Hoja za Watetezi wa Muungano
1. Muungano ukivunjika Wapemba walio na maduka dar watarudi
kwao
Huu ni upotoshaji
kwani kuna wachina wanauza hadi karanga, jee kuna muungano wa china na
Tanganyika?
2. Wazanzibari na Watanganyika wameowana
Hii ni hoja ya pili
ambayo pia haina mashiko, Wazanzibari na Watanganyika wameowa wazungu na
wachina jee kuna muungano na nchi hizo, Mzee wetu (Mpigania haki Maarufu za
wazanzibari) Nassoro Moyo aliowa mtanganyika mwaka 1951, jee kulikuwa na
muungano wakati huo.
3. Wazanzibari tukivunja muungano tutakosa kununuwa vitunguu na
mbatata tanganyika,
Tunafanya biashana na nchi mbali mbali Africa na ulaya na Asia jee
kuna muungano na nchi hizo.
4. Wanaodai muungano wa mkataba au uvunjike wanataka kumleta
muarabu
Huu ndio kabisa sio
akili bali matope, nimezaliwa miaka ya sabiini, sijui habari za mfalme wala upumbavu gani
nahitaji Zanzibar yangu yenye mamlaka kamili.
5. Wazanzibari tutagawanyika uunguja na Upemba
Zanzibar ilikuwepo
kabla ya Muungano, jee kuna muungano wa Unguja na Pemba?
6. Tunaihitaji Tanganyika kwa ajili ya ulinzi
hii ni kututia
woga ila kuna nchi ndogo kuliko Znz na zina ulinzi imara, jeshi letu la
Zanzibar lilikuwa strong kabla ya muungano, baada ya muungano ndio tumefika
tulipo.
Next time nitaeleza faida kwa nini tunahitaji Zanzibar mamlaka kamili
No comments:
Post a Comment