Saturday 11 February 2012

Iacheni Zanzibar na bahari yake

BAHARI Kuu si suala la Muungano, na kwa hivyo bahari inayoizunguka Zanzibar na rasilimali zake isiingiliwe na watu wasio husika.
Hivyo ndivyo anavyosema Profesa Abdul Sheriff katika jawabu lake kwa Waziri Profesa Anna Tibaijuka. Kwa upande mwingine Prof. Sheriff anasema kuwa, kwa bahati mbaya kumekuwa na tabia ya kudharau na kupuuza ushiriki wa watu wa Zanzibar katika masuala nyeti na mazito yanayowagusa Wazanzibari. Prof. Sheriff anatolea mfano kitendo cha Mheshimiwa Samuel Sitta kudai kuwa Zanzibar ilishirikishwa
katika kuandaa muswada wa mabadiliko ya katiba kumbe kushirikishwa kwenyewe ni danganya toto.
Akifafanua alisema, katika suala hilo muhimu sana, Zanzibar haikushirikishwa katika vikao, lakini ilitakiwa tu kupeleka maoni yake. Waliotakiwa kufanya hivyo Waziri anayehuiska na Utawala Bora pamoja na Mwanasheria Mkuu. Kwa mujibu wa barua ya Prof. Abdul Sheriff, viongozi hao katika SMZ walitoa mapendekezo 13, lakini yakachukuliwa mawili tu huku menguine 9 yakitupwa katika pipa la taka. “Former Speaker Samuel Sita claimed that Zanzibaris were consulted, naming the Zanzibar Minister of Good Governance and the AG, but it turned out that they were asked to submit their recommendations, but adopted only two out of 13, and threw the rest in the dustbin, and then went on to add many more without consulting even the Zanzibar Government.”
Haya ndiyo anayosema Sheriff akisema kuwa ‘dharau’ hii imerejewa tena katika suala la kuongeza eneo la Bahari la Tanzania ambapo Prof. Tibaijuka anasema kuwa Zanzibar iliwakilishwa wakati si kweli. Akasema, kilichofanyika ni kumchukua Waziri Shamhuna lakini Shamhuna mwenyewe anakiri kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijui jambo hilo.
“It seems that mainland leaders feel that if you have a few Zanzibaris in your gang, then Zanzibaris are represented – and it is never difficult to get a few vibaraka, as we know all too well from our history. The question is whether the people in Zanzibar even knew this business was cooking.” Anasema Prof. Sheriff
akimaanisha kuwa katika dharau zake, Tanzania Bara inadhani kuwapata vibaraka wachache, ambao sitabu kuwapata, basi inaweza kuwaburuza Wazanzibari. Anasema, katika suala hili la Tanzania (Bara) kujiongezea mipaka ya baharini, Zanzibar haina hata habari kwamba kuna jambo hilo. Katika nasaha zake Profesa Sheriff anakumbusha kuwa katika yale mambo 11 ya muungano, bahari haimo. Lakini anaongeza kwa kusema kuwa japo hata katika hii ‘jinai’ ambayo imefanywa ya kuongeza mambo ya muungano na kuwa 22 bila kufuata utaratibu, bado bahari kuu na rasilimali zake haipo katika hayo 22. Katika hali hiyo, Prof. Sheriff anamtaka Waziri Tibaijuka kuwaomba radhi Wazanzibari, kwanza kwa kutaka kuwaburuza katika jambo muhimu kama hili, na pili kwa kujaribu kuwagawa kwa kulifanya jambo hili kwamba ni la Jussa wakati ni la Wazanzibari wote. Lakini kama neno l a ziada, Waziri Tibaijuka
akatakiwa kuzingatia busara ya mkongwe wa siasa nchini Mzee Nassoro Moyo pale alipomwambia Samuel Sita kwamba asidhanie kizazi cha vijana wa sasa ni wale wa kale wa “hewala bwana.”
Chanzo: Annur

No comments:

Post a Comment