Monday 28 January 2013

Athari ya Vyombo vya dola Kujiingiza kwenye Siasa

Katuni na -- malikiblog
Na mwandishi wetu
muonekano wa jeshi la polisi kwa raia umekuwa ukidorora siku hadi siku. Hii ni kutokana na athari za chombo hicho cha dola kutofanya kazi zake kwa uadilifu. Police ni chombo kinachotegemewa kusimamia uslama wa raia wote ambao raia wa tanzania wamegawanyika dini tofauti, makabila tofauti, na vyama tofauti, akiwa mpinzani au chama tawala, akiwa mkristo au muislamu akiwa mmakonde au mchaga wote hao ni watanzania. kutokana na uhalisia wa jamii ilivyo uadilifu kwa makundi yote ni kitu kuhimu sana ila iwapo jeshi letu la police litaegemea upande fulani ndio hayo yanayojitokeza sasa hivi imeonekana raia adui zao nambari moja ni jeshi la polisi, ila haya ni matokeo ya kilichopandwa na jeshi hilo, na inahitajika kazi ya ziada kuweza kurejesha imani ya raia kwa jeshi hilo. Kama ni kuzuia maandamano au mikutano basi ni kwa vyama vyote, dini zote na makabila yote.
Wakatabahu

No comments:

Post a Comment