Imeshajidhihirisha kuwa Wazanzibari hawataacha kudai haki zao mpaka wazipate.
Na itafika wakati Watanganyika nao watakapochoka na chokochoko hizo na wao kuamua kuanza kudai haki zao kwa hila na kwa nguvu. Sijui kama wahusika watakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na Watanganyika na Wazanzibari watakapoamua kudai haki zao kila mmoja kivyake.
Kuna nafasi adhimu ambayo viongozi wetu wanataka kutukosesha bila sababu za msingi. Kwa mtu anayepima upepo, atagundua kuwa watu wengi hawaridhishwi na aina ya Muungano uliopo. Na kwa hakika kabisa, miongoni mwa watu hao ni viongozi wetu wengi tu.
Tatizo ni kuwa waliopo madarakani hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kuwa ndio walioshiriki kuua Muungano. Wana hofu kuwa Zanzibar ikiruhusiwa kutoka basi Muungano utakuwa umekufa. Ile fursa kuwa kuondoka kwa Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuunda Muungano imara wala hawajaiona.
Wamejawa hofu ya kihistoria iliyopatia upofu wa masuala dhahiri kuwa kwa kulazimisha Muungano, eti tu kwa sababu ulianzishwa na waasisi wa taifa, watakuwa wanadumisha utaifa. Lakini kama wakiamua kufungua macho, watabaini kuwa wanachokifanya kinaua utaifa.
Kama nilivyoeleza awali, Zanzibar haiwezi kuendelea kuvumilia kulazimishwa kuwepo ndani ya Muungano. Itafika mahali itageuka mbogo na kulazimisha kile inachokitaka. Itakuwa vigumu sana kuzuia na kudhibiti hali ya mambo wakati huo.
Kama tunataka salama, ni heri tukaiacha Zanzibar iondoke kwenye Muungano sasa hivi kwa amani na utulivu, nasi tutabaki salama huku tukiwa na uwezekano wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu zaidi.
Lakini iwapo tutasubiri mpaka Zanzibar, au hata Tanganyika, ikaamua kujiondoa kwa nguvu, hatutabaki salama na wala hakutakuwa na uaminifu uliobakia wa kuwa msingi wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu.
Chanzo: Tanzania Daima

Umoja unahitajika Kukabiliana na Tanganyika

Na mwandishi wetu
Naungana na Wazanzibari wenzangu kutoa wito kwa wazanzibari wote kuwa kitu kimoja katika kipindi hichi ambacho Zanzibar iko kwenye msuguwano na serikali ya jamhuri ya muungano (Tanganyika) kuhusu muswada uliopitishwa na baraza la wawakilishi kuhusu nyongeza ya masafa ya bahari.
Kwa kweli suwala hili limetuwekea wazi jinsi gani wenzetu watanganyika walivo na nia mbaya na Zanzibar na jinsi gani wanavotumia mwanya wa kutugawa na kututawala, Tumeona jinsi gani Prof. Tibaijuka alivoigeuza hoja ya wajumbe wa baraza la wawakilishi na kuifanya ionekane kuwa ni hoja ya CUF, hii ni njia moja wanaoyoitumia kupotosha umma wa kizanzibari kwenye mambo ya msingi kama haya.
Nampongeza Mheshimiwa Hamza kwa utambuzi wake wa kulijuwa hilo na kutahadharisha mapema kuhusu njia ovu za kutugawa na kutumia udhaifu wa viongozi wetu wachache ambao hawana uzalendo na visiwa hivi na ambao wameweka maslahi yao mbele kuliko ya umma wa kizanzibari.

Hawa historia itawakumbuka juu ya usaliti wao dhidi ya Wazanzibari, na akina hamza na Jussa pia pia nao historia itawakumbuka na kuwaenzi  kwani historia inaonesha wale wote ambao wanakuwa upande wa umma ndio ambao hufanikiwa katika mbio zao kwenye nyanja mbali mbali ikiwemo za kisiasa.
Mwisho napendekeza Wazanzibari tuwe na utamaduni wa kuonesha hisia zetu kwenye mambo muhimu kama haya ili kwa hatuwa hizo tutakuwa tunawapa nguvu na kujiamini wale viongozi wetu ambao wanatetea maslahi yetu, nimeona hatuwa nyingi zinachukuliwa na sisi ambao tuko kwenye hii mitandao ambayo coverage yake ni ndogo sana mimi ningependekeza wale ambao wako nyumbani tuwe na utamaduni hata wa kuitisha maandamano locally kuwaunga mkono hawa viongozi wetu kwa mfano siku ambayo wanajadili hoja muhimu kama hizi tunapaza sauti zetu hata pale nje ya baraza la wawakilishi.

Jussa: Tibaijuka amepotoka

Tibaijuka amepotoka

Nimeona kuna haja ya kutoa maelezo mafupi kuhusiana na Hoja ya Kujadili Jambo la Dharura niliyoiwasilisha Baraza la Wawakilishi na kupitishwa na Baraza hilo tarehe 23 Januari, 2012 baada ya kuona kuna njama za makusudi za kujaribu kuipotosha kutoka upande wa Tanzania Bara, zikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao anaonekana alikurupuka (au sijui alikurupushwa) kuufanya tarehe 25 Januari, 2012, siku mbili baada ya Baraza la Wawakilishi kujadili na kupitisha hoja niliyoiwasilisha, alikuja na maelezo marefu ya kuthibitisha kwamba Zanzibar ilishiriki kikamilifu katika mchakato wote wa kutayarisha na hatimaye kuwasilisha Andiko Rasmi la kuomba Umoja wa Mataifa kuiongezea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukanda wa bahari kuu (Exclusive Economic Zone) kwa ziada ya maili za baharini (nautical miles) 150 baada ya kuongezewa maili 200 za awali, eneo ambalo ni sawa na kilomita za mraba 61,000.

Inasikitisha kuona mtu mwenye dhamana ya Uwaziri tena akiwa Profesa anashindwa hata kujiridhisha juu ya undani na uhalisia wa lile analotaka kulitolea taarifa kwa umma. Kama angelifanya juhudi ndogo tu za kuwasiliana na Ofisi za Baraza la Wawakilishi na kuomba kupatiwa nakala ya Hoja niliyoiwasilisha, Prof. Tibaijuka asingepotoka kiasi ambacho alipotoka.

Hoja yangu haikugusia suala la kushirikishwa au kutoshirikishwa Zanzibar katika mchakato huo. Mimi si mjinga wa kiasi cha wale wanaokurupuka kuzungumzia mambo wasiyoyajua hata nishindwe kuona picha inayomuonesha ofisa wa Zanzibar akiwa na ujumbe wa Tanzania Bara uliokwenda kuwasilisha andiko hilo. Isitoshe, hata katika maelezo ya hoja yangu nilinukuu habari iliyochapishwa na gazeti la Nipashe la tarehe 17 Januari, 2012 ambalo liliripoti maelezo yake Prof. Tibaijuka akitaja ushiriki wa maofisa na wataalamu wa Zanzibar katika matayarisho ya andiko hilo. Ndiyo kusema, nilikuwa najua ninachokizungumzia kwa sababu mimi sina tabia wala mwenendo kama wa Prof. Tibaijuka wa kukurupuka kuzungumzia nisichokijua.

Kama angejipa nafasi ya kuitafuta na kuisoma Hoja yangu ambayo sasa si yangu tena maana imeshapitishwa na Baraza la Wawakilishi na hivyo ni Hoja ya Baraza la Wawakilishi angejua kwamba miongoni mwa mambo niliyoyahoji ni hilo la kwa nini Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Mhe. Ali Juma Shamuhuna, na maofisa wa Wizara yake walishiriki katika mchakato huo huku wakijua kwamba Baraza la Wawakilishi lishapitisha maamuzi tarehe 08 Aprili, 2009 ya kukataa ushirikiano katika suala la EEZ na kutaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imiliki na kusimamia wenyewe ukanda wake wa EEZ. Uamuzi huo unajulikana hata na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kutokana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Waziri Kiongozi wa wakati ule, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, kumuandikia Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kumueleza maamuzi ya Zanzibar yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi.

Kwa upande mwengine, mimi na Wajumbe wengine saba (7) waliochangia hoja hiyo tulikosoa kitendo cha Waziri Shamuhuna kushiriki katika suala hilo bila ya kulitaarifu Baraza la Mapinduzi (ambalo kwa Zanzibar ndiyo Baraza la Mawaziri) ikiwa ni kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 43 (5) inayozungumzia uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).

Kitendo cha Prof. Tibaijuka kukurupuka na kujibu hoja isiyokuwepo ya ushiriki wa Zanzibar kinaonesha jinsi asivyo makini katika kazi zake na ndiyo maana akashindwa kupembua na kutofautisha mambo madogo kama haya. Nadhani Rais Jakaya Kikwete anapaswa kufikiria tena uteuzi wake kwa mama huyu ambaye ameonesha dhahiri hana uwezo wa kuchambua mambo.

Kwa upande mwengine, namuonea huruma Prof. Tibaijuka kwa kufanya jaribio la jambo lisilowezekana tena katika Zanzibar ya leo. Kitendo chake cha kuihusisha hoja niliyoiwasilisha na CUF kilikuwa na lengo la kuchochea mgawanyiko wa itikadi za kisiasa katika suala kubwa linalogusa maslahi ya Zanzibar kama hili. Bahati nzuri, angejipa nafasi ya kuwasikiliza Mhe. Hamza Hassan Juma, Mhe. Asha Bakari Makame, na Mhe. Ali Mzee Ali, wote wakiwa Wawakilishi wanaotoka CCM, angejua kuwa zama za kuwagawa Wazanzibari zimepiwa na wakati kwani wote walitahadharisha juu ya uwezekano wa upotoshaji kama ule aliokuja kuufanya Prof. Tibaijuka.

