Wednesday 29 February 2012

Maalim Seif: SUK ni imara, Zanzibar ni shwari

Na Joyce Mmasi
NI zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu Wazanzibari wafungue kurasa mpya za maisha ya kisiasa pale walipofanya mabadiliko ya katiba na kuruhusu nchi hiyo kuwa na serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa na vyama viwili vya siasa ambavyo ni CCM na CUF.
 
Kuundwa kwa serikali hiyo kumeleta matumaini kwa wananchi wa nchi hiyo ambapo wengi wa Wazanzibar wamekuwa wakiiunga mkono serikali hiyo kwa kile wanachosema imerejesha maelewano, upendo, amani na kutokubugudhiana kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Macho na masikio ya wapenda amani duniani kote wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya serikali hiyo kwa kuangalia matokeo yake kufuatia kuundwa na hatimaye kuanza kuwatumikia wananchi wake hadi sasa ambapo imetimiza mwaka na zaidi sasa.
 
REDET ni Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia  Tanzania wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Ukiwa miongoni mwa wafuatiliaji wa maendeleo ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, Mpango huo umefanya semina ya siku mbili mjini Zanzibar kwa ajili ya kuangalia hali ya kisiasa katika visiwa hivyo ambapo mada kuu katika mjadala huo uliowahusisha viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, wasomi, wanasheria, watendaji wa serikali na watu wa kada mbalimbali ilikuwa   “Uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar”

Makamu wa Rais wa serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni miongoni mwa wanasiasa aliyechangia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa mpango wa kuundwa kwa serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa, ndiye alifungua semina hiyo.

Mwaka mmoja wa SUK Zanzibar
Akifanya tathmini ya mwaka mmoja wa serikali hiyo, Maalim Seif anaanza kwa kutamka kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni imara na kuwa uimara wake unaongeza mafanikio ya wazanzibar na maslahi ya Watanzania wote.
 
“Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imetokana na matakwa ya wananchi wenyewe wa visiwa hivi, baada ya kuona mfumo uliopita yaani mfumo tenganishi hauna faida kubwa katika kujenga umoja na kukuza maendeleo ya Wazanzibari, ” anasema.
 
Licha ya uimara wa serikali hiyo, Seif anaweka angalizo kwa kusema kama ilivyo katika mataifa mengine, mfumo wowote mpya unapoanzishwa huja na changamoto mbali mbali, hivyo kuhitajika marekebisho ya hapa na pale, ili kuufanya uweze kufanikisha malengo yaliyokusudiwa tangu mwanzo.
 
“Uzuri ni kwamba Zanzibar ina fursa nzuri ya kuweza kujifunza kupitia sehemu nyingine za dunia, ambazo zina serikali zenye mfumo wa aina hii” anasema.

Anaendelea kusema kuwa, jambo la kutia moyo kwa kila aliyeuunga mkono uamuzi wa kuwa na serikali hiyo ni kuwa, katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa serikali shirikishi wazanzibar wanashuhudia faida nyingi.

“Faida moja kubwa ni maelewano makubwa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar. ..... kabla ya kuja kwa utaratibu huu tulikosa maelewano, hali iliyokuwa imesababishwa kwa kiasi kikubwa na kutofautiana kwetu katika itikadi za kisiasa na kukosa mashauri ya pamoja katika kuendesha nchi yetu na kujiletea maendeleo” anasema.
 
Anasema, Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa serikali shirikishi wananchi wenye itikadi tafauti pamoja na viongozi wao, wanakaa pamoja wakishirikiana katika kila uwanja wa maisha na zaidi katika mambo ya kuwaletea maendeleo yao.

“Sina budi kukiri kwamba changamoto za hapa na pale zinatokea na hazitaacha kutokea, lakini kutokana na utaratibu tuliojiwekea kuweka maslahi ya wananchi wetu mbele, changamoto zinapojitokeza tunakaa pamoja kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi kwa haraka” anasema.
 
Maalim Seif anasema, Serikali ya Umoja wa Kitaifa badala ya kupoteza muda mwingi kushughulikia kutatua migogoro, muda karibu wote unatumiwa kufikiria, kubuni na kupanga mipango ya maendeleo itakayowanufaisha wananchi ambapo anasema tayari wawekezaji wa ndani na nje wamevutiwa na hali hiyo na wamo katika mazungumzo na taasisi husika kuwekeza nchini humo.

Anaongeza kuwa, mafanikio ya makubaliano ya muafaka yalianza kuonekana katika uchaguzi wa 2010 ambao anasema ulionesha maendeleo makubwa katika uwanja wa kampeni, kwa vyama vyote kutumia haki yao ya kufanya kampeni bila ya vizingiti.

“Kampeni za 2010 zilikuwa za kiungwana. Pamoja na kuwa na hamasa, lakini kwa kiasi kikubwa hapakuwepo na malumbano, matusi wala kushambuliana. Kila mgombea alijikita katika kutetea sera na ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujenga hoja za kuwashawishi wananchi watoe kura zao kwa mgombea na chama chake....   Haya ni maendeleo mazuri na ni wajibu wetu sote kuyaendeleza na kuyafanya kuwa bora zaidi” anasema.

Hali ya kisiasa Zanzibar baada ya SUK
Maalim Seif pia anaizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar baada ya kuundwa kwa serikali hiyo ambapo anasema ni shwari na kwamba ile tabia ya kupingana kwa sababu za kisiasa inaelekea kwisha kabisa, jambo analosema litawezesha serikali kufanya maamuzi kwa haraka na ambayo yatakubalika kwa wananchi wa mirengo yote mikubwa na viongozi wao.

“Kwa ujumla hali ya kisiasa ya Zanzibar hivi sasa ni shwari, na wananchi wanafanya shughuli zao za kisiasa, kijamii na kimaendeleo bila ya bughudha yoyote. ni maendeleo makubwa tukilinganisha na tulikotoka” anasema.

Anasema kuwa na Serikali ya Umoja  wa Kitaifa katika mfumo wa vyama vingi ni hatua kubwa sana, ambayo inaonyesha upevu wa kisiasa ambao utaiwezesha nchi hiyo kusonga mbele kimaendeleo kwa kasi zaidi.

Ile tabia ya kupingana kwa sababu tu za kisiasa imepungua sana na kuelekea kwisha kabisa, jambo ambalo litawezesha serikali kufanya maamuzi kwa haraka na ambayo yatakubalika kwa wananchi wa mirengo yote mikubwa na viongozi wao.

Anasema kutokana na matokeo hayo, sasa wawekezaji wanavutiwa na hali ya amani na utulivu ya Zanzibar, ambayo hujenga mazingira bora katika shughuli za uwekezaji na shughuli za kiuchumi kwa jumla.

Changamoto wanazokabiliana nazo
Anasema licha ya mafanikio hayo, zipo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo na kusema miongoni ni kuwa wapo baadhi ya viongozi na watu ambao hawafurahishwi na Maridhiano ya Wazanzibari.

“Watu hao ni wachache. Baadhi yao wamekuwa wakijaribu kutia fitna ili kuvuruga maelewano, kwa bahati mbaya yako magazeti machache yanayotolewa Tanzania Bara ambayo yamepania kuleta chochoko ili kuvuruga kuaminiana kulikojengeka......Hata hivyo, kwa vile walio wengi wanaona umoja wetu huu una faida kuliko hasara watu hao hawatafanikiwa” anasema.

Anaeleza changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni katika kukidhi matarajio makubwa ya wananchi juu ya serikali yao, pengine kuliko hali halisi ilivyo ambapo anasema, wananchi wengi wanatarajia serikali yao itaweza kutatua kwa muda mfupi kero kubwa zinazowakabili katika maisha, kama vile mifumko ya bei za bidhaa muhimu na kuwepo hali ngumu ya maisha.
 
Hata hivyo anasema tokea serikali hiyo ilipoanza kazi imekuwa ikichukua hatua kubwa kuhakikisha ugumu wa maisha ya Wazanzibari unapungua, na wananchi kote Unguja na Pemba wanapata nafuu katika maisha.

“Uhaba wa fedha serikalini pamoja na hali isiyotarajiwa inayojitokeza ulimwenguni, kama vile kupanda kwa bei ya mafuta mara kwa mara, kushuka thamani ya shilingi dhidi ya dola, uharamia katika bahari yetu ya Afrika Mashariki, pamoja na majanga ya ukame na mafuriko katika nchi tunazozitegemea zaidi kununua bidhaa za vyakula, vitu hivi baadhi ya wakati huchangia kutofikiwa malengo yetu’ anasema.
 
Anaongeza kuwa serikali inachukua juhudi kubwa kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi ambapo wakati mwingine serikali hulazimika kupunguza kodi za bidhaa zote muhimu, kwa kuzingatia hali za maisha ya wananchi wetu.

Zanzibar gets bumper clove harvest

AS Zanzibar boasts of big clove harvest this year, plans are underway for census of clove trees, the Minister of Trade, Industry, and Marketing, Mr Nassor Ahmed Mazrui, said on Tuesday that his office was now looking for funds for the project.
“We managed to buy 4,687 tonnes of cloves from farmers by last Monday and farmers got more than 70bn/-. Our estimate was to buy 3,000 tonnes,” he said. Mr Mazrui attributed the success to the campaign against smuggling and good price of 15,000/- per kilogramme.
“But we need to have strategies to improve production at 10,000 tonnes in the near future,” he said. The strategies being implemented include counting all cloves trees in the islands, replacing old trees by planting at least 500,000 trees annually for ten years, restructuring the Zanzibar State Trade Corporation (ZSTC), have new law of cloves and branding before establishing a Clove Development Fund (CGF).
“As we prepare new clove law, the government is also considering liberalising the market with great care. The government will not rush to liberalise the clove to avoid risks of collapse,” the minister said.
He said although there was control of cloves smuggling, some greedy people managed to smuggle into Kenya 46 bags full of cloves last week. This year’s clove picking season which started in July, last year is approaching the end by May, this year.
Source: Daily News

Saturday 25 February 2012

KWA NINI TUUJADILI MUUNGANO


Hoja 18 za Baraza la Katiba, juu ya Kwa Nini Tuujadili Muungano ni hizi zifuatazo: Tutakuwa tunawaletea hoja moja moja ili kuongeza ufahamu wa nini tufanye kama wazanzibari katika kuchangia katiba mpya ijayo
 1.  Kuundwa kwake
 Kuundwa kwa Muungano wa Tanzania kuna udhaifu wa kisheria kama ambavyo imeshawahi kuelezwa mara kadhaa na wanasheria na wanasiasa kadhaa wa kadhaa. Ni Muungano ambao ulianzishwa kwa utashi wa viongozi wawili wa kisiasa wakiwa ni Marais wa nchi mbili huru, lakini mambo ya msingi yakiwa hayajazingatiwa.

Ni utaratibu unaokubalika kimataifa na kisheria hata kufuatwa na nchi za Jumuia ya Madola, ambazo kwa kuwa Zanzibar na Tanganyika zote zilikuwa kwa njia moja au nyengine chini ya Himaya ya Uingereza, kwamba viongozi wakuu wa nchi wanaweza kuingia Mikataba ya Kimataifa kwa niaba ya nchi zao.Hivyo viongozi wakuu wawili marais Aman abeid Karume na Julius Nyerere wakaingia mkataba wa kuunganisha nchi zao

Utiaji huo wa saini ulishuhudiwa na viongozi kadhaa wa kila upande wakiwamo kwa upande wa Zanzibar Ali Mwinyigogo, Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na kwa upande wa Tanganyika walikuwepo akina Ali Mwinyi Tambwe, Bhoke Munanka na Osca Kambona. Utiaji saini wa Mkataba wa Muungano haukuhalalisha kukubaliwa na kuridhiwa kwa Muungano na watu wa Zanzibar.

Na ndipo Rais Abeid Amani Karume wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar akaingia mkataba na Rais Julius Nyerere wa Serikali ya Tanganyika, lakini ilikuwa lazima hatua hiyo ifuatiwe na ile ya kuridhia Mkataba huo, na Mabunge ya nchi zao - hili ni sharti kwa mujibu wa mfumo wa kisheria, lakini pia lilifanywa ni sharti ndani ya Mkataba wa Muungano, (Kifungu cha 8) ambacho kilisema wazi kuwa baada ya kusainiwa na viongozi hao Mkataba huo ulilazimika upate ridhaa ya mabunge ya nchi zao.

Upande wa Tanganyika ulitimiza sharti hilo kwa kupitishwa Sheria Namba 22, 1964, ambapo nakala kivuli ya Mkataba wa Muungano iliambatanishwa, na huku sote tunajua kuwa hadi hivi leo nakala halisi ya Mkataba wa Muungano haijaonekana hadharani.

Nakala halisi ya Mkataba wa Muungano imeshindwa kutolewa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, ambaye alisema katika Hati ya Kiapo kwenye kesi Namba 20, 2005 iliyofunguliwa na Rashid Salim Adi na wenzake katika Mahkama kuu ya Zanzibar, kwamba Serikali ya Zanzibar haina hati halisi ya Muungano.

Bila ya shaka hili ni suala sio tu la kushangaza lakini ni la aibu kwa Serikali kukosa kuwa na Mkataba halisi wa kimataifa wa Muungano, na kwa hivyo si suala ambalo linafaa liendelee kufunikwa daima dawamu.

Kama ambavyo tumesema wakati Tanganyika iliridhia Mkataba huo Zanzibar haikufanya hivyo jambo ambalo Rais wa Pili wa Zanzibar Aboud Jumbe katika kitabu chake cha The Partnership amesema ni mgogoro kamili wa kisheria.

Zanzibar ikiwa ndio kwanza inatoka kwenye Mapinduzi na kusimamishwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1963, ilitunga Sheria iliyoitwa Legislative Powers Decree, Namba 1, 1964 ambayo ilitoa mamlaka ya kutunga sheria kwa Baraza la Mapinduzi, na kwa hivyo Baraza hilo la Mapinduzi lingeweza kuwa Bunge la kuridhia Mkataba wa Kimataifa uliokuwa umetiwa saini baina ya Karume na Nyerere na sharti hilo likiwa limetajwa kwenye Mkataba wenyewe.

Lakini watu waliokuwa na dhamana ndani ya Serikali wakati huo pamoja na Jumbe wamesema Baraza la Mapinduzi halikuridhia Mkataba huo. Ikumbukwe wakati huo Baraza la Mapinduzi lilikuwa na mamlaka ya kikatiba ya kutunga sheria.

Wolfgang Dourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwa wakati huo, kauli yake ni hiyo hiyo na zaidi ananukuliwa akisema hivyo katika Mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) 1985,  na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi kwa wakati huo, Salim Rashid amesema katika Hati ya Kiapo kwenye kesi ya Rashid Salim Adi na Wenzake kuwa Mkataba wa Muungano haukuridhiwa na Baraza la Mapinduzi.

Halafu pia msomi anaeheshimika katika uwanja wa Katiba, Professa Issa Shivji amethibitisha kupitia vitabu vyake viwili kile cha 1990 Legal Foundations of the Union of Tanganyika and Zanzibar na kile cha 2008 Pan-Africanism or Pragmatism. Lessons of the Tanganyika-Zanzibar Union kuwa hakuna pahala popote pale ambapo Mkataba wa Muungano inaonyesha umeridhiwa na mdau wa pili yaani Zanzibar.

Ila bila ya shaka hoja inakuja kuwa hakuna ambae amechukua hatua moja mbele ya kusaili uhalali wa Muungano ambao unakosa sifa muhimu na awali kabisa ya kuridhiwa au tuseme kwa usahihi zaidi kukosa kuridhiwa na upande mmoja na kwa hivyo ukaruhusiwa kusonga mbele hadi leo.

