Saturday 28 January 2012

Umoja unahitajika Kukabiliana na Tanganyika

Na mwandishi wetu
Naungana na Wazanzibari wenzangu kutoa wito kwa wazanzibari wote kuwa kitu kimoja katika kipindi hichi ambacho Zanzibar iko kwenye msuguwano na serikali ya jamhuri ya muungano (Tanganyika) kuhusu muswada uliopitishwa na baraza la wawakilishi kuhusu nyongeza ya masafa ya bahari.
Kwa kweli suwala hili limetuwekea wazi jinsi gani wenzetu watanganyika walivo na nia mbaya na Zanzibar na jinsi gani wanavotumia mwanya wa kutugawa na kututawala, Tumeona jinsi gani Prof. Tibaijuka alivoigeuza hoja ya wajumbe wa baraza la wawakilishi na kuifanya ionekane kuwa ni hoja ya CUF, hii ni njia moja wanaoyoitumia kupotosha umma wa kizanzibari kwenye mambo ya msingi kama haya.
Nampongeza Mheshimiwa Hamza kwa utambuzi wake wa kulijuwa hilo na kutahadharisha mapema kuhusu njia ovu za kutugawa na kutumia udhaifu wa viongozi wetu wachache ambao hawana uzalendo na visiwa hivi na ambao wameweka maslahi yao mbele kuliko ya umma wa kizanzibari.

Hawa historia itawakumbuka juu ya usaliti wao dhidi ya Wazanzibari, na akina hamza na Jussa pia pia nao historia itawakumbuka na kuwaenzi  kwani historia inaonesha wale wote ambao wanakuwa upande wa umma ndio ambao hufanikiwa katika mbio zao kwenye nyanja mbali mbali ikiwemo za kisiasa.
Mwisho napendekeza Wazanzibari tuwe na utamaduni wa kuonesha hisia zetu kwenye mambo muhimu kama haya ili kwa hatuwa hizo tutakuwa tunawapa nguvu na kujiamini wale viongozi wetu ambao wanatetea maslahi yetu, nimeona hatuwa nyingi zinachukuliwa na sisi ambao tuko kwenye hii mitandao ambayo coverage yake ni ndogo sana mimi ningependekeza wale ambao wako nyumbani tuwe na utamaduni hata wa kuitisha maandamano locally kuwaunga mkono hawa viongozi wetu kwa mfano siku ambayo wanajadili hoja muhimu kama hizi tunapaza sauti zetu hata pale nje ya baraza la wawakilishi.

No comments:

Post a Comment