Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria
ya
Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote
wanaotaka kushiriki
katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana
katika tovuti ya Tume ambayo ni
www.katiba.go.tz
Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora
na upungufu wake na
kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria
kuhusiana na mchakato wa
upatikanaji wa Katiba Mpya.
1. MAMBO YA
KUZINGATIA
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa
na Sheria, Tume
inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
(a) Nani Mwenye
Haki ya Kushiriki:
Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki
ya kushiriki katika
mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania,
lakini amepoteza uraia wa
Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo
atakuwa ametenda kosa chini ya
Sheria.
(b) Utaratibu wa Utoaji
Maoni:
Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama
zifuatazo:
(i) utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti
(www.katiba.go.tz) barua
pepe ya Tume, (katibu@katiba.go.tz), nukushi + 255-22-2133442 begin_of_the_skype_highlighting FREE +
255-22-2133442 end_of_the_skype_highlighting
na
+255-224-2230769 na
(ii) utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua
zitakazotumwa kwa Tume kutumia
anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, S.L.P.
1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775
Zanzibar.2
Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania
wakati wa
ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama
Watanzania
wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni
iliyoandaliwa
na Tume.
(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:
Kila mtu
atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina
yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali
ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au
barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake
(ukurasa unaoonyesha maelezo ya
mtu mwenye pasi hiyo).
Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji
wa maoni ni jambo la uhuru
na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata
Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania
pekee.
“TOA MAONI, TUPATE KATIBA
MPYA”
No comments:
Post a Comment