Na hio kwa wakati huu ndio sababu muhimu ya kujadili Muungano, maana kama sharti muhimu hilo halikutimizwa ina maana kila kilichofuatia kinakosa uhalali wa kisheria na wakati huu tukijadli kuja kwa Katiba Mpya hilo lazima liwe mbele kwenye ajenda

Thursday 23 February 2012

Siku John Okelo alipotimuliwa Zanzibar

Ahmed Rajab
YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP). Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964 .
Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.
Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.
Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.
Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa — Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani — kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga. 
Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.
Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable & Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe.
Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari.  Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa ‘Waafrika’ wa Zanzibar kutoka kwa ‘wageni’.
Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi.  Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.
Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama ‘nyumba ya karata’.
Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo.  Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: “Nani huyu? Katokea wapi?”
Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.
Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa. 
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na  kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.
Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar. Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo ‘Kamati ya Watu Kumi na Nne’ ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.
Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.
Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.   
Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe ‘kabla ya majeshi yangu kuja.’ Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.
Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua.   Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.
Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.
Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege.  Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.
Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya ‘machine gun’.
Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na  kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana. ‘Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi,’ alieleza Hashil.  
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya. 
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na ‘wanamrejesha’ Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.
Kumbe alikuwa mtu wa kabila la  Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa ‘kiongozi mpendwa wa Mapinduzi’ ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?
Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ‘ukatili na unyama wa Waafrika.’ 
Hakuna ithibati  yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.
Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka.  Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia ‘wakwezi na wakulima’ na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.
Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party. Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa ‘kikomunisti’.  Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.
Source: Raia Mwema

Wednesday 22 February 2012

EEZ issue to be debated by House of Representatives

THE Zanzibar government has said it has no mandate to stop the Union Government from extending the Exclusive Economic Zone in the Indian Ocean.
The government declared this amid pressure from the public as well as some members of the House of Representatives, who have been speaking out against the Union Government’s move to demarcate its exclusive economic Zone. “We stick to our promise that the government.
will give its position about EEZ during the next session of the House of  Representatives scheduled for March 28, this year,” said Mr Mohamed Aboud Mohamed, State Minister in the Second Vice-President’s office.
“We cannot stop the process, and I do not think we have reasons for doing so. Let us wait, we are discussing it and the government’s position will be out during the next session.” He said.
Zanzibar Attorney General (AG) Mr Othman Masoud also said that it might look embarrassing and illegal for Zanzibar to stop the Union government to extend the EEZ from the current 200 to 350 nautical miles. “I think people don’t understand the EEZ issue, because of poor media coverage, and statements by politicians. It is high time the people, including reporters and politicians, read about EEZ and the process of demanding for the extension, so that people can be well informed instead of exaggerating the matter,” said the AG.
Some legislators during recent House session proposed that Zanzibar government write immediately to the Union  government, asking it to halt the EEZ request process, until the internal dispute over the sea area was resolved. The legislators, led by Mr Ismail Jussa Ladu (Mji Mkongwe - CUF), asked the speaker to allow a debate on the motion. The angry legislators reminded the speaker about the 2010 resolution in which oil and natural gas were removed from the list of union matters as well as the EEZ.
Source: Dailynews

Tuesday 21 February 2012

Zanzibar yapokea ripoti ya mgawanyo wa fedha za muungano

ZANZIBAR tayari imepokea ripoti ya Tume ya Pamoja ya Usimamizi wa Fedha kuhusu mgawanyo wa fedha zinazotokana na washirika wa maendeleo kwa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema hayo jana wakati alipozungumza na gazeti hili.
Alisema tume hiyo tayari imewasilisha ripoti yake kwa pande mbili za Muungano kuhusu mgawanyo wa fedha zinazotokana na washiriki wa maendeleo pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imepokea taarifa ya tume ya pamoja ya fedha kwa ajili ya kuifanyia kazi...ngazi muhimu zote tayari imepitiwa na Zanzibar imeridhika nayo,” alisema.
Alisema ripoti hiyo imepitiwa na vyombo vya juu vya SMZ ikiwemo Baraza la Mapinduzi ambalo hujumuisha mawaziri wote wa Serikali.
Hata hivyo, Omar alisema Zanzibar kwa sasa inasubiri kukamilika kwa taarifa hiyo kwa ajili ya utekelezaji wake kutoka kwa upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo bado Baraza la Mawaziri halijakaa kuijadili.
Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Serikali zote mbili na mwenyekiti wake William Shelukindo.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko kuhusu mgawanyo wa fedha zinazotokana na washirika wa maendeleo ikiwemo za misamaha ya madeni pamoja na gawio la Benki Kuu ya Tanzania.
Zanzibar imekuwa ikilalamika gawio inalopata la asilimia 4.5 kwamba ni dogo na limepitwa na wakati na halilingani na matumizi halisi ya SMZ katika shughuli zake.
Chanzo: Habari leo

Mtihani Mwengine Zanzibar

Na Salim Said Salim
MAMIA ya vijana wa Zanzibar waliofanya mtihani wa kidato cha nne wanakabiliwa na mtihani mwingine, tena ni mkubwa zaidi kuliko ule walioufanya mwaka jana na hawajui waukabili vipi huu mtihani mpya.
Matokeo yao ya mtihani wa kidato cha nne yamefutwa na kuambiwa juhudi zao zote za kujitayarisha kwa miezi kadha zimekwenda na maji, yaani  “Ajwar” (pata potea).
Hivi sasa watoto hawa, wengi wao wakiwa wanatokana na familia za kimasikini, wamebaki wakilalama huku wakiwa na huzuni na hivi sasa wanahangaika huku na kule kama kuku anayetaka kutaga na hakuna dalili za kupata mafanikio.
Watoto hawa wa kimasikini wanaona dunia imewapa mgongo na huko wanakokwenda ni kiza kitupu na hakuna mtu  wa kuwaashia taa ya kuona kilipo usoni. Ni unyonge mkubwa.
Ama kweli Waswahili hawakukosea waliposema mnyonge hana haki, lakini tukumbuke walipotutahadharisha kwa kusema; ‘Mnyonge mnyongeni, lakini  haki yake mpeni”.
Kwa kweli inasikitisha sana, inahuzunisha na inatisha kuona viongozi wetu wengi wanaliona suala la kufutwa matokeo ya mtihani kama vile ni jambo la kawaida na hawataki kukubali madhara yake kwa vijana wetu waliofutiwa matokeo ya mitihani.
Sishangai hata kidogo na mtazamo wao huu kwa sababu watoto wa hawa wakubwa ambao tumekuwa tukidhani na wengi kuamini watatuonea imani na kuwahurumia watoto wa kimasikini wanasoma nje ya nchi. Matatizo ya elimu tuliyonayo nchini, hayawahusu.
Ukifanya utafiti wa haraka utaona kuwa watoto wa karibu viongozi wote wa serikali na matajiri hawawapeleki watoto wao katika shule za serikali kwa sababu wanaelewa vizuri kwamba huko hakuna elimu ila kupoteza wakati.
Kwanza  kuna msongamanao ndani ya madarasa, walimu ni wa kuokoteza na wanafunzi wanatumia muda mwingi kupokea wageni au kutakiwa kwenda kwenye sherehe za kitaifa zisizokwisha.
Baaadhi ya viongozi wa serikali na matajiri, bila ya aibu, wamewapeleka watoto wao katika shule zilizodhaminiwa na washirika wa maendeleo wa nchi za nje kusaidia watoto yatima.
Hii leo ukienda shule ya yatima ya OSS ya Zanzibar utashangaa na kushitushwa kuona zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi si yatima bali ni watoto wa viongozi na wafanyabiashara wakubwa wa nchi hii.
Hii ni aibu na  ni dhambi, lakini wenye fedha na vyeo mara nyingi huwa hawajali kwa vile wanaongozwa na jeuri na kibri na si utu na ubinaadamu, imani wema au hisani. Watu hawa hawaoni kuwa wanavyofanya ni vibaya.
Wakati sasa umefika kwa serikali kulitupia macho suala hili kwa kuonyesha imani na huruma kwa watoto wa kimasikini.
Huu mchezo wa kuchezea mitihani na hatimaaye kuathiri zaidi watoto wa kimaskini ni wa hatari na hauna mwisho mwema.
Hivi sasa katika kila pembe ya Unguja na Pemba wazazi na watoto wao wanasikitika na wengine kulia kutokana na kufutwa kwa matokeo ya mithani wa kidato cha nne kwa mamia ya watoto wa kimaskini.
Ukweli ni kwamba Baraza la Mitihani Tanzania limeshindwa kazi yake na wizara zetu za elimu, Bara na visiwani  zimeshindwa kuwajibika katika kuhakikisha mitihani haivuji.
Matokeo yake ni kwamba watoto wa kimasikini na wazee wao walioweka matumaini kwamba elimu ingewasaidia kutokana na umaskini (ukweli ni ufukara) na unyonge wa maisha ndio wanaoumia na kuteseka.
Hapa tujiulize ni nani wa kulaumiwa kwa kuvuja mitihani? Ni hawa wanafunzi au kutokuwepo uadilifu na ulinzi wa kutosha hata mitihani ikavuja?
Kilichojitokeza hapa ni kwamba wanaostahiki kulaumiwa na kubeba dhamana  ni Baraza la Mitihani kwani ni dhahiri kuwa kazi imewashinda na kwa vile imedhihirika wazi kuwa hawawezi kusimamia mitihani kinachotakiwa ni kujiuzulu.
Lakini lililo muhimu zaidi  ni kwa wahusika kuwajibishwa kikazi na kisheria na si kuwaadhibu watoto wa kimaskini.
Hapa nataka nikumbushe kwamba zama za ukoloni nilipokuwa ninafanya mitihani ya darasa la nane na baadaye kidato cha nne hizi habari za kuvuja mitihani na udanganyifu zilikuwa hazisikiki.
Kama wakoloni waliweza kudhibiti mitihani isivuje miaka ile nini kinachopelekea leo kuvuja kwa mitihani iwe jambo la kawaida kama si kutokuwapo uadilifu na kushamiri kwa uhuni?
Tujiulize kulikoni hii leo? Jawabu unayoipata na ambayo ni sahihi kwa mapana na marefu ni kutokuwepo uongozi mzuri katika kusimamia mitihani na uhuni kutawala mwenendo mzima wa kuendesha shughuli za serikali.
Hii ni aibu na fedheha, tena kubwa na wahusika hawastahili kuvumiliwa wala kuonewa huruma. Kama wao hawahurumii watoto wa kimasikini hapana sababu kwa jamii kuwaonea huruma.
Lakini  ukichunguza utaona waliohusika na uvujaji wa mitihani wamepoa na hawana wasiwasi kwa vile wana uhakika wa kulindwa kwa sababu za kisiasa.
Si ajabu hivi sasa  waliohusika na kuvujisha mitihani wakawa wanapanga namna bora ya kuvujisha mitihani ya mwaka huu ili kujipatia fedha za bure kwa kuwa wanaelewa na kujiamini kuwa hawatawajibishwa kikazi wala kisheria. Kwa watu hawa kuvujisha mitihani ni sehemu ya kazi yao.
Hali hii ni ya hatari na inatisha. Serikali inapaswa kuelewa kwamba uhuni wa kuvujisha mitihani na baadaye kufuta matokeo ya shule kadhaa unawaumiza na kuwadhulumu watoto wa kimasikini ambao walitegemea elimu hapo baadaye ingewakomboa na maisha duni wanayokabiliana nayo hivi sasa.
Katika nchi nyingi zinazoheshimu utawala bora na demokrasia (tofauti na ilivyo Tanzania) panapotokea aibu kama hii ya kuvuja mitihani hatua ya kwanza inayofuata ni kwa viongozi wa juu wa Wizara ya Elimu (Bara na Visiwani) na wale wa Baraza la Mitihani kuachia ngazi kwa vile kazi waliopewa imewashinda.
Lakini huu utamaduni mchafu na unaonuka tulionao wa  kulindana kwa maovu tunayoyatenda au kuruhusu wasaidizi wetu kufanya uhuni na wasiwajibishwe utaendelea kutuponza na gharama zake ni kubwa.
Mpaka pale tutapoanza kutoa umuhimu kwa uwajibikaji hizi hadithi za kuvuja mitihani kila mwaka zitaendelea na matokeo yake ni kuendelea kuwaumiza watoto wa kimasikini zitaendea tena kwa kasi zaidi.
Wahusika na uvujaji wa mitihani watasema Tumethubutu na tunaweza na tutaendelea”.
Ni vizuri kama hatuwezi kuwasaidia watoto wa kimaskini tuache kufanya maovu yanayosababisha kuwakandamiza.
Leo mambo haya yananyamaziwa na hapa na pale ndiyo hupigiwa kelele, lakini tukumbuke kama leo suala hili halitazusha balaa historia hapo baadaye itatuhukumu kwa kuwadhulumu watoto wa kimaskini.
Suala la mitihani ni mtihani, lakini maisha ni kupambana na mitihani. Ni vema tukapambana na mtihani huu bila ya woga au kulindana bila ya sababu za msingi.
Chanzo: Tanzania Daima

Sunday 19 February 2012

Abortion in Tanzania- Wazanzibari tukatae hizi njama chafu za kibeberu


ROME, February 13, 2012 (LifeSiteNews.com) – A new “reproductive health” bill being proposed in Tanzania’s National Assembly is “pure western imperialism,” according to a local pro-life leader. Emil Hagamu, Human Life International’s Regional Coordinator for English-Speaking Africa, called the bill “foreign ideology that is being imposed on our African culture whose objective is depopulation.”
“Western countries want to exploit our natural resources and they know they can only do so if they suppress the growing population of young people and next generations,” he told LifeSiteNews.com.
The purpose of the bill, called the “Safe Motherhood” bill, is to change the way Tanzanians think about family life, children and marriage, Hagamu said.
The bill, being sponsored by Care International and brought before a legislative committee this month, will usher in the total abortion and contraceptive “reproductive health” program pushed by such groups as Planned Parenthood International.
In a detailed analysis made available to LSN, Hagamu says the bill will create effective abortion on demand, for any reason or none, and place a legal penalty on health care providers who refuse to participate. Currently abortion is legal in Tanzania in cases where the mother’s “life,” is at risk, and legal precedent exists for abortion in cases where the woman’s “mental” or “physical health” are at risk.
The bill proposes to expand the current abortion law to allow the killing of children who are suspected of “a severe physical or mental abnormality,” who resulted from rape or incest, and in cases where the pregnant woman is “a mentally disordered person,” and “is not capable of appreciating pregnancy.” Health ministers will be required to designate abortion facilities from among existing health centers.
The bill, Hagamu said, “undermines and bypasses African cultural and moral values” about the raising of children; “disregards the religious laws and practice on marriage”; and “will criminalize” pro-life and Christian teachings on contraception. Tanzania is 30 percent Christian, 30-35 percent Muslim and 35 percent followers of “indigenous beliefs.”
“The whole document puts emphasis on reproductive health - with emphasis on contraception to minors and young people,” he said.
Care International sponsored the bill under a cloak of secrecy, Hagamu told LSN. “Care International have done it with secrecy and speed that if not for God’s intervention we might have seen the law passing without any of us knowing what transpired in the process.”
The bill proposes to make contraception, including hormonal drugs, “universally accessible and mandatory to minors without parental knowledge or consent.” It says that all forms of contraception will be made available based on “individual rights to control fertility.” “It shall be the duty of government to provide access to contraception and family planning services including commodities, counseling, information and education.”
The need for the bill was discussed at “safe motherhood stakeholders” meetings over the last year organized by the sponsors, “which underscored the need to formulate a law that would protect pregnant women from maternal mortality and infant mortality,” the Tanzania Daily News reports.
International pressure is coming on strong in support of the bill, with media organs like the New York Times asserting that Tanzania’s current laws are creating “a deadly toll of abortion by amateurs,” and international pressure groups like the European Pro-Choice Network claiming that Tanzania is suffering a “silent pandemic of unsafe abortion.”
At the same time, the UNFPA, UNICEF and UNWomen are claiming that Tanzania is experiencing unusually high population growth that must be curbed. Speaker of the country’s National Parliament, the Hon. Anne Makinda, told a meeting of the UNFPA that population growth is a “critical issue” for Tanzania.
“Our country has one of the highest rates of population growth in the world; on average every Tanzania woman gives birth to five or six children,” Makinda said.
According to the latest government statistics, however, this was an exaggerated estimate at best. Tanzania is at or slightly below the average overall fertility rate of most developing countries in Africa, with 4.16 children born per woman.
The country has a total population of about 42.7 million and a population growth rate of 2.002 percent. This is compared to neighbouring Kenya with a population just over 41 million, an overall fertility rate of 4.19 children born per woman and a population growth rate of 2.462 percent. Another Tanzania neighbour, Zambia, has a population of 14 million, an overall fertility rate of 5.98 children born per woman and a population growth rate of 3.062 percent.
What does stand out in Tanzania’s statistics is the high rate of maternal mortality, with 790 deaths per 100,000 live births in 2008. This is compared to Zambia with 470 maternal deaths per 100,000 live births and Kenya with 530 maternal deaths per 100,000 live births in the same year.
The abortion lobby continues to insist that legalized abortion, always equated with “safe abortion,” is the premier solution to maternal morality and morbidity (birth-related injuries and illness). But organizations that do maternal health care work while rejecting abortion, confirm that lowering maternal mortality rates depends on getting women proper obstetric health care before and after their children are born.
Matercare International, a group that has worked in maternal health care in Africa since 1981, says that maternal deaths and injury and abortions are “readily preventable” but that there is little interest on the international stage.
Most of the maternal deaths in Africa, the group says, occur among “very young mothers, in small villages, and a few at a time.” One of the most common causes of maternal death and illness is obstetric fistula that can be reversed with a simple surgical procedure. Matercare International founder, obstetrician Dr. Robert Walley, says, “Most die in terror from haemorrhage or in agony from obstructed labour.”
All of these conditions are treatable by competent, professionally trained obstetric physicians and nurses, and it is the lack of this training that is the real cause of the problem, not the lack of “safe” legal abortion. Dr. Walley maintains that the staggering rates of maternal death and abortion in Africa can be put down to “neglect” by international health organizations obsessed with abortion.
“Mothers in the developing world do not have access to safe, clean, dignified places to have their babies or access to expert medical services to look after them and while obstetric fistulae can be treated surgically.

