WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk. Mwinyihaji- Makame amewataka wabunge
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) kutoka Zanzibar, kuhakikisha maslahi
ya Zanzibar yanalindwa ipasavyo katika jumuiya hiyo.
Dk. Makame alisema hayo jana ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar
wakati alipokutana na wabunge hao na kuzungumzia mambo mbalimbali
ikiwemo uongozi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na uratibu wa
Wazanzibari wanaoishi ughaibuni.
Katika maelezo yake, Dk. Mwinyi alisema kuwa umefika wakati kwa
Zanzibar kuendelea kutambulikana na kujua nafasi yake katika jumuiya
hiyo.
Alisema kuwa Zanzibar ina mengi yanayopaswa kujulikana ikiwa ni
pamoja nayo kujua mengi yanayotokea na yanayoendelea katika jumuiya
hiyo.
Dk. Makame alielezea anafarajika kuona wabunge hao wanafanya kazi
kwa ushirikiano mazuri na wenzao kutoka nchi husika katika msimamo mmoja
wa kuletea maendeleo nchi zao.
Dk. Mwinyi alisema wabunge hao kutokana na kutetea maslahi ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna haja kwa jumuiya hiyo kufanya kazi
katika sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo ni
Zanzibar na Tanzania Bara, ili mikakati na mipango ya
maendeleo iende sawia.
Wabunge hao akiwemo Dk. Said Kharib Bilal na Septuu Mohammed,
walimueleza Waziri Makame kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikifanya kazi zake
kwa ushirikiano wa pamoja kupitia wajumbe wake kutoka nchi zote tano
wanachama
No comments:
Post a Comment