Mwisho, niseme nimesikitishwa na kitendo cha Mhariri wa gazeti la Mwananchi kupitia Tahriri ya gazeti lake la tarehe 26 Januari, 2012, kupotosha kile kilichopitishwa na Baraza la Wawakilishi hadi kufikia kusema kuwa kimetokana na ‘maneno ya mitaani’ huku akijaribu kukionesha kama ni jambo langu binafsi. Kutokana na upotoshaji huo, nimemuandikia Spika wa Baraza la Wawakilishi barua ambayo nitaifikisha Jumatatu ya tarehe 30 Januari, 2012 kumuomba atumie Kanuni ya 116 (2) (a) kumuita Mhariri huyo mbele ya Kamati ya Maadili na Kinga za Wajumbe na kumtaka ajieleze kwa nini asichukuliwe hatua kwa kutenda kosa la jinai chini ya Sheria ya Kinga, Haki na Fursa za Baraza la Wawakilishi (Sheria Nam. 4 ya 2007), kifungu cha 32 (1) (a).

Ismail Jussa
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe
ZANZIBAR

Thursday 26 January 2012

Kwa hili, Jussa Hana haja ya kuomba radhi

Ally Saleh
Nimesoma makala ambayo inaelekea kua imechapishwa katika gazeti kuhusu matamshi ya Waziri wa Muungano wa Ardhi na Makazi, Professa Anna Tibaijuka na kufadhaishwa na udhaifu wa ufahamu wake katika suala linalohusu Hoja Binafsi ya Mheshimiwa Ismail Jussa.

Kama Profesa Ana Tibaijuka angefahamu Hoja Binafsi ya Jussa basi asingetamka kabisa kuwa Jussa aombe radhi, wala asingetamka kabisa kuwa Serikali ya Zanzibar ilirishirikishwa.

Alichosema Jussa na anachokisema Professa Tibaijuka ni vitu viwili tofauti, na kama Professa Tibaijuka alipita baina ya mstari kwa mstari wa Tamko la Jussa basi kwa hakika yeye alipaswa kuilaumu Serikali ya Zanzibar na sio Jussa.

Lakini hata hilo la kuilamumu Serikali ya Zanzibar halipo, kama ambavyo nitaeleza.

Anavyodai Profesa Tibaijuka ni kuwa mchakato si wa leo na jana na kwamba ulianza tokea mwaka 2007 na wakati wote kulikuwa na ushiriki kamili wa maafisa wa Serikali ya Zanzibar na hata kushiriki katika safari ya kwenda New York kukabidhi andiko hilo.

Tukubali hilo la ushiriki wa SMZ, lakini ndio linalifanya jambo hilo kwa ukubwa na upana wake liwe halali? La.

Kwanza ni haramu kwa kuwa mwaka 2009 Baraza la Wawakilihsi lilipitisha Azimio la Baraza kwamba mambo yote kuhusu mafuta na suala la bahari na mipaka yake litoke au litolewe na kusimamiwa na Zanzibar wenyewe.

Kwa hivyo kuanzia 2009 mtu yoyote aliyefanya chochote kinyume na Azimio la Baraza alikuwa anakwenda kinyume na sheria na kinyume na Katiba.

Pili, kuanzia mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka jana kuwa Zanzibar inarudisha mipaka yake yote ilikuwa yake kabla ya kuja kwa Jamhuri ya Muungano, inakifanya kila kitu kinachohusu mipaka kikifanywa na Serikali ya Muungano bila ya ridhaa ya Zanzibar ni haramu na batili.

Najua hapa kunaweza kuwa hoja kwamba Katiba ya Muungano ni Katiba mama na kwa hivyo mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar hayawezi kukiuka matakwa ya Katiba ya Muungano, lakini hilo ni kosa kuamini hivyo kwa sababu katiba hizo mbili ni sawa katika ukubwa wake.

Tatu, Profesa Tibaijuka ajue kuwa Hoja ya Jussa haijakataa uwepo wa mipaka ya Tanzania, lakini ilichokuwa ikitaka ni pande mbili hizi kufahamiana ndani ya mipaka ya Tanzania haki za Zanzibar ni zipi kwa sababu katika bahari kuna suala la uchumi, uvuvi na uwekezaji mambo ambayo yote si ya Muungano,

Bila ya kwanza kumalizana ndani kujua haki za Zanzibar itakuwa kama vile suala la Jumuia ya Afrika Mashariki ambapo katika Mambo 14 ya Afrika Mashariki ni 3 tu ambayo ni ya Muungano na kwa hivyo Tanzania inaisemea na kuichukulia maamuzi Zanzibar katika mambo 11 ambayo si ya Muungano.

Profesa Tibaijuka ni Waziri wa Ardhi, Makazi na Nyumba mambo ambayo yote si ya Muungano, anapataje haki na uwezo wa kwenda kuiwakilisha Tanzania na kuisemea Zanzibar wakati katika wizara yake suala la bahari halimo.

Na hata kama lingekuwemo basi bahari si suala la Muungano na kwa hivyo pande hizi mbili zingebidi zikae upya kuamua kufikiria iwapo ipo au hakuna haja ya kulitia suala hilo katika Mambo ya Muungano.

Au kwa wakati huu kwa kuwa si la Muungano pande hizi mbili lingelikabili vipi suala hilo kama ajenda ya Muungano. Kwamba mawaziri wameshiriki na Serikali kutoa wajumbe hakulifanyi jambo hilo liwe halali kama ambavyo hakulifanyi jambo hilo liwe la Muungano.

Pia Professa Tibaijuka kama angemfahamu Jussa na kwa hivyo mawazo ya Wazanzibari ni kuwa hawaamini jambo lolote linalofanywa na Serikali ya Muungano kuhusiana na Zanzibar na kwa hivyo chochote kile kinapaswa kufikiwa maamuzi na hata kukatibiana na mapema.

Sijui kama Professa Tibaijuka anajua kuwa shaka hii ni kubwa na imeonekana katika mambo kadhaa wa kadhaa na kama anataka afaidi mtizamo wa Wazanzibari juu ya wanavyouona Muungano na pingamizi zake asome makala ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud “ Masuala ya Muungano Yasiokuwa na Majibu.”

Hadaa, mbinu na hila mbali na udhaifu katika utekelezaji na maamuzi umeonekana katika mambo mengi kiasi ambacho inatisha na Muungao huu umekuwa ukenda msege mnege na kupindana mkono kuliko ridhaa ya upande mmoja.

Maamuzi kadhaa yanayofanywa kwa kuwa hayana mashiko ya kikatiba na sheria katika zile zinaozoitwa kero za Muungano, yamebaki kama yalivyo na kwa kweli asilimia 95 ya kero za Muungano ni zile zenye kuibana na kuikandamiza Zanzibar.

Waziri Professa Tibaijuka ambaye ni mgeni sana katika kilinge cha Muungano alipaswa afahamu taswira yote hii na asione malalamiko ya Jussa ni ya kuzuka tu na yasiokuwa na mashiko.

Kwa kumalizia hata kama Serikali ya Zanzibar ilishiriki basi wananchi wanasema wamefanyiwa khiyana na Serikali yao na kwa kupitia kwa Baraza la Wawakilishi wanataka Serikali yao ijue kuwa ilifanya makosa kushiriki katika mchakato huo bila ya kwanza kujua nafasi ya Zanzibar.

Profesa Tibaijuka fikiri jambo moja tu juu ya Serikali ambayo unasema ilishiriki katika mchakato huo. Wewe ni Waziri lakini uliyepewa kufuatana naye kwenda New York alikuwa ni Mkurugenzi Ayoub Muhammed Mahmoud wakati Wizara hiyo ina Naibu Waziri mzima…wewe ulijisikiaje kufananishwa na Mkurugenzi kuwa ndio colleague wako?

Kwa hili Ismail Jussa hana haja ya kuomba radhi. Ni kama alivyosema Muhammed Ghassany mwandishi wa habari wa Zanzibar. Mwizi anakamatwa amemebeba vitu vya watu anasepa navyo na alipokabiliwa akasema, “Mwizi mie…niombeni radhi.”

Prof. Sherif amjibu Tibaijuka

The controversy about the extension of the sea boundary has come at the right time when Zanzibaris have shown that they will no longer be hijacked when their vital national interest are at stake, regardless of party affiliation. It was rather disingenuous for Prof Tubaijuka to try to introduce party divisions when she claimed that CUF was claiming that Zanzibar was not consulted. If she heard the debate in the House of Representatives, it was almost unanimous, and prominent CCM backbenchers made a point of saying that this was not the question of CUF but of the whole of Zanzibar. She should not try to divide Zanzibaris again. We have suffered enough from such tactics.

It seems that mainland leaders feel that if you have a few Zanzibaris in your gang, then Zanzibaris are represented – and it is never difficult to get a few vibaraka, as we know all too well from our history. The question is whether the people in Zanzibar even knew this business was cooking – certainly the House of Representatives, a body that was elected by the whole people of Zanzibar, did not know about it until the professor was in New York presenting the document to the UN. I and many of my friends who try to keep up with events affecting our country were taken by surprise.

Prof Tibaijuka may be right that some people even in the Zanzibar Government may have been aware of this project, but the Minister of Lands in Zanzibar, Mr Shamhuna himself said in the House of Representatives that he know about it, but the Zanzibar Government did not know it officially. The Executive Summary of Tanzania’s submission to the UN has 2 long lists of institutions and people who were involved in this project, but mentions only Shamhuna’s Ministry of Lands out of 9 institutions, and only one State Attorney from Zanzibar out of 8 members of the Technical Core Group. Now Professor Tubaijuka mentions a few more names of Zanzibari ‘representative’, including my friend and former student Zakia Meghji, but if my memory serves me right, she used to be an MP for Moshi, and has never pretended to be representing Zanzibar except as a person who was born in Zanzibar. This is definitely a case of desperation in looking for Zanzibari faces.

But all this still does not cover the substantive issue involved. It is well known that Foreign Affairs is a Union matter, and therefore any dealings with the UN has to involve the Minister of Foreign Affairs, even if the exact issue involves only one side of our Union. There are plenty of cases when this has been done about issues concerning non-Union matters of Mainland Tanzania. Therefore, it is not a favour to Zanzibar that once in a while the Ministry of Foreign Affairs has to take up the case when Zanzibar’s interests are concerned – it is our right, iof we are part of the Union. The same applies to the defence of Tanzania’s territorial boundaries, which include the now extended boundaries in the Indian Ocean – that is its responsibility.