Saturday 18 February 2012

Balozi Iddi: GNU imeunganisha wazanzibari

Na Mwanajuma Mmanga

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema mabadiliko yanahitajika katika nyanja mbali mbali zikiwemo za kiutendaji ili kuondokana na utaratibu wa kufanyakazi kwa mazoea ambao hauna tija.
Balozi Seif alieleza hayo jana ukumbi wa hoteli ya Bwawani kwenye ufungaji wa mkutano wa pili wa hali ya siasa visiwani Zanzibar, ulioandaliwa na Mpanago wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Alisema baada ya utulivu wa kisiasa ulioletwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa, jambo la msingi linalohimizwa ni mabadiliko katika utendaji na kuacha na tabia ya kufanyakazi kwa mazoea ‘business as usual’.
Alifahamisha kuwa tabia hiyo haitaleta maendeleo ya haraka kwa wananchi ambao wamekuwa na shauku kubwa ya kupiga hatua za maendeleo mbele baada ya kuwepo kwa utengamano wa kisiasa miongoni mwa Wazanzibari.
Balozi Seif alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, inafanyakazi kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi kuliko maslahi binafsi. “Hakuna jambo linaloamuliwa na mtu mmoja peke yake bali serikali nzima chini ya uongozi wa Baraza la Mapinduzi. Tukisema huu ni uamuzi wa serikali uamuzi huo umefikiwa katika misingi hiyo”,alisema Balozi Seif.
Alifahamisha kuwa hakuna kitu kilichoundwa na mwanadamu ambacho hakiwezi kuboreshwa, hivyo changamoto zinazotolewa na wadau zinazoikabili serikali zitafanyiwa kazi. “Serikali itakuwa makini kuangalia mapendekezo hayo ili yaweze kuboresha si serikali tu bali hata taasisi nyengine zinazohusiana na utendaji wa kazi wa serikali yenyewe”, alisema Balozi Seif.
Aidha aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa kuunda kwa serikali ya Umoja wa kitaifa imeamuliwa na wananchi wenyewe kwa kura ya maoni ambapo hivi sasa imekupo faida kubwa ya ushirikiano na kuaminiana miongoni mwa wananchi ikilinganishwa na hapo awali.
Alisisitiza kuwa pamoja na mabadiliko katika serikali kuhitajika, lakini hayapaswi kuwa ya haraka mno kwani huku akitolea mfano nchi ya Urusi ambayo ilitaka kufanya mabadiliko ya haraka.
Katika mkutano huo wa siku mbili wataalamu mbali wa sheria walipata nafasi ya kuwasilisha mada ambapo walionesha changamoto inayoikabili serikali ya Umoja wa Kitaifa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Katika mada yake Kaimu Katibu Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad alisema serikali ya Umoja iliyopo Zanzibar inatofautiana na ile ya Kenya na Zimbabwe ambazo ziliundwa baada ya machafuko yaliyotokana na uchaguzi.
Alisema serikali hizo ni za muda wakati ile ya Zanzibar ni ya kudumu iliyobainishwa katika katiba baada ya wananchi kuridhia katika kura ya maoni.

Zanzibar MPs protest Tanzania bid for more sea

Tanzania’s plan to seek an extension of continental shelf outside the Exclusive Economic Zone (EEZ) is facing renewed resistance, as the Zanzibar Parliament prepares to petition the UN to block the move.
A section of MPs in Zanzibar House of Representatives are claiming that the Isles was not involved in the decision to extend the EEZ and sharing of marine resources.
The MPs plan to send a delegation to the UN to ask for the withdrawal of the application by the Mainland government.
The extension would give Tanzania the right to explore and exploit non-living and mineral resources on the seabed and sub-soil of the extended continental shelf adjacent to the EEZ in accordance with the United Nations Convention on the Law of the Sea.
It is expected that the area will increase the potential for oil and gas exploration as well as fishing activities.


Anna Tibaijuka, the Minister for Lands, Housing and Settlements Development, said the decision to apply for the extension of Extended Continental Shelf (ECS), which lies 150 miles beyond the current 200 miles, was reached by the Cabinet and the process involved both parts of the Union.
“The extension of ECS will benefit both parts of the Union and it is not wise to be at odds before the UN has even deliberated on and approved the application,” said Prof Tibaijuka.
The consideration of the submission made by the United Republic of Tanzania will be included in the provisional agenda of the 13th session of the Commission scheduled to be held in New York from July 30 to 10 August 2012.
“The Union government is wrong to go to the UN without consulting the Zanzibar government. The move is also against our April 2009 resolution demanding that oil and natural gas as well as EEZ be removed from Union matters,” said Ismail Jussa of the Civil United Front (CUF).
“Years back, the Zanzibar House of Representatives had decided that marine and oil issues should be the preserve of Zanzibar, therefore Tanzania mainland had no reason to undertake such sensitive matters on behalf of Zanzibar,” he added.
Early last month, the United Republic of Tanzania submitted an application to the Commission on the Limits of the Continental Shelf (CLCS) of the UN, in accordance with Article 76 paragraph 8 of UN Convention on the Law of the Sea.
Kenya has also applied to acquire an additional 103,000 square kilometres and has already secured a maritime agreement with Tanzania, its neighbour to the south. The UN requires that countries that share the ocean must reach an agreement on the border issue.

