Viongozi wawili mashuhuri nchini Cameroon wamekamatwa kwa kuhusika na ununuzi wa ndege mbovu ya rais.
Wawili hao ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Ephraim Inoni na aliyekua Waziri wa mambo ya ndani Marafa Hamidou Yaya.Wakati huo Bw Yaya alikuwa katibu wa afisi ya Rais huku Inoni akiwa naibu wake. Baadaye Inoni aliteuliwa Waziri Mkuu na Yaya akapalekwa Wizara yenye ushawishi ya mambo ya ndani. Wadadisi wamesema Yaya alionekana kuwa mrithi wa kiti cha urais kabla ya kuachishwa kazi mwaka 2011.
Punde baada ya habari kutokea kukamatwa kwa viongozi hao, raia wengi walijitokeza kushuhudia wawili hao wakisafirishwa katika jela kuu la nchi.
Wengine ambao wanashikiliwa kufuatia sakata hiyo ni pamoja na Aliyekuwa Waziri,Jean-Marie Atangana Mebara, Balozi wa Zamani nchini Marekani,Jerome Mendouga na aliyekuwa mkuu wa shirika la ndege nchini Cameroon Yves Michel Fotso.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment