Tuesday 20 December 2011

Maalim aitaka COSTECH kufanya tafiti Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalimu Seif Shariff Hamad ameielekeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuisaidia Zanzibar kufanya utafiti ili iweze kuzitumia tafiti hizo kuboresha maisha ya wananchi.
Maalim Hamad alitoa maelekezo hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa tume hiyo kufuatia ziara aliyoifanya kwenye ofisi za jengo hilo, ambapo aliielekeza ifanye utafiti katika maeneo manne visiwani humo.
Eneo la kwanza ambalo ninawaomba muliiangazie ni la mazingira.Kama munavyojua Zanzibar ni visiwa na mabadaliko ya tabia nchi yanaviathiri sana visiwa vyetu na kwa hiyo utafiti wenu utatusaidia tujue hatua za kuchukua,” alisema.
Maeneo mengine ambayo aliiomba COSTECH isaidie ni katika upande wa masuala ya ukimwi, ulemavu na mihadarati ambapo alisema tafiti hizo zitasaidia kuelewa matatizo halisi yalivyo na njia za kutumia ili kuyaondoa.
Aidha, aliiasa COSTECH kuzitangaza huduma zake kwa wananchi ili waweze kuzielewa na hatimaye kuzitumia katika maendeleo yao kwa kuwa wananchi walio wengi nchini bado hawajui kuhusiana na huduma zinazotolewa na tume hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Hassan Mshinda, alisema tume imeweza kugharamia mafunzo kwa wataalamu wapatao 295 katika ngazi za shahada za uzamili na uzamivu baada ya serikali kuongeza kiwango cha fedha za utafiti kwa tume hiyo toka Sh. bilioni moja hadi bilioni 16 kwa mwaka huu.
Alisema wataalamu hao wamepelekwa kwenye vyuo vikuu vitano vya umma nchini vya Dar es Salaam, Sokoine, Muhimbili, Ardhi na Nelson Mandela kilichoko Arusha ambapo katika ngazi ya uzamili, tume imewagharamia wataalamu 195 na katika ngazi ya uzamivu inawalipia wataalamu 100
Chanzo: nipashe

1 comment:

  1. Wow, ni jambo zuri unalilizungumza kuwa COSTECH ifanye tafiti Zanzibar, lakini tatizo sio hila tu na wala sio kwa Zanzibar tuu na Africa kwa ujumla hasa hizi nchi za kusini mwa jangwa la sahara hasa Tanzania kuna tatizo la viongozi wa nchi zetu kufanya kazi kwa mazowea kama wanavolalamika kuhusu staffs wa kawaida, kwa nini nasema kwa mazowea ukiangalia mfano mzuri wa nchi za Asia kama Singapore, malaysi na nyenginezo ukiwauliza siri ya mafanikio yao wanasema kuwa serikali zao zilifanya kazi kwa kutegemea tafiti zilizofanywa na Wataalamu wao pamoja na wageni na ukifuatilia research Zanzibar zinafanywa sana tu na hata kwenye hayo maeneo uliyoyagusia kuna research tayari zimefanywa jee, nikuulize maalim tokea muingie madarakani mwaka mmoja uliopita kuna mradi au implementation ya kitu chochote ambacho kimefanywa serikalini based on research zilizopo, na kama hamna jee mulijaribu kuwaita wataalamu tulionao kuona jinsi gani wanaweza kutafiti mradi kabla ya kuutekeleza. sasa ni vizuri mukabase kwenye research kwa sababu research ni pamoja na takwimu za problem na outcomes na recommendation ambazo zinasaidia kutekeleza majukumu yenu based on takwimu ambazo kama mtu atafanya jambo kutegemea experience yake tu bali either ata undersestimate au ata overestimate

    ReplyDelete