Kiama cha kughushi vyeti chaja

18th February 2012
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imetangaza kwamba itaanza kuhakiki vyeti vyote vinavyotolewa na vyuo vikuu nchini na vya nje, pamoja na kuvisajili ili kutambua vyuo vinavyotoa elimu ya juu kiholela.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome, alisema imeamua kujaribu kujikita katika mfumo utakaoiwezesha kufanya mabadiliko mbalimbali ili kuboresha utoaji huduma zake.
Profe. Sifuni alisema kuwa katika utaratibu utakaoanza hivi karibuni, suala zima la ithibati litaangaliwa kwa umakini, kwani TCU inataka kuhakikisha programu zote zinatolewa kwenye vyuo vikuu vinavyotambulika na kwamba taarifa kuhusu utoaji elimu ya juu kiholela itatolewa hivi karibuni.
Aidha, alisema kuwa programu zote zitakazotolewa na vyuo vya juu ni lazima zithibitishwe na Tume hiyo na kama zinatolewa nje ya nchi zitambuliwe ikiwa ni pamoja na shahada na stashahada.
Alisema katika kutambua shahada ya kwanza, ya pili na ya uzamivu, Tume hiyo imewasiliana na wataalamu ili wasaidie kuweka kumbukumbu na mawasiliano kati ya TCU na wahitimu wa vyuo, ambapo baada ya mhitimu kujaza fomu ya kwenye mtandao ili kuomba cheti chake kitambulike, atatakiwa kupeleka cheti chake halisi ili kikaguliwe.
Aliongeza kuwa baada ya kukaguliwa, TCU itatoa cheti kitakachoonyesha kuwa cheti cha mhusika kimekaguliwa, na cheti hicho kinaweza kutumiwa na mhitimu sehemu yoyote na endapo watakitilia mashaka cheti chake ataweza kuwaonyesha cheti cha uthibitisho kutoka TCU.
Alifafanua kwamba lengo la utaratibu huo ni kuwasaidia wale wenye vyeti vya nje kuvisajili kwa muda mfupi, ambapo itachukua wiki mbili cheti kusajiliwa.
VYA WALIO KAZINI PIA KUKAGULIWA
Akijibu swali kuhusu wale ambao tayari wapo kazini na wana vyeti kutoka vyuo vya nje ambavyo havijatambuliwa na TCU, Profesa Mchome alisema wamekwisha kupokea maelekezo kutoka kwenye Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuwa pia vyeti vyao vinatakiwa kusajiliwa.
“Kwa wale wafanyakazi walio na vyeti vya nje, na ambao wapo kazini, lakini bado TCU haivitambui vyeti vyao, tutatangaza na kutoa muda ili wote wavilete tupate kuvitambua” alisema.
UDAHILI 2012/13
Profesa Mchome pia alitangaza kuanza kwa muda wa udahili wa wanafunzi kwa msimu wa masomo wa 2012/2013, ambapo watahiniwa wamegawanywa katika makundi matatu, ambayo ni waombaji wa moja kwa moja, waombaji wasio wa moja kwa moja, na waombaji wenye sifa zinazolingana.
Alisema kwa waombaji wa moja kwa moja, wanatakiwa kuanza kuomba udahili kuanzia Aprili 23 mwaka huu kutegemea na matokeo ya kidato cha sita kwa wale wote waliomaliza kidato cha sita mwaka 2010, 2011 na 2012, pamoja na wale walio na stashahada za ualimu mwaka 2010, 2011 na 2012.
Kundi la pili ni waombaji wasio wa moja kwa moja wanaotakiwa kuomba kuanzia Aprili 1, mpaka Aprili 30, 2012 waliomaliza kidato cha sita, wenye stashahada za ufundi na wenye stashahada za ualimu waliomaliza sio chini ya miaka miwili iliyopita.
Kundi la tatu ni wenye sifa zinazofanana na hizo, ambao wanaweza kuomba moja kwa moja.
Hao ni wenye stashahada zinazotambuliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE), ambao hawapo kwenye kundi la kwanza wala la pili la waombaji.
Wengie ni wenye stashahada kutoka nje ya Tanzania ambazo zinatambuliwa na NACTE na wengine wenye shahada ambao wanataka kujiunga na programu nyingine za shahada kama uchumi na biashara
Wengine ni wahitimu wa kidato cha sita na wana vyeti vyenye sifa ya kuwaruhusu kujiunga na vyuo vikuu.
Profesa Mchome alisema TCU imeamua kuweka viwango vilivyo sawa katika ufundishaji hasa katika masomo ya biashara na mfumo wa kutambua tuzo za vyuo vikuu ili kuleta ulinganifu kwa vyuo.
Aidha, alisema TCU ina mpango wa kuviunganisha vyuo vyote vilivyopo chini ya NACTE na TCU ili viwe na mfumo mmoja utakaovitambulisha.
CHANZO: NIPASHE

Friday 17 February 2012

Tangazo muhimu la mijadala ya mustakbali wa nchi yetu - Zanzibar

Inshaallah Kesho Jumamosi asubuhi saa 2.30 katika ukumbi wa Beit Al Yamin Malindi kutakuwa na mjadala wa wazi wa wadau wote wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne. Mjadala huo utawashirikisha walimu wa skuli za serikali na binafsi, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wa elimu karibuni katika mjadala huo ili kutoa maoni yenu katika mjadala huo. Aidha Kesho hiyo hiyo jioni inshallah saa 4:30 eneo la Mapembeani Mwembe Tanga kutakuwa pia na mkutano wa kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba, mkutano ambao umeandaliwa na baraza la katiba zanzibar mnaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo, vitabu vya KATIBA TUITAKAYO vitatolewa bure katika mkutano huo. watakaoongoza utoaji wa elimu ni pamoja na Professa Abdul Shareef, Awadh Said na Ally Saleh. Mnakaribishwa kuhudhuria kwa wingi na mnaombwa kwa kila atakayesikia tangazo hili amuarifu na mwenzake

Thursday 16 February 2012

Ukosefu wa utawala bora ndio unaopalilia ufisadi

WIKI iliyopita waziri mkuu wa zamani wa Angola Marcolino Moco, akiwa ziarani Ureno, alimshambulia vikali Rais José Eduardo dos Santos kwa namna anavyoyatumia madaraka yake kuwatajirisha jamaa zake. Moco anamuelewa vilivyo dos Santos na anaujua nje ndani utawala wake.

Mbali ya kuwa waziri mkuu (1992 hadi 1996) aliwahi kwa muda wa mwaka, kuwa katibu mkuu wa MPLA, chama kinachotawala nchini humo. Nyadhifa hizo alizishika chini ya Dos Santos. Hali kadhalika, Moco ni katibu mtendaji wa kwanza wa Jumuiya ya Nchi Zizungumzazo Kireno (CPLP).

Moco, ambaye bado ni mwanachama wa MPLA, alisema kwamba ayafanyayo Dos Santos yanastahili kulaaniwa kwa sababu ni mambo ya fedheha na ni ya kashfa.

Dos Santos si kiongozi pekee barani Afrika mwenye kushtumiwa kwa kuyatumia vibaya madaraka yake kwa minajili ya kupora mali ya taifa au kwa kuvitumia vyombo vya dola kwa kujitajirisha yeye na wanawe na jamaa zake na wengine walio karibu naye.

Nchini Tanzania tumeshuhudia jinsi Ikulu ya Dar es Salaam ilivyogeuzwa na kuwa pahala pa kufanyia biashara wakati wa utawala wa Rais (Mstaafu) Benjamin Mkapa. Tunashuhudia pia jinsi ufisadi unavyozidi kushamiri nchini hadi leo.

Maovu hayo ya Angola na ya Tanzania yameweza kutendwa kwa sababu ya ukosefu wa ‘utawala bora’ na kutopevuka kwa demokrasia.

Inapofuatwa kikwelikweli, demokrasia huwa ni mfumo wa serikali ya watu, iliyoundwa na watu na kwa ajili ya watu. Tunapoutaja mfumo wa ‘serikali ya watu’ tunaikusudia serikali yenye kuwashirikisha wananchi kupitia wabunge waliowachagua.