But this does not mean that the Union Government therefore becomes the owner of all the resources within the territorial boundaries of Tanzania. The Articles of Union had defined 11 Union Matters that came under the Union Government, and the sea is not one of them. Since 1964, the Union Matters have been increased to 22, illegally according to Prof. Shivji, but even in this extended list you will look in vain for the blue seas. It is for this reason that Prof. Tubaijuka is the Minister of Lands, Housing and Human Settlements Development (all non-Union matters), but the seas are not included. Why she was sent and not the Minister of Foreign Affairs is for the Union President to explain.

Therefore, it has to be admitted that since the oceanic resources are not a Union matter, but are of vital concern for the islands of Zanzibar which are surrounded by the sea on all sides, the people of Zanzibar have a direct stake in what is decided about their resources. And here it is not enough to mention a few names, however, highly placed they may be, and say Zanzibaris were represented.

The same argument was used in the case of the first draft of the Constitution Bill. Former Speaker Samuel Sitta claimed that Zanzibaris were consulted, naming the Zanzibar Minister of Good Governance and the AG, but it turned out that they were asked to submit their recommendations, but adopted only two out of 13, and threw the rest in the dustbin, and then went on to add many more without consulting even the Zanzibar Government.

Don’t they ever learn?

What the Representative Ismail Jussa was trying to do was to teach our Big Brother another lesson, and the mainland-based Swahili newspaper dares to ask him to apologise to Prof Tubaijuka? I think it is Prof Tubaijuka and the Union Government that need to apologise to the people of Zanzibaris for trying once gain to take us for a ride. But as the old politician Hasan Nassor Moyo told Samuel Sitta, the new generation in Zanzibar is not the same as the old generation of the 1960s, and will not say ‘hewallah bwana.’

Abdul Sheriff

Monday 23 January 2012

Ombi la eneo la bahari kuu lapingwa- Shamhuna atakiwa kujiuzulu

Wajumbe wengi wa baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar wametaka Waziri wa Maji, Makaazi, na Nishari Zanzibar Juma Shamhuna ajiuzulu. kufuatia sakata la kushirikiana kinyemela na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanikisha ombi la kutaka nyongeza ya eneo la bahari ikijumuisha mipaka ya visiwa hivyo, pasipo kulishauri baraza hilo.Wito wa kutakiwa kujiuzulu kwa waziri huyo mkongwe visiwani Zanzibar unafuatia hoja binafsi iliyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa. Kufutia hali hiyo Sudi Mnette alizungumza na Issa Yusuf, Mwandishi kutoka Zanzibar kujua ni yapi yaliyojitokeza hadi wakati huu . Tafadhali bonyeza hapa.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamemtaka waziri wa nishati zanzibar Bw Ali Juma Shamuhuna ajiuzulu, pamoja na kupitisha azimio la kuitaka serikali ya zanzibar kuwasilisha mara moja barua ya kupinga kitendo cha serikali ya muungano wasilisha ombo kwa umnoja wa mataifa kuongezewa eneo la kiuchumui katuika bahari kuu (EEZ).

Azimio hilo limefuatia hoja binafsi iliyowasilishwa na Mwakilishi wa jimbo la Mji mkongwe Bw Ismail Jussa Ladu kuhoji uhalali wa serikali ya muungano kuwaslisha ombi hilo UN bila kuishirika Zanzibar kikamilifu.

Katika kukabiliana na serikali ya muungano, Jussa akitoa mapendekezo manne ambayo wajumbe wote wapiga kura kuridhia pamoja na pendekezo la tano linaloitaka baraza la mapinduzi zanzibar kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na baraza la wawakilishi mwezi Aprili mwaka 2009.

Mapendekezo ya Jussa ni kama ifuatayo: Kwamba seriklai ya zanzibar inadikie serikali ya muungano barua ya kusitisha mara moja mchakato wa maombi ya kutaka kuongezewa eneo la ukanda wa bahari kuu, na kwamba iwapo serikali ya muungano ikipuuza serikali ya zanzibar ipeleke ujumbe UN kutaka mchakato usimamishe.

Wiki iliyopita Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Waziri wake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Anna Tibaijuka iliwasilisha maombi katika umoja wa mataifa
kuomba eneo la ziada la maili 150 nje ya eneo la sasa la maili 200 za ukanda wa kiuchumi wa eneo huru la bahari.

Katika mchakato huo serikali ya muungano ilimshirikisha waziri wa nishati wa zanzibar Bw Ali Juma Shamuhuna kama alivyokiri mwenyewe kwa wajumbe wenzake ndani ya baraza la wawakilishi wiki iliyopita.

“Kama waziri ni serikali, basi zanzibar ilishirikishwa, na nilimpeleka msaidizi wangu kuniwakilisha, lakini kama serikali ni baraza la mapinduzi, basi hakushirikishwa katika jambo hili,” Shamuhuna alisema.

Kauli yake ilizuiwa maswali mengi kwa wajumbe wenzake miongoni mwa maswali hayo yakiwa ni inakuwaje jambo zito kama hilo Shamuhuna analibeba peke yake wakati baraza lilipitisha azimio linalotaka eneo lote la bahari la EEZ pamoja na maliasli ya mafuta liondolewe katika orodha ya muungano?

Serikali ya muungano haijajibu hadi leo kuhusu azimio la baraza, lakini viongozi wa seriklai ya muungano wamekuwa wakitoa kauli kwamza matatizo yote ndani ya muungano yatashughulikiwa.

Katika kuonesha kutoridhika na Shamuhuna, ndipo baadhi ya wajumbe wakamtaka waziri huyo ajiuzulu mwenywe au rais amtimue kazi kutokana na madai ya kuidhalilisha baraza baada ya kushirikiana na Prof Tibaijuka kupeleka ombi UN.

“Inakuwaje waziri anakuja hapa bila ya kuwa na msimamo juu ya maswala nyeti kama haya…waziri Shamuhuna inabidi ajiuzulu au rais amuwajibishe. Kama hatua haitochukuliwa, tunaweza kutumia kifungu cha 41 kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali…,” alisema mwakilishi Hamza Hassan Juma (CCM Kwamtipura).

Wajumbe wengine ambao walitoa kauli za waziwazi dhidi ya Shamuhuna na kumtaka aachiye ngazi ni Hija Hassan Hija (CUF- Kiwani), Mbarouk Wadi Mussa (CCM- Mkwajuni), Asha bakari makame (CCM wanawake), Omar Ali Shehe (CUF-Chakechake), na Rashid Seif Suleiman (CUF- Ziwani).

Ali Mzee Ali (CCM kuteuliwa) alitumia lugha ya kiprofesa pia kumlaumu Shamuhuna kwamba alijitia kitanzi mwenyewe katika kuelezea ushiriki wake katika swala ambalo bazara tayari limetolewa msimamo mwaka 2009.

Juhudi la mwanasheria mkuu wa serikali Othman Masoud kujaribu kutaka kumkingia kifua hazikufua dafu, kwani aliposema kwamba ni mapema kumhukumu mtu barazani alijibiwa kwa wajumbe kuguna, na baadae Jussa kumwambia kuwa wazanzibari ambao wamekuwa wakimheshimu sana wameanza kuvunjika moyo naye tangu alipopata wadhifa wa mwanasheria mkuu.

Hivi sasa kinachosubiriwa kwa hamu kubwa ni jibu la serikali ambalo makamo wa pili wa rais wa zanzibar Balozi Seif ali Iddi aliahidi wiki iliyopita kuwa katika kikao cha baraza la mapinduzi swala hilo litazungumzwa na kujadiliwa ikiwa pamoja na kuangalia athari ya ombi la serikali ya muungano la kutaka nyongeza ya EEZ kwa zanzibar.

Friday 20 January 2012

SMZ yatakiwa kutoa maelezo juu ya nyongeza ya masafa ya bahari

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akiendesha kikao cha baraza hilo kinachoendelea katika ukumbi wa Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kutoa taarifa katika baraza la mawaziri suala la Tanzania kuwasilisha ombi la nyongeza masafa ya bahari kuu kwenye Umoja wa Mataifa. Kificho alisema hivyo baada ya Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna kusema kwamba yeye kama wizara taarifa anayo hiyo lakini katika baraza la mawaziri hakuna taarifa ya jambo hilo iliyowasilishwa.

“Nakuomba waziri mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna kuleta taarifa hiyo baraza la mawaziri kwa ajili ya kuifanyia kazi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi” alisema Spika Kificho.

Kificho, aliwaambiwa wajumbe wa baraza hilo wasubiri na kuiagiza Serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa Zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa serikali ya Tanzania.

Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa Muungano kupeleka maombi hayo kwa Umoja wa Mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.

Aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo kwani suala hilo linahusu pande mbili na wananchi wa Zanzibar wana haki ya kujua mwenendo wa mambo katika nchi yao.

Awali Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alitoa taarifa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasilisha ombi katika umoja wa mataifa kuomba kuongezewa masafa zaidi ya maili mia mbili katika bahari kuu.

Jussa alitoa hoja ndani ya baraza la wawakilishi akiwataka wajumbe wa baraza hilo lijadili suala hilo kwa uwazi hasa kwa kuzingatia suala hilo lina athari kubwa kwa wazanzibari iwapo litafanikiwa.

Alisema hatua hiyo ya Serikali ya Muungano ni nzito na inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vizuri kwani waathirika wakuu huenda wakawa zaidi ni wazanzibari.

Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa jana katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
“Waheshimiwa wawakilishi hoja hiyo imetugusa sana wananchi wanzanzibari tunaomba muichangamkie, hatutaki mambo ya hewala bwana, hoja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusema kuwa Zanzibar imeshirikishwa kwa vile mjumbe mmoja kutoka Zanzibar anaonekana katika picha ya pamoja na mama tibaijuka katika kuwasilisha ombi hilo la umoja wa mataifa hatuitaki wala haitoshelezi” alisema Jussa katika kikao hicho cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huko Mbweni Zanzibar.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rasi, Ali Mzee Ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa na sio kuamuliwa na upande mmoja.

Suala la masafa ya bahari kuu limekuwa na mgogoro kati ya Zanzibar pamoja na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kiasi ya baraza la wawakilishi kupitisha azimio kuhusu jambo hilo, ambalo limeingizwa katika orodha ya kero za muungano.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Shamuhuna alisema kwamba wizara yake inayo taarifa kamili ya suala hilo ambapo alitakiwa yeye kufunga safari kwenda umoja wa mataifa kuwasilisha ombi hilo pamoja na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi wa jamhuri ya muungano Bi Anna Tibaijuka.

Hata hivyo Shamuhuna alisema kwamba kutokana na kutingwa na kazi nyingi alimtuma afisa wake kufuatana na ujumbe huo kwenda katika safari hiyo.

“Ujumbe huo kwa sasa upo katika umoja wa mataifa na tayari unatarajiwa kuwasilisha ombi hilo ambapo Tanzania baadaye itapangiwa tarehe kwenda kusikiliza shauri lao”.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar baadhi yao wamehoji hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupeleka maombi Umoja wa Mataifa (UN) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari na kutaka ufafanuzi wa suala hilo kuwasilishwa ndnai ya kikao hicho, hatua ambayo kimsingi Spika Kificho alikubaliana nao wajumbe hao na kuiagiza serikali kuwaislisha suala hilo barazani hapo.

Tanzania inawasilisha ombi la kuongezwa zaidi masafa ya eneo la bahari kuu kutoka mia mbili na sasa kufikiya mia nne, kama shauri hilo litakubaliwa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, anaelezwa kuwasilisha hoja hiyo na kuiwasilisha Umoja wa Mataifa (UN) huko New York Marekani.

Thursday 19 January 2012

Ripoti ya Kuzama kwa MV Spice Islander

Ripoti ya Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islanders 1 imependekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Mustafa Aboud Jumbe pamoja na wahusika wengine wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kutokana na uzembe waliofanya na kusababisha kuzama kwa Meli hiyo

Akitoa mapendekezo ya Ripoti hiyo leo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeyakubali mapendekezo ya ripoti hiyo na kusema itaiachia Mahaka na Jeshi la Polisi kutimiza wajibu wao

Dk.Abdulhamid amesema miongoni mwa watu ambao walibainika na makosa katika ajali hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Haji Vuai Ussi,Mkuu wa kituo cha usimamizi wa usalama wa vyombo vya baharini wa Shirika la Bandari,Usawa Khamis Said na Kaimu Mdhibiti wa Bandari ya Malindi Sarboko Makarani Sarboko.

Wengine ni pamoja na Wanahisa wa Kampuni inayomiliki meli hiyo Jaku Hashim Ayub ambaye ni Mwakilishi na Mbuge wa Jimbo la Muyuni,Salim Said Mohammed, Makame Hasnuu Makame na Yussuf Suleiman Issa.

Dk.Abdulhamid amesema wahusika wote waliotajwa katika ripoti hiyo ikiwa ni pamoja na Captain wa Meli hiyo Said Abdallah Kinyanyite na wasaidizi wake,Afisa usafirishaji wa Shirika la Bandari Hassan Mussa Mwinyi na Mkaguzi wa Meli wa Mamlaka ya Usafisiri wa Baharini Juma Seif Juma watachukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa yao

Mrajis wa meli Abdallah Mohammed Abdallah, Afisa Usalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Simai Nyange Simai, na wasimamizi wa watatu wa uingiaji wa abiria katika meli hiyo Yussuf Suleiman Issa,Shaib Said Mohammed na Juma Abdallah Hussein nao wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

Wengine ni Afisa Mkuu wa Mv.Spice Abdalla Mohammed Ali,Mhandisi Mkuu wa Meli hiyo Khamis Ahmada Hilika, Mabaharia wote wa Meli hiyo pamoja na Askari wa Bandarini waliokuwepo zamu katika kupanga abiria siku ya tukio ambao ni Sajent Jumbe Muhaji na Koplo Juma Abdulla.

Akizungumzia juu ya fidia kwa wahanga wa ajali hiyo Dk.Abdulhamid amesema jukumu la kuwalipa wahanga hao liko mikononi mwa wamiliki wa meli hiyo kwa mujibu wa sheria na kwamba vigezo vya kulipwa wahanga vitafuata utaratibu maalum uliowekwa ambapo kwa waliofariki watalipwa si chini ya Sh Milioni Kumi

Kwa waliopata ulemavu watalipwa asilimia 75% ya Fedha watakazolipwa waliofariki dunia ambapo waliokuwemo katika meli hiyo bila kupata ulemavu watapata asilimia 50% ya kiwango hicho.

Kuhusu fedha za michango ya maafa ambazo zimetolewa na taasisi mbalimbali Dk. Abdulhamid amesema fedha hizo zitagawiwa kwa wahusika chini ya utaratibu maalum utakaowekwa na Mfuko wa Kamati ya maafa uliopo chini ya Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais

Aidha Dk.Abdulhamid alisema ripoti hiyo itawekwa wazi na kupatikana katika mitandao na Maktaba kuu ili wananchi waweze kuisoma.

Ripoti ya Tume hiyo iliundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kufuatia kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islanders 1 tarehe 9/09/2011 katika Mkondo wa Nungwi kuelekea Pemba ambapo inasadikiwa ilikuwa na abiria 2470 na tani kadhaa za mizigo

Wapalestina wajifunze kwetu, nasi tujifunze kutoka kwao

Ahmed Rajab
“JITAYARISHE kunyanyaswa na kudhalilishwa,” ndivyo alivyoniambia sahibu yangu mmoja mwenye asili ya Kipalestina kama miaka miwili iliyopita. Alikuwa akiniaga baada ya kunikirimu kwa chakula cha usiku nyumbani kwake mjini Amman, Jordan. Alihisi lazima anionywe hivyo kwa vile siku ya pili alfajiri nilikuwa ninaelekea Israeli kwa mara yangu ya mwanzo.

Nilipanga kuingia Israeli kwa kuivuka Daraja ya Allenby au kama inavyoitwa siku hizi Daraja ya Mfalme Hussein, niweke maskani mjini Jerusalem kwa wiki nzima ili niweza kuizuru miji mingine ya Israeli na halafu nivuke mpaka wa Eratz na kuingia Ukanda wa Gaza kwa ziara ya siku mbili.

Sikutaka kukaa sana Gaza kwa sababu kulikuwa moto. Wiki sita kabla, mabomu ya Israeli yaliitwanga Gaza, yakazifanya shule na majumba yawe vifusi na kuwaua Wapalestina chungu nzima. Na rafiki yangu wa Amman aliponiambia nijitayarishe kunyanyaswa alikusudia kunyanyaswa na ‘vijijanajeshi’ vya Kiyahudi kwenye kivuko cha mpakani cha Eratz cha kuingilia Gaza. Hayo yalinikuta.

La kuudhi zaidi ni kwamba wanyanyasaji ni vitoto vidogo unaweza ukafikiri kama vina umri wa miaka 16. Lakini wana silaha nzito na ufedhuli umewajaa kwenye ndimi zao. Kwa hivyo wao wanakuwa mabwana — ingawa wengine ni wasichana — na wewe unakuwa mtoto.

Kwa hakika, niliyaona mengi Israeli. Nilizifuata nyayo za Yesu Kristo, nikatembea kwenye Mji Mkongwe wa Quds, yaani Jerusalem, nikaswali Ijumaa mbili kwenye msikiti wake wa Al Aqsa. Kiguu na njia nikaizuru miji ya Tel Aviv, Jaffa, Sderot na Be’er Sheva ambao ni mji mkubwa katika Jangwa la Negev.

Niliiona Israeli kuwa ni nchi ya kuta, vizuizi, vikwazo, vipingamizi na vikaratasi vya ruhusa na vibali vya kila aina wanavyotakiwa Wapalestina wawe navyo.  Daima wanadhalilishwa kwa kila namna ya idhilali. Nyumba zao zinabomolewa, wanafukuzwa makwao na lengo la Wazayoni mjini Jerusalem ni kuufanya mji mzima uwe na sura ya Kiyahudi. 

Wapalestina hawaruhusiwi kujenga Jerusalem ya Magharibi kwa Wayahudi lakini Wayahudi wanaruhusiwa kujenga Jerusalem ya Mashariki kwa Wapalestina. Ajabu ni kwamba juu ya yote hayo Wapalestina wanaendelea kucheka, kutabasamu na wanaweza kufanya dhihaka.

Siku moja nilialikwa kwenye Bunge la Israel, Knesset, na Dakta Dov Khenin, Mbunge wa chama cha Hadash, chama pekee cha Wayahudi na Waarabu na ambacho ni cha mrengo wa kushoto na chenye wabunge wanne. Khenin hali kadhalika ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha Israel, Maki.

Ofisini mwake bungeni Khenin ametundika picha ya Che Guevara. Nilipomwambia kwamba tathmini yake ya mustakbali wa mzozo wa Israel na Wapalestina inakosa rajua, ikiyaona mambo yote kuwa hayana mbele wala nyuma, yamejaa misiba na mashakil alinijibu kwa kumnukuu mwanafalsafa wa Kitaliana, Antonio Gramsci.

Alinikumbusha kwamba Gramsci akitaka pawepo na ‘pessimism of the intellect, optimism of the will’ yaani pawepo na ukosefu wa rajua ya akili, (lakini) pawepo na msimamo wa kutegemea mazuri katika dhamira.’ Gramsci akitaka hivyo ili ukosefu wa rajua uwe ni kichocheo cha kuchukuwa hatua, na msimamo wa kutegemea mazuri uwe ni ukakamavu wa kuamini kwamba hatua hiyo italeta mageuzi ya maana hata pakiwa na nakama. 

Mbunge huyo alinisikitikia kwamba ubovu wa Israeli ni kuwa hakuna mlingano wa aina yoyote kati ya Waarabu na Wayahudi. Jamii hizo mbili zimegawika vibaya. Hajakusudia Wapalestina na Wayahudi lakini Waarabu wa Israel na Wayahudi wao.

Si tu kwamba Waarabu na Wayahudi wanazungumza lugha tofauti lakini hata misamiati wanayoitumia ni tofauti, dhana (concepts) zao pia ni tofauti katika siasa hata katika utamaduni na katika maingiliano yao ya kijamii ambayo ni madogo mno na pia kwa namna wanavyoangaliana.

Kwa ufupi, pande zote mbili zina hofu. Wayahudi wanatishwa na Waarabu; Waarabu nao wanawaogopa Wayahudi. Lakini aliniambia alitaka nitambuwe kwamba 'Israeli sio tu pahala pa kukutania matatizo lakini pia ni pahala penye uwezekano mwingi,’ yaani kuna mengi yanayoweza kutendeka.

‘Je, Israeli ni dola la ubaguzi wa kikabila?’ Swali hilo nilimuuliza mwandishi habari maarufu Gideon Spiro kwenye mgahawa wa Bookworm Café mjini Tel Aviv. Bookworm, kwa hakika, ni duka la vitabu lakini lina mgahawa na ni mahali ambapo Waisraeli wa mrengo wa kushoto hupenda kukutana.

Sijui nini kiliniandisi nimuulize Gideon swali hilo kwa vile jibu nilikuwa nalo. Labda nikitaka kushangazwa, kumsikia Mwisraeli mwenye siasa za mrengo wa kushoto akiutetea msimamo wa Serikali yake kuhusu suala hilo kwa kukana kwamba dola lao si la kibaguzi.

Siku chache kabla nilimuuliza mwandishi mwingine Wakiisraeli mwenye mawazo ya wastani na jibu alilonipa halikuwa na shaka yoyote. Alisema kwamba Israel ni dola la kibaguzi.

Lakini Gideon, mzee wa miaka 77, akiwa na tabasamu iliyokunjika ikichezacheza kwenye ndimi zake na macho yake yakimetameta, alilipima jibu lake: ‘Ni mfumo wa utawala wa kimbari (ethnocracy)’. Akasita, akapiga fundo la kahawa aipendayo aina ya Cappuccino iliyojaa povu la maziwa na akaendelea kunieleza hivi:

‘Kwa Wayahudi ni utawala wa demokrasia yenye mipaka, kwa Wapalestina walio kwenye maeneo yanayokaliwa na Israeli ni utawala wa udikteta wa kijeshi na kwa Waarabu wa Israeli ni utawala wa demokrasia yenye ubaguzi. Lakini kwa Wayahudi na Waarabu pamoja utawala huo si wa demokrasia,’ alisema.

Gideon Spiro aliongeza kunena kwamba hata miongoni mwa wenyewe kwa wenyewe Wayahudi wanabaguana. Wayahudi wenye asili za kizungu ndio walio tabaka la juu lenye kutawala na Wayahudi waliosalia, hasa walio weusi, wako chini, wa mwisho, fungu la Mungu.

Nilipoingia Ukanda wa Gaza sikuona kitu ila maangamizi na maafa na mji uliovunjwavunjwa na kuangushwa kwa mabomu ya Waisraeli. Ijapokuwa umasikini umezagaa na watu wengi wanaishi chini ya ule uitwao mstari wa ufukara, hata hivyo niliwasikia wakiangua vicheko na niliziona nyuso zao zikiwa na bashasha.

Nilipata wasaa wa kwenda Ramallah, kwenye Ufukwe wa Magharibi, kwa siku moja. Nililizuru kaburi la Yasser Arafat na niliona ushahidi wa jinsi Wapalestina walio ughaibuni wanavyomimina fedha kwao na kukujenga. Hilo ni funzo moja kwetu sisi.

Jingine lililonivutia Ramallah ni namna watu wenye dhamana katika utawala wa huko walivyobobea katika fani zao mbalimbali. Nina hakika kwamba watapopata uhuru wao na kuondoshewa bughdha za 'kukaliwa' na Waisraeli basi watapiga hatua kubwa mbele kuishinda Israeli katika muda wa miaka 20 tu ijayo, juu ya rushwa iliyosambaa.

Katika kutafakari kwangu baada ya kuyazuru maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israeli niliona kwamba kuna mingine tunayoweza kujifunza kutoka kwa Wapalestina na yapo ambayo Wapalestina wanayoweza kujifunza kutoka kwetu.

Kwa upande wetu ni kuwa umma unaposema kwa sauti moja kuwa umechoshwa watawala huwa hawana budi ila kuridhia. Hivyo, umma unapovinjari unakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko.

Pili, ni kwamba mabavu au ubabe hauwezi kudumu milele. Huu ni ukweli wa kihistoria. Utawala wa Arafat uliandamwa na kashfa za rushwa na ubadhirifu. Hata mkewe Arafat, Suha, aliingizwa kundini kuwa miongoni mwa waliokuwa wakiramba asali.

Hatimaye umma ulivinjari na wakuu wa Mamlaka ya Palestina akiwemo Waziri Mkuu, Ahmed Qurei walijiuzulu. Lilipoingia wimbi la kujivua gamba waliingia walokuwemo na wasiokuwemo, kila mmojawao akibeba dhamana ya kuwa ndani ya Serikali iliyoshindwa kutekeleza matarajio ya wananchi. Huko ndiko kuwajibika.

Tatu, tunaweza kujifunza kutokana na maendeleo ya kijamii, hasa Ukanda wa Gaza ambako pamoja na vikwazo na hali ngumu inayotokana na ukandamizaji unaoendelea wa dola ya Kiyahudi, utawala wa chama cha Hamas bado unaungwa mkono kwa vile unawajali na kuwafaraji walalahoi.

Lile ambalo Wapalestina wanaweza kujifunza kutoka kwetu ni haja ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama iliyoko Zanzibar. Serikali kama hiyo haikupatikana Palestina tangu chama cha Hamas kilipokishinda chama cha Fatah katika uchaguzi wa mwaka 2006 huko Gaza na kukilazimisha chama cha Fatah kuhodhi mamlaka ya utawala katika Ufukwe wa Magharibi pekee.

Licha ya makubaliano yaliyofikiwa mwishoni mwa mwaka jana jijini Cairo kati ya pande hizo mbili serikali aina hiyo bado haijapatikana. Hivyo panakosekana msimamo mmoja wa Wapalestina dhidi ya Israeli.

Kufanikiwa kwa Palestina mwaka jana kujiunga na Shirika la  Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) 2011, kunaibua swali la kwa nini  iwe ni vigumu kwa Zanzibar, licha ya kuhudhuria vikao mbalimbali  vya  shirika hilo mjini Paris?

Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikipigania kuwa na uwakilishi katika jumuiya kadhaa za kimataifa kama Jumuiya ya Nchi Za Kiislamu  na hata  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la dunia FIFA. Juhudi hizo zimekwama hadi sasa. Pengine serikali imeshindwa kulivalia njuga vya kutosha suala hilo.

Kuna usemi kwamba katika siasa kila kitu kinawezekana. Ikiwa Misri imefikia amani na Israeli, kwa nini pasiwe na uwezekano wa Hamas kukaa pamoja na Israeli kuendeleza mchakato wa kupatikana amani?

Na kwa Tanzania, kwa nini tusiweze siku moja kushuhudia Tanganyika na Zanzibar zikiingia katika enzi mpya na kuwa na uhusiano mpya uliojengeka juu ya msingi wa haki na usawa kati ya nchi mbili zilizo huru? Yote hayo yanawezekana kwani uamuzi wa haki na wenye nguvu ni ule wa umma na sio wa viongozi.
Raia Mwema

Wednesday 18 January 2012

RC Ataka Mchakato Katiba Ujadili Nafasi ya Zanzibar

na Haji Nasor, Pemba

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi amewataka wananchi kisiwani humo kujadili kwa kina nafasi ya Zanzibar kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati utakapofika wa kutoa maoni juu ya kuandikwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakapofika.
Alisema ili kulifanikisha hilo wakati huo tume itakapopita kukusanya maoni, waache woga, jazba, na wasiwasi na badala yake wajitarishe vyema kwa kuzungumzia kwa kina nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu huyo wa mkoa, alitoa kauli hiyo ukumbi wa mikutano wa ZSSF, Chake Chake alipofungua mdahalo wa kuwajengea uwezo wananchi juu ya kutoa maoni ya kuandikwa kwa katiba mpya ya Tanzania wakati tume itakayoteuliwa itakapopita.
Dadi alieleza kuwa jazba, woga na fujo hazitosaidia kutoa maoni yao kwenye mchakato huo na badala yake wawe makini kuyaelezea kwa kina mambo wayatakayo kwenye katiba hiyo, ili kuona Zanzibar inafaidika mara dufu kwenye Muungano huo.
Aliendela kueleza kuwa, Katiba katika taifa lolote lile ulimwenguni ndio nguzo kuu na dira kwa maendeleo ya wananchi husika, hivyo katika uandikaji wa Katiba hiyo ni vyema kwa wananchi hao kujipanga ili kupata katiba waitakayo.
“Wananchi hamnabudi kuhakikisha wakati ukifika wa kutoa maoni yenu muwe makini na msisahau kuwa katiba ndio dira na msingi mkuu wa kufikia maendeleo katika taifa hili’’,alifafanua Dadi.
Katika hataua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa wa Kaskazini Pemba amewataka wananchi kuifahamu vyema katiba ya sasa na mambo yaliyomo, hilo litasababisha kuwa na mchango mzuri kwenye mchakato wa kukusanya maoni kuelekea kuandika Katiba mpya.
Mapema akitoa maoni yake juu ya mambo yanayopaswa kuingizwa kwenye katiba mpya mwanasiasa, Said Soud alisema kuwa ni vyema katiba hiyo mpya kubanisha juu ya kuwepo kwa serikali tatu ili katika mgawanyo wa rasilimali za muungano kuwepo kwa uswa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muungano.
Soud alieleza kuwa Tanzania ilipaswa iwe na katiba tatu moja ikiwa ya Zanzibar, Tanganyika, na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ikijumuisha pande mbili za Muungano huo.
Naye Nassor Harith alisema katiba ijayo ni vyema ikaweka mgawanyo sawa wa misaada na rasilimali za Muungano ili nayo Zanzibar ineemeke na matunnda ya Muungano huo na sio kama ilivyo sasa.
Aidha wananchi wengine waliochangia kwenye mdahalo walisema, ni vyema kabla ya kupita kwa tume maalum wananchi wakaendelea kuelimishwa juu ya njia bora na sahihi ya kutoa michango yao wakati tume hiyo itakayoteuliwa itkapoanza kazi rasmi.
Nae Mwenyekiti wa mwemvuli wa Jumuia zisizo za Serikali Kisiwani Pemba, Abubakary Mohamed, ambao ndio walioandaa mdahalo huo alisema kuwa, wanajipanga ili kuhakikisha wanagawa kopi za katiba kwa wananchi wa Pemba ili kuzisoma na kuzifahamu.
Aliongeza kuwa pamoja na ahadi hiyo ni vyema kwa wale walio na uwezo kuzitafuta katiba zote mbili kuzisoma na kuzifahamu ili wakati utakapofika waweze kuchangia mambo wanayoyafahamu.
Mdahalo huo ambao uliwashirikisha wananchi wa makundi mbali mbali ikiwa ni pamoja na wasomi, wananchi wa kawaida, wenye ulemavu na viongozi wa jumuia za kiraia ulikuwa na lengo la kuwajengea uwezo wananchi ili kuwaweka tayari wakati utakapofika wa kutoa maoni wawe na uhakika.
 

Saturday 14 January 2012

Kamati kuu CCM yampitisha Raza jimbo la Uzini

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichokaa jana Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kuchagua mgombea atakayekiwakilisha Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mdogo wa Uwakilishi katika Jimbo la Uzini,

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza Daramshi kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini mkoa wa kusini Unguja. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.

Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.

Alisema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.

Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Khamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari, Septemba 23, mwaka jana.

Kuhusu minong’ono kwamba Raza ana utata katika uraia wake, Nape alisema Kamati Kuu imelitaza jambo hilo kwa makini lakini haikuweza kulipa uzito wa kumyima Raza nafasi ya kugombea kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa kuthibitisha hilo.

“Bado tunao muda wa kutosha, kama yupo mwenye ushahidi wa kutosha kuhusu hili anaweza kuleta ushahidi, ukiwa na uzito hatutaupuuza”, alisema Nape.

Friday 13 January 2012

Tuwacheni Uvyama kwenye sherehe za kitaifa

Wafuasi wa CCM wakipita wakati wa sherehe za kutimiza miaka 48 ya mapinduza ya Zanzibar
Wafuasi wa CUF wakipeperusha bendera za chama chao kwenye sherehe hizi
Na Aby 13/12/2012
Kwa kweli huu ni utaratibu unaokera hasa katika kipindi hichi ambacho tunahitaji umoja wa Wazanzibari kuliko wakati wowote mwengine. Utaratibu huu wa kuingiza taswira za vyama katika sherehe za kiserikali inaonesha kwa kiwango gani wazanzibari hatujawa tayari kuacha tofauti zetu za kivyama na kuelekeza nguvu katika kujenga umoja ambao unahitajika kuweza kupambana na upande wa pili wa muungano katika kudai haki na maslahi ya Zanzibar iliyonyanganywa miaka 48 iliyopita.
Bali ndio kwanza tunaleta vitu ambavyo vitatugharimu kwa kiasi kikubwa, na hii zaidi inaonesha kuwa watu ambao wako katika level ya katikati kwenye vyama ndio ambao hawataki kubadilika, ukiangalia jukwaa kuu utaona viongozi wote wako neutral katika kivazi na hata ukifuatilia katika mazungumzo katika hutba zao
Haya mambo tusipokuwa makini ndiyo yatakayotupelekea kupoteza muelekeo na tukija tukipoteza mara hii basi zanzibar ndiyo itakuwa imeangamia milele, umoja unahitajika hasa tukijuwa kuwa kuna watu ndani yetu hawaipendelei Zanzibar katika kujinasuwa katika muungano usio na maslahi kwa wazanzibari, hii ilizidi kunishtuwa wiki iliyopita kuona uongozi wa juu ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa GNU unapingana kwenye jambo kubwa la maslahi ya Taifa, mmoja anasema tuwe na muungano wa serikali tatu na pia urais wa Tanzania uwe wa kupokezana badala yake mwengine kwa maslahi yake binafsi na hayo maslahi ya vyama ambayo ndiyo yaliyotufikisha hapa ana-act kinyume chake hii ni kutusaliti wazanzibari kwani nyinyi viongozi wetu tulitegemea muwe mbele katika kuungana na pia iwe ni sababu ya kutuunganisha sisi katika kudai haki ya Zanzibar katika katiba mpya.
Tunawaomba viongozi wetu wakemee suwala hili ili kwenye sherehe za kitaifa kuwe na picture sahihi ya sherehe zinazowakilisha taifa badala ya kuwa ukumbi wa kuonesha tofauti za vyama vyetu kwani vyama havikuwepo, vimekuja na baadae vitaondoka, lakini Zanzibar na wazanzibari ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo, tuwajengee misingi mizuri vizazi vyetu ili wasije wakaja kutulaumu kama sisi tunavowalaumu waliwotutangulia

Thursday 12 January 2012

Mshikamano wadhihirika Pemba, Unguja

SHEREHE za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan jana zilifana huku zikionesha kurejea kwa mshikamano mkubwa wa wananchi wa Unguja na Pemba,
ambao sasa wameweka pembeni itikadi za vyama na kuweka utaifa mbele.
Sherehe hizo zilifanyika huku Wazanzibari wakiunganishwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayotokana na maridhiano ya kisiasa ambayo lengo lake ni kuondosha siasa za chuki na uhasama.
Mbwembwe za viongozi wa kitaifa wakati wakiingia katika Uwanja wa Amaan pamoja na
gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama, ni miongoni mwa matukio muhimu ambayo yalifanikisha na kupamba sherehe hizo.
Wananchi walishangilia viongozi wao wa kitaifa akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed
Shein, ambaye aliingia uwanjani akisindikizwa na pikipiki za askari wa Polisi zaidi ya 10.
Lakini aliyevutia zaidi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jakaya Kikwete, ambaye alipokewa kwa kupigwa Wimbo wa Taifa.
“Ni sherehe ambazo zinatakiwa kuendelea kusherehekewa kila mwaka kwa lengo la vizazi vijavyo kujua na kutambua tunatoka wapi na tunakwenda wapi,” alisema mmoja wa waasisi wa
Mapinduzi, Hassan Nassoro Moyo, wakati akizungumza na gazeti hili.
Moyo alisema kauli hiyo kufuatia baadhi ya watu wakipinga kufanyika kwa sherehe hizo
ambazo hutumia fedha nyingi, huku wananchi wakihitaji huduma muhimu ambazo hazipatikani.
Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya miaka 48 zimetumia jumla ya Sh milioni 700 kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Aidha, wananchi walijitokeza mapema na kuingia Amaan saa moja asubuhi bila kujali ukali wa
jua.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na wananchi wengi kutoka Pemba ambao walifika hapa kwa usafiri wa boti na meli.
“Sherehe zimefana kweli kweli huku zikionesha mshikamano wa wananchi wa Unguja na
Pemba, ambao sasa wameungana na kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa,” alisema Juma Jongo.
Akihutubia umati uliojumuika Amaan, Dk. Shein alisema malengo ya Mapinduzi ya mwaka
1964 yataendelea kutekelezwa ikiwamo kuwapatia wananchi huduma muhimu na maendeleo bila ubaguzi.
Alisema malengo hayo ni muhimu kutekelezwa na kusimamiwa kikamilifu, kwani ndiyo yaliyofanya wananchi wa Zanzibar kufanya mapinduzi na kumwondoa mkoloni.
Aliongeza kuwa huduma za maji safi na salama, elimu kwa watoto wote wenye uwezo wa
kwenda shule na huduma za afya na kutunza wazee wasiojiweza, zitaendelea kutolewa.
Alisisitiza umoja na mshikamano wa wananchi wa Unguja na Pemba akisema ndiyo siri ya
mafanikio yote ya utulivu wa kisiasa, huku akisisitiza pia kuimarishwa kwa Muungano na kupatiwa ufumbuzi wa kero zilizopo kupitia Kamati ya Pamoja chini ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilali.
Akifafanua kuhusu hali ya uchumi na changamoto zinazoikabili Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Dk. Shein alisema hali ya uchumi ni ngumu kutokana na mfumuko wa bei za vyakula
na kuongezeka kwa vitendo vya uharamia.
Alisema kasi ya ukuaji wa uchumi imefikia asilimia 6.5 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.7
mwaka 2009 na ukuaji mdogo wa sekta ya viwanda na huduma ambapo mwaka 2010 ukuaji wa
huduma ulifikia asilimia 8.7.
Kwa upande wa mfumuko wa bei alisema ni tatizo kubwa na umekua kwa asilimia 6.6 kwa
Januari mwaka juzi na mwaka jana hadi asilimia 18.7.
Hata hivyo, alisema SMZ imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na matatizo hayo ikiwamo
kupunguza ushuru kwa bidhaa muhimu za vyakula ukiwamo mchele na unga wa ngano.
Alisema SMZ inaendelea kutekeleza sera na mapinduzi ya kilimo katika uzalishaji wa chakula
na kupunguza kutegemea kuagiza bidhaa muhimu ukiwamo mchele kutoka nje.
Kuhusu mafanikio, aliitaja sekta ya miundombinu ya barabara, kwamba imeleta mapinduzi
makubwa ya uchumi na sasa barabara nyingi za vijijini zipo katika hali nzuri kwa kiwango cha
lami.
Alisema taasisi za ukusanyaji wa kodi ikiwemo Mamlaka ya Mapato (TRA) na Bodi ya Mapato
(ZRB) zimefanya vizuri na kuvuka lengo la kukusanya mapato kwa asilimia 10 kutoka Sh bilioni
171.68 hadi Sh bilioni 181.48.
Mapema aliwataka wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao katika
mchakato wa marekebisho ya Katiba wakati ukifika.
Source: Habari Leo

Tunahitaji mapinduzi ya uchumi, maisha Z’ bar

Thursday, 12 January 2012 10:00
LEO ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Siku hii ni ya kukumbukwa kwani ni siku ambayo wananchi wa Zanzibar waliuangusha utawala wa Kisultani ambao ulikuwa ukiwakandamiza na kuwanyonya katika nchi yao.