Tunaposema kuwa serikali ya kidemokrasia ni ile iliyoundwa na watu tunakusudia serikali inayoendeshwa na waliochaguliwa na wale walio wengi. Huchaguliwa katika uchaguzi mkuu.

Na tunaposema kuwa serikali ya kidemokrasia ni ile iliyopo kwa ajili ya watu huwa tunaikusudia serikali yenye kuwatumikia wananchi.

Hadi sasa tumeizungumzia demokrasia kwa mkato.

Serikali ya kidemokrasia huhimiza na huruhusu haki za uraia kama vile uhuru wa kusema, uhuru wa kuabudu au kutoabudu, uhuru wa kutoa maoni na wa kushiriki katika harakati mbalimbali nchini.

Serikali aina hiyo, kadhalika, husisitiza na hulinda utawala wa sheria pamoja na kuheshimu haki za walio wachache katika jamii.

Kwa jumla, jamii inayoelezewa kuwa ni ya kidemokrasia ni ile jamii ambamo watu wake huonekana kuwa ni sawa mbele ya serikali na mbele ya sheria.

Yapo mengine pia katika mfumo wa kidemokrasia, kwani demokrasia si dhana au mfumo wa kisiasa tu, bali pia ni mfumo wenye kanuni ya kiuchumi na ya kijamii. Serikali inayofuata mfumo huo huwashughulikia wote katika jamii, hasa walio masikini na wengine wasio na hali nzuri za kimaisha.

Serikali hiyo huhakikisha kwamba inatoa huduma nzuri za kijamii ikiwa ni pamoja na huduma ya afya na elimu ya bure, kuwapatia wasiojiweza nyumba za kuishi kwa bei nafuu kama si bure. Huwa ni haki ya kila mwananchi kupata huduma zote hizo; wananchi wote huwa ni sawa na hawabaguliwi si kwa itikadi zao za kisiasa, za kidini, za kikabila, za kijinsia au kwa visingizio vyovyote vile.

Nchi ya kidemokrasia huwaona raia wake wote kuwa watu walio sawa mbele ya sheria. Na hii ina maana kwamba katika utumishi wa serikali watu huwa wanaajiriwa serikalini kwa mujibu wa vigezo maalumu, vikiwa pamoja na sifa za masomo na uzoefu wa kazi. Watu huwa hawaajiriwi serikalini au kupandishwa vyeo kwa sababu ya utiifu wao wa kisiasa au kwa sababu wamekifadhili chama kinachotawala.

Katika mfumo kama huo, ajira serikalini au katika taasisi nyingine za umma huwa hazirithiwi wala huwa hakuna kupendeleana kwa sababu watu wana udugu au ujamaa au usuhuba au kwa sababu muajiriwa ni mtoto wa fulani.

Kwa ufupi, huo ndio msingi wa mfumo wa kidemokrasia.

Jingine lililo muhimu ni kwamba katika mfumo aina hiyo kunakuwa na utenganisho wa madaraka au mamlaka kati ya Baraza la Kutunga Sheria (Bunge), Mahakama na Serikali (Rais). Hakuna mtu mmoja pekee anayekuwa na madaraka au mamlaka ya utendaji.

Badala yake kunakuwa na Katiba ya Kidemokrasia inayohakikisha kwamba vyombo vya dola vina taratibu za kudhibitiana ili kuepusha matumizi mabaya ya madaraka.

Hivyo, Bunge linakuwa na mamlaka ya juu dhidi ya tawi la Utendaji la serikali (yaani Rais) na Mahakama yanakuwa na uhuru kamili na huwa hayawezi kuingiliwa ama na Bunge au na Rais.

Sehemu muhimu ya mfumo aina hii ni kuheshimu haki za kimsingi za binadamu, kama zilivyotajwa na Umoja wa Mataifa katika Tangazo lake la Haki za Binadamu. Tangazo hilo linaharamisha kila aina ya ubaguzi na linasema kwamba wanadamu wote ni sawa na wana hadhi sawa ya utu.

Ili kuustawisha mfumo wa demokrasia ni muhimu kwamba wananchi wawe na uhuru wa kusema, uhuru wa kutoa maoni yao na uhuru wa kukusanyika na kuunda vyama wavitakavyo.

Watu wasioridhika na hali ya mambo ilivyo pia wawe na uhuru wa kueleza manung’uniko yao. Vyombo vya habari navyo lazima viwe huru pamoja na njia nyingine za mawasiliano na visiwe vinazuiwa au vinajizuia vyenyewe kueneza habari zisizopendwa na wakubwa.

Ikiwa hizi ndizo kanuni za kimsingi za demokrasia, basi tunaweza kuzipima nchi na kuangalia iwapo katiba zao zinazikumbatia kanuni hizi au la. Hili ni suala linalostahiki kutiwa maanani nchini kwa vile kuna mchakato utaopelekea kuandikwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Tunaweza kujiuliza maswali kadhaa. Kwa mfano, kwa kiwango gani hii katiba ya sasa ya Tanzania inakidhi kanuni za kuifanya iwe ‘nchi ya kidemokrasi’, na hasa katika mfumo wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa vile huu ni Muungano wa nchi mbili zilizo huru inavyotakiwa ni kwamba serikali yake iendeshwe kwa msingi wa usawa baina ya sehemu hizo mbili.

Swali jingine ni iwapo katiba ya sasa inaupa upande mmoja wa Muungano madaraka makubwa sana kushinda upande mwingine, labda kwa sababu ya ukubwa wake au wingi wa watu wake.

Tunaweza pia kujiuliza iwapo ni sawa katika jamii ya kidemokrasia kuwa na Rais Mtendaji aliye na madaraka yasiyo na kikomo? Katiba ya sasa ya Tanzania ina vifungu vyenye kumpa Rais nguvu kubwa mno bila ya kuwa na taratibu za vyombo vingine vya dola za kumdhibiti asiyatumie vibaya madaraka yake.

Ili kuweza kuipima nchi na kuingalia kama ni ya demokrasia changa au ya udikteta unaoendelea itatubidi tuyaangalie madaraka ya Rais, ya Bunge na uhuru wa Mahakama pamoja na ubora wa sheria za nchi na nguvu zisizoshindika za taasisi za serikali, urasimu ambao unapalilia hongo na ulaji rushwa.

Kuna kigezo kingine ambacho tunapaswa kukizingatia. Nacho ni jinsi Jumla ya Pato la Taifa (GNP) linavyogawiwa kwa wananchi.

Ni muhimu pia kuangazia jinsi fedha chafu, yaani zile zinazopatikana kwa njia mbalimbali za kifisadi, zinavyokuwa na dhima katika uchumi wa taifa na jinsi ‘zinavyofuliwa’ na kusafishwa kwa kuingizwa katika uchumi.

Kwa hiyo, tukiyaangalia yote hayo tutaona kwamba demokrasia ni mfumo wa kikatiba na wa kiserikali wenye kuhimiza pawepo maridhiano katika siasa pamoja na utaratibu wa kuihalalisha serikali.

Tunapoutaja ‘utawala bora’ tunakuwa tunauzungumzia uhalali wa serikali kutawala na mahusiano yaliyopo baina ya serikali na wanaotawaliwa. Utawala bora ni sehemu muhimu ya utawala wenye kujigamba kwamba ni wa kidemokrasia. Na ni lazima huo utawala bora uwe unakwenda sambamba na utawala wa sheria na uwaridhishe wananchi kwamba serikali ipo ili iwatumikie wananchi na si wananchi wapo kuitumikia serikali.

Katika jamii yenye utawala bora, serikali hupata uhalali wake kutoka kwa wapigaji kura. Kwa hakika, uchaguzi ni kijenzi muhimu cha ‘utawala bora’. Uchaguzi huwa unafanywa baada ya vipindi maalumu, unakuwa wa ushindani, unakuwa wazi, na unakuwa ‘huru na wa haki’ na washindani au wagombea wote wanapata fursa sawa. Chaguzi zinazofanywa namna hiyo aghalabu huwa na matokeo ambayo wagombea wote huyakubali wakitambua kwamba hakujapita mizungu yoyote wakati wa uchaguzi.

Nchi nyingi za Kiafrika zisemazo kwamba zina misingi ya demokrasia na utawala bora zimeunda wizara au idara za serikali zenye kushughulikia masuala haya pamoja na shughuli za kikatiba.

Wizara kama hiyo ipo Zanzibar. Huo ni mwanzo mwema; lakini si kuanzishwa kwa wizara aina hiyo kutakoifanya nchi iwe na utawala bora au muovu. Nchi itakuwa ni yenye utawala bora pale wananchi wake watapokuwa na uhuru wa kimsingi, maisha mazuri na watapokuwa wanalindwa na sheria bila ya ubaguzi au mapendeleo.

Rais Aboud Jumbe: Ilikuwaje chama kikampindua?

WAKATI alipokubali kuunganisha chama chake cha Afro-Shirazi (ASP) na chama cha Tanganyika African Union, Oktoba 1976, Rais wa Zanzibar, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, hakujua kwamba kwa kufanya hivyo, alikuwa anajitia kitanzi cha kupoteza urais wa Zanzibar miaka minane baadaye.

Tangu mwanzo, chale zilimcheza Jumbe, pale Mwalimu Julius Nyerere, Septemba 5, 1975, alipopendekeza kwenye kikao cha pamoja cha Halmashauri Kuu [NEC] za TANU na ASP, kwamba vyama hivyo viungane. Lakini Jumbe, kwa kusita, na kwa hofu na shaka iliyofichika, alitaka chama chake kipewe muda zaidi kuweza kufikiria pendekezo hilo.

Hatimaye, makubaliano ya Oktoba 1976 yalizaa chama kipya kilichoitwa Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichozinduliwa Februari 5, 1977. Ni CCM kilichompiga buti Jumbe, Januari 1984, kwa tuhuma za kuthubutu kuhoji muundo wa Muungano, akapoteza nafasi zote za uongozi – urais wa Zanzibar, umakamu mwenyekiti wa CCM Taifa, na umakamu wa rais wa Muungano. Ilikuwaje?

Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi aliongoza Zanzibar kuanzia Aprili 1972 baada ya kifo kwa kupigwa risasi cha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Alirithi nafasi hiyo kwa msaada mkubwa wa Mwalimu Nyerere dhidi ya matakwa ya baadhi ya Wazanzibari ambao walitaka mtu mwenye kuenzi na kuendeleza fikra na utawala wa kibabe wa Karume, arithi nafasi hiyo. Walimtaka Kanali Seif Bakari.

Mwalimu hakukubaliana na maoni ya Wazanzibari ya kumteua Kanali Seif Bakari, mwanajeshi, kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya pili, Zanzibar. Alijenga hoja kwamba, kwa kuwa Karume aliuawa na mwanajeshi, Luteni Hamud Hamud, kumteua mwanajeshi mwingine (Bakari) kuwa Rais, kungeleta picha na hisia kwamba, kuuawa kwa Karume yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi.

Nyerere akampendekeza aliyekuwa Waziri katika Ofisi ya Rais (mambo ya Muungano), Aboud Jumbe, kuchukua nafasi hiyo. Hoja yake ikapita.

Jumbe na Nyerere walifanana kwa mengi: wote walikuwa wasomi waliosoma pamoja Chuo Kikuu Makerere; kisha wote wakawa waalimu. Jumbe alilegeza mengi yenye ukakasi yaliyokithiri wakati wa utawala wa Karume. Hata ile misuguano iliyotia fora kabla ya hapo, kati ya Karume na Nyerere juu ya Muungano na kutishia kuvunjika kwa Serikali ya Muungano, ilitoweka.

Hatimaye Jumbe alianza kukubalika Visiwani na Bara; akawa kipenzi cha Rais wa Muungano, Mwalimu Nyerere. Mara nyingi alialikwa Bara na baadaye akapaona kama nyumbani kwake.

Lakini kadri alivyozidisha ziara za kirais Bara na nje ya nchi kumwakilisha Nyerere, ndivyo alivyozidi kujitenga na siasa pamoja na mambo mengi ya Visiwani. Hatimaye alipaona Dar es Salaam kuwa kwake zaidi kuliko Zanzibar. Aliweza kuruka kwa ndege kwenda Zanzibar mchana kwa ziara fupi, na kurejea Dar jioni.

Kutokuwepo kwake Zanzibar kwa muda mrefu kulizua pengo na ombwe la kiuongozi kwa kuwa hakuna miongoni mwa wasaidizi wake aliyethubutu kumfuata Dar Es Salaam kwa mashauriano. Kwa sababu hii kila kitu kilisubiri arudi Zanzibar kwa “ziara” fupi, hata kama ni idhini ya kukata mti.

Nyerere alifurahishwa na utendaji wa Jumbe na kuingiwa hamu ya kutaka Muungano zaidi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuviunganisha TANU na ASP, kama tulivyoona mwanzo.

Ili kumfurahisha Mwalimu Nyerere juu ya Muungano, mara nyingi hotuba zake zilianza hivi: “Tunataka umoja; ni kwa njia hii pekee kwamba tunaweza kubadili mambo mengi, ili kwamba palipo na kukata tamaa pawe na matumaini, penye chuki pawe na upendo na amani……”.

Muungano ulivyozidi kuimarika, ulifika wakati Jumbe akajiona kama mrithi halali mtarajiwa wa Rais Nyerere, na hivyo kujimwaga zaidi roho na mwili kwa mambo ya Muungano, badala ya kushughulikia utawala wa Visiwani. Ni matarajio hayo ya kurithi nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, yaliyomfanya akubali kirahisi kuungana kwa ASP na TANU. Ingekuwa enzi za Karume, na kwa jinsi tofauti kati yake na Nyerere zilivyokuwa dhahiri na kubwa, huenda TANU na ASP visingeungana.

Kuanzia Februari 1972 hadi Aprili 1983, Chama kipya – CCM kilifurahia ndoa mpya kwa utulivu; lakini pale Nyerere alipopendekeza marekebisho zaidi ya “kuimarisha Muungano”, mlipuko mpya wa malalamiko ulitokea Zanzibar, moja ya hayo ni hofu ya nchi hiyo kumezwa na “Tanganyika”.

Hofu ya Wazanzibari iliongezeka pale Watanzania Bara walivyozidi kupendekeza kuwa na Serikali moja ya Muungano, badala ya muundo wa Serikali mbili ndani ya Muungano. Hofu hizi za Wazanzibari zilianza kumweka pabaya Jumbe juu ya uswahiba wake na Nyerere; alianza kuitwa “msaliti” wa Wazanzibari na Zanzibar, naye akaanza kugeuka nyuma, lakini kwa kukanganyikiwa; alikuwa njia panda.

Ili kurejesha imani ya Wazanzibari kwake, lakini kwa chukizo kwa Nyerere, Jumbe aliomba mawazo ya kiserikali kutoka kwa makatibu wakuu wote wa wizara na watendaji wakuu wengine wa Serikali ya Zanzibar.

Wote walikataa muundo wa Muungano wenye Serikali moja, wakapendekeza kuwe na Serikali tatu – Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano tu. Lakini kubwa lililomchanganya akili Jumbe lilikuwa njiani, likimnyemelea.

Mwaka 1983, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Muungano, Edward Moringe Sokoine, aliteuliwa kuwa waziri mkuu. Sokoine alikuwa kiongozi makini, shupavu, mnyoofu na mwenye mvuto mkubwa kwa watu. Na katika kipindi kifupi tu, alijidhihirisha kuwa “chaguo la watu” na mrithi halali wa Nyerere ambaye naye alimkubali kwa ishara na kwa vitendo. Akawa anaonyesha upendeleo dhahiri kwa Sokoine. Kuna sababu nyingi kwa hilo; lakini itoshe kutaja tatu tu kati ya hizo.

Moja ni kwamba, Nyerere alianza kumwona Jumbe kama kiongozi mpweke, asiyeungwa