Tunachukua fursa hii kutoa pongezi kwa Wazanzibari na Watanzania kwa jumla kwa kuadhimisha siku hii muhimu, lakini pongezi zaidi kwa kudumisha amani na udugu miongoni mwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa miaka yote 48.

Sote tunafahamu kwamba safari ya miaka 48 aliyoianzisha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, haikuwa rahisi kwani kumekuwapo changamoto nyingi za hapa na pale kiasi cha kutishia umoja wa kitaifa wa Wazanzibari.

Yote hayo yalikuwa mapito, lakini jambo kubwa la muhimu hii leo ni kujadili jinsi ya kusonga mbele na kuhakikisha haturudii makosa ambayo kutokea kwake kulisababisha matatizo mengi, ikiwa ni pamoja na kugharimu maisha ya Watanzania wenzetu kadhaa.

Mara nyingi maadhimisho ya aina hiyo, hasa ya kiserikali hutumika kwa kuandaa sherehe na shamrashamra za hapa na pale, huku wengi wakizitumia kwa mapumziko nyumbani ambako hutulia na familia zao.

Sisi wa Mwananchi tunaiona sikukuu hii ya kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kuwa, ni siku ya kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakokwenda kwa maana ya kila mmoja wetu kujiuliza ni upi mchango wake katika miaka yote hiyo.

Lakini pia ni wakati wa watawala waliopo sasa kubaini changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii ambazo zimekuwa ni vikwazo vinavyowazuia Wazanzibari kusonga mbele kimaendeleo kiasi cha kuwafanya baadhi yao kuishi katika maisha ya umasikini na ufukara wa hali ya juu.

Tusiwe na choyo kwa vizazi vijavyo, bali tuwe na upendo na ukarimu kwa kutumia siku hii, kutafakari na kuchukua hatua za dhati dhidi ya matatizo yaliyopo, tukiutazama ustawi wa Zanzibar miaka 48 ijayo kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu zetu.

Leo tunaiona Zanzibar na kuifurahia kutokana na msingi uliojengwa na wasisi wake, ambao walikuwa na mtazamo kwamba baada ya miaka 48 tutakuwa na nchi yenye asali na maziwa.

Lakini inawezekana pale walipoachia wao, tuliopo leo tumeshindwa kupiga hatua ya kuridhisha na ndiyo maana bado kuna malalamiko kutoka kwa Wazanzibari ambao hawaridhishwi na mambo yanavyokwenda.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na vyama vya CCM na CUF kwa pamoja ina changamoto kubwa ya kujiuliza kwamba, katika idadi ya miaka inayokaribia nusu karne Wazanzibari wamevuna nini au wana nini cha kujivunia?

Pia tujiulize mapinduzi yalikuwa na maana gani Januari 12, 1964 na leo hii 2012 miaka 48 baadaye, mapinduzi haya yana maana gani kwa Wazanibari? Bado yana maana ile ile ya miongo yapata mitano iliyopita au maana yake imebadilika?

Kadhalika tujihoji, kama lengo la mapinduzi lilikuwa ni kuwakomboa wanyonge kutoka katika minyororo na utumwa chini ya utawala wa Kisultani, je lengo hilo limefikiwa? Hivi leo  minyororo na utumwa wa Wazanzibari ni nini au ni upi?

Maswali hayo na mengine mengi yanapaswa kupatiwa majibu kutoka kwa viongozi wetu wa sasa. Tena majibu sahihi ambayo siyo tu kwamba yanawatia moyo wananchi wa Zanzibar, la hasha, bali majibu ambayo utekelezaji wake utaleta nafuu kwa maisha yao, sasa na siku zijazo.

Kwa jinsi hali ilivyo sasa, tunahitaji Mapinduzi mapya Zanzibar na haya si mengine bali ni mapinduzi ya kiuchumi yatakayomwezesha kila Mzanzibari kuishi maisha bora yanayolingana na thamani ya utu wake. Inawezekana iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake. Mungu ibariki Zanzibar.
Source: Mwananchi

Akina Professor Jay, Sugu na uongozi wa taifa

Ahmed Rajab
JUZI nilikuwa nikiangalia mahojiano katika stesheni moja ya televisheni ya lugha ya Kifaransa. Aliyekuwa akihojiwa alikuwa Youssou N’Dour, mwimbaji maarufu wa Senegal aliyetangaza kwenye mahojiano hayo kuwa ataugombea urais wa nchi yake katika uchaguzi utaofanywa Februari 26, mwaka huu.
Katika mahojiano hayo mwimbaji huyo, mwenye umri wa miaka 52, alitamka haya: “Mimi sikusoma lakini nimezingatia yaliyofanywa na waliosoma tangu uhuru nikaingiwa na mori wa kutumia haki yangu na kutoa mchango wangu kwa wananchi wa kawaida. Nimetafakari nikaona nina wajibu wa kuingia katika kinyanganyiro hiki.”
Ingawa mwaka jana Chuo Kikuu cha Yale kilichoko Marekani kilimtunukia shahada ya heshima ya udaktari wa muziki  N’Dour,  kama alivyosema mwenyewe, si mtu aliyesoma. Sana sana amesoma katika shule ya msingi na hakuingia shule ya sekondari.
Alipotimiza umri wa miaka 12 tayari alikuwa akipanda kwenye majukwaa kuwatumbuiza mashabiki wa muziki.  Kabla ya kuwakusanya wanamuziki kadhaa walio na ustadi katika fani hiyo na kuanzisha kundi lake la Étoile de Dakar (Nyota ya Dakar), N’Dour alikuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la Orchestra Baobab na kabla ya hapo Star Band.
Ingawa hakusoma hivyo Youssou N’Dour alitumia kipaji chake kisicho kifani kwa kusoma katika shule ya maisha na kuyafanya maisha yake yawe kivutio. Tangu aanze kujitafutia riziki kwa kuimba ameutumia muziki kuwa ngazi ya kujijenga, sio yeye tu bali pia Waafrika wenzake na taifa lake. Leo hii amefanikiwa kuitangaza Senegal katika ulimwengu wa burudani na kuipatia sifa duniani. 
Ameshirikiana na waimbaji walio wanaharakati maarufu kama Bob Geldof na Bono kusaidia katika kampeni za kupambana na maafa, tangu ya ukame, njaa, magonjwa, umasikini na madeni ya nchi za Magharibi yanayobebwa na nchi zetu.
Pamoja na yote hayo, N’Dour ameanzisha miradi binafsi huko kwao Senegal ya studio ya kisasa ya muziki, steshini ya redio, nyingine ya televisheni na gazeti, akiwaajiri jumla ya vijana wasiopungua 4,000.
Wengi wanajiuliza ni wanamuziki wangapi maarufu barani Afrika  walioweza kufanya alau nusu ya aliyofanya N’Dour. Jibu hakuna.
Kwa muda wa takriban robo karne tangu akiasisi kikundi chake hakuna mwanamuziki wake hata mmoja aliyemuacha mkono. Hili pia ni la kupigiwa mfano. Ni jambo linalodhihirisha  uadilifu wake N’Dour kwa wale anaowaongoza, iwe kimuziki au kibiashara.
Kujitokeza kwake kuwania urais kumeshaanza kuwatia kiwewe wanasiasa wakongwe tangu Rais Abdoulaye Wade, mwenye umri wa miaka 86, hadi baadhi ya wapinzani wake.
Hofu ya Wade, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kidemokrasia cha Senegal, sio kwamba N’Dour ataweza kushinda moja kwa moja katika duru ya mwanzo, la  hasha. Kinachomtia wahka ni umaarufu wa N’Dour unaoweza kusababisha uchaguzi kuingia duru ya pili. Hiyo ni duru ambayo Wade anaihofia. Anahofia kwamba endapo uchaguzi utaingia duru hiyo na wapinzani wake wakashikana kumuunga mkono mgombea mmoja basi hatoweza kufua dafu.
Nilikutana na Wade kwa mara ya kwanza mwishoni mwishoni mwa mwaka 1999, nilipokuwa nikihariri Jarida la Africa Analysis na miezi kadhaa kabla hajachaguliwa kuwa Rais. Aliletwa ofisini mwangu na Balozi Gaby Sar, aliyekuwa Balozi wa Senegal mjini  London, jambo lililonifanya nimpe heko balozi huyo kwa ustaarabu wake wa kisiasa na Serikali yake kwa uvumilivu wake. Ni nadra kumuona balozi wa kiafrika akimhudumia kiongozi wa upinzani, akimpangia miadi na akifuatana naye na serikali yake isikereke kwa hayo. 
Wakati nilipoonana naye, Wade alikuwa amekwishagombea urais mara nne na mara zote akibwagwa na Rais Abdou Diouf. Nilipokutana naye nilimuonea huruma na sikudhania katu kwamba miezi michache tu baadaye, atatimiza ndoto yake na hatimaye kumshinda Diouf. Nilimuona kuwa ni mtu myenyekevu na haikunipitia kwamba ana ujeuri anaouonyesha sasa.
Wade ni mtu aliyesoma; tena amesoma sana. Kwa hakika ni msomi kwani kuna tofauti kati ya mtu aliyesoma na msomi. Unaweza ukasoma masomo ya juu na kupata mashahada ya juu na usiwe msomi. Na unaweza kuwa msomi bila ya kupata cheti hata kimoja cha masomo.
Wade ana shahada mbili za udaktari — wa sheria na wa uchumi.  Alikuwa akifundisha sheria Ufaransa na nchini Senegal aliwahi kuwa mkuu wa kitivo cha sheria na uchumi katika Chuo Kikuu cha Dakar.
Alipokuwa kiongozi wa upinzani, Wade alikuwa akiukosoa sana  utawala wa chama cha Kisoshalisti wakati wa muasisi wake, Léopold Senghor na baadaye wakati wa uongozi wa Diouf. Nadhani Senghor alimng’amua mapema Wade kwani akimwita ‘sungura’.
Siku hizo Wade alikuwa akipigania sana utaratibu wa rais kutawala mihula miwili tu. Lakini katika kuhakikisha anakuwa tofauti na wengine akataka kipindi kiwe cha miaka saba badala ya mitano kama alivyofanya Paul Kagame, nchini Rwanda. Wade aliyeahidi kuiheshimu Katiba sasa ameivunja ahadi yake na ameibadili Katiba.
Alipoulizwa na mmoja wa wananchi wenzake mbona amekwenda kinyume cha ahadi aliyoitoa alipoingia madarakani alijibu: “Kweli niliyasema hayo wakati ule, lakini sasa nimebadili nia; tatizo likowapi ?”
Tatizo kubwa linalomkabili Wade hivi sasa ni zile shutuma zinazomuandama za utumiaji fedha za umma kwa ubadhirifu, ufisadi, kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari, ukiukwaji wa haki nyingine za kibinadamu na upendeleo wa kuwapa kazi jamaa zake. Mwanawe wa kiume, Karim amemteua kuwa waziri na binti yake, Sindjely amempa kazi ya kuwa msaidizi muhtasi wa Rais. 
Wade anawakebehi wanaosema kuwa yeye ni mzee na huenda asimalize kipindi chake kwa kuhoji kuwa ikiwa babu zake na baba yake waliishi na kufika umri wa miaka 100 ushei, kwa nini naye asifike umri huo.
Hivi sasa gumzo kubwa nchini Senegal ni juu ya uzee wake. Papo hapo kujitokeza kwa Youssou N’Dour kumeanzisha mjadala mwingine kwamba mtu asiye na elimu ya juu hawezi kuwa rais. Suala hili limeanzisha mtindo mpya barani Afrika. Nakumbuka nchini Tanzania, Augustine Mrema alilazimika haraka haraka ajiandikishe chuo kikuu kimoja cha Marekani apate shahada kwa njia ya mtandao ili aweze kugombea urais.
Cha kushangaza ni kuwa raia wa kawaida anaweza kugombea udiwani, ubunge au  hata kuwa waziri bila ya kujali kama ana shahada au elimu ya juu lakini ikija katika kugombea urais anaangushwa. Raia huyo anageuzwa wa daraja la pili na haki yake kukandamizwa.
Hata hivyo, tukitafakari hebu tujiulize hao wanaojiona kuwa ni wasomi au waliosoma pamoja na mashahada waliyonayo wameweza kweli kutimiza matarajio ya raia wa kawaida? Historia inatuonyesha kuwa wengi wao ndio walioharibu zaidi. Wamekosa muelekeo, uadilifu na nia safi ya kulitumikia taifa.
Siku hizi waliosoma wanaingia katika siasa ili wapate madaraka waweze kupora mali ya taifa. Angalia tu mishahara na marupurupu wanayojipa wabunge; yalinganishe hayo na mishahara duni ya watumishi wa kawaida serikalini.  Ndio maana ukaona kwamba leo madaktari, wanahiyari wawe wabunge na mawaziri wakati kuna uhaba wa  madaktari hospitalini. Wahadhiri nao vivyo hivyo wakati kuna uhaba  wa waalimu.
Linalochoma zaidi ni kuwaona wanasayansi wa vipawa vya juu wakizitupilia mbali taaluma zao wakikimbilia kwenye uwanja mchafu wa tope za kisiasa kwani siasa nchini mwetu zimegeuzwa kuwa hivyo. Ndio maana zinanuka.
Lakini si lazima ziwe hivyo. Na ndio maana wanachomoza wanasiasa wapya mithili ya Youssou N’Dour wanaoingia katika siasa kichwa upande kwa lengo la kuzisafisha siasa chafu. Wanaingia katika siasa wakiamini kwamba uongozi ni uwezo na busara na sio lazima kusoma kwingi.
Bila ya shaka hakuna anayetaka kiongozi mbumbumbu. Anayetakiwa ni kiongozi atayeweza kuongoza nchi kwa hekima na uadilifu. Anayetakiwa ni kiongozi imara atayeweza kuamua na kutekeleza uamuzi wake bila ya kuyumbishwa na majambazi wa kisiasa.
Ikiwa waimbaji wa Bongo Flava kama akina Professor Jay (Joseph Haule) na Sugu (Joseph Mbilinyi-Mbunge wa Mbeya Mjini) au hata Bob Junior na Ali Kiba watataka uongozi na wakaonyesha watakuwa na sera safi za kuongoza nchi kwa maadili ya utawala bora kwa nini wananchi wasiwachague? 
Tayari katika uchaguzi uliopita wapiga kura wa Mbeya (Mjini) walimchagua Sugu wa CHADEMA awe mbunge wao akimshinda mwalimu wake wa zamani wa shule, Benson Mpesya aliyekuwa mgombea ubunge mzito kutoka CCM.
Tupime maendeleo yaliyoletwa na vongozi wetu katika sekta za afya, elimu na kilimo. Tuangalie jitihada zao za kukabili njaa na kuondosha umasikini na tusiangalie tu barabara wanazozijenga. Siku hizi imegeuka  nyimbo watu kusema waziri au rais fulani amefanya mengi. ‘Angalia barabara kutoka mahala fulani hadi fulani.’
Sahibu yangu mmoja kutoka Liberia aliwahi kuniambia: “Afrika tunayapima zaidi maendeleo ya mwanasiasa kwa kuangalia kilomita ya barabara aliyojenga, badala ya sekta nyingine.”  Na mara nyingi barabara hizo huzijenga kwao.
Sitoshangaa ikiwa kutapita mizengwe nchini Senegal ya kumzuia Youssou N’Dour asiwe mgombea wa urais. Tayari wanaojiona kuwa ni wasomi wameshaanza kumbeza kuwa hawezi kuzungumza Kifaransa kwa ufasaha, kana kwamba Kifaransa chake ndicho kitakachofanikisha kupatikana elimu bora, matibabu bora na kupambana na umasikini. Lakini wasomi wetu wamezoea;wanaposhindwa kutoa hoja za maana hata kasumba kama hizi huzitumia.
Chanzo: Raia Mwema

Sunday 8 January 2012

Kafulila atimiza ahadi ya kusomesha wanafunzi 300

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ametimiza ahadi yake ya kusomesha wanafunzi 300 wanaotoka katika familia masikini katika jimbo lake, kwa kuwalipia ada na michango mingine katika sekondari mbalimbali walikopangiwa baada ya kufauli mitihani ya darasa la saba mwaka jana.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ilagala, katika wilaya ya Kigoma, Kafulila, alisema mwaka uliopita aliwalipia ada na michango mingine wanafunzi 100 waliofaulu mitihani ya darasa la saba, na wote wanatoka katika familia duni kiuchumi.
“Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu niliahidi kuwasomesha wanafunzi 300 katika kipindi changu cha Ubunge, na mwaka jana nilianza na wanafunzi 100, mwaka huu licha ya matatizo niliyonayo na chama changu cha NCCR- Mageuzi nitahakikisha nawalipia ada na michangi mingine wanafunzi 300 wanaotoka katika familia masikini kama mimi,” alisema Kafulila.
Alieleza kuwa, yeye hajihusishi na mchakato wa kuwapata wanafunzi hao, kwani mambo yote huanzia kwenye kamati za shule, mikutano mikuu ya mijiji na hatimaye kamati za maendeleo za kata (WDC), hivyo wanafunzi wanaofanikiwa kupenya katika mchakato huo ni wale wenye sifa zinazokubalika.
Kafulila alisema, ameamua kuchukua wanafunzi 300 kutokana na hali halisi kwani wanafunzi hao watamaliza kidato cha nne mwaka 2014 na 2015, ambapo na yeye atakuwa anamaliza kipindi chake cha Ubunge kwa mujibu wa sheria.
Aidha, alisema ili kuhakikisha wanafunzi wa Kigoma wanapata elimu na ujuzi kama wengine nchini, amenunua maabara tano za sayansi mwaka huu, kati ya kumi na nne zinazohitajika jimboni kwake, ambapo fedha za kugharamia zinatoka kwenye Mfuko wa Jimbo.
Aliahidi kukamilisha maabara tisa zilizosalia katika bajeti ya mwaka ujao wa 2013, ili kila sekondari katika jimbo iwe na maabara zitakazowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo na hivyo kuwa hodari katika masomo ya sayansi.
Kuhusu uhaba wa walimu na vitabu katika shule nyingi za msingi na sekondari katika wilaya ya Kigoma, Kafulila, alieleza kuwa kwa sasa taifa linakabiliwa na uhaba wa walimu katika maeneo mbalimbali, ingawa wanaoathirika zaidi na kadhia hiyo ni watoto wa masikini.
Pia, alisema atahakikisha zahanati zote zinapata umeme wa mfumo wa jua ili ziweze kutoa huduma bora ya kutibu kwa wagonjwa na kuhifadhi dawa kwenye majokofu, jambo litakalosaidia huduma kutolewa kwa ufanisi zaidi.
Chanzo: Nipashe



Nyongeza
Hapa nataka niwaulize hawa Wabunge wetu wa Zaznibar, jee wao pesa za majimbo wanapewa kidoga kuliko wenzao, nimekuwa nikifuatilia wabunge wa Tanganyika jinsi wanavofanya mambo makubwa kupitia pesa za mfuko wa jimbo lakini kwa bahati mbaya sana hawa wabunge wetu hawafanyi chochote kwenye majimbo yao hii inaonesha aidha hawapewi pesa au kama wanapewa huwa zinaishia wapi?
Inatokezea mbunge unamwambia changia laki tatu anashindwa na akitowa hiyo shilingi kumi analalamika kama anaitowa kwenye mfuko wake.
Na hii ndiyo sababu wabunge wetu wanafanya biashara kichaa kama ile wanayofanya wale wamachinga pale Darajani yaani wanamuhitaji mteja mara moja tu wanakuibia au wanakupandishia bei ili siku ya pili usende tena na hawa wabunge wetu wengi wao baada ya miaka mitano wananchi wanawaweka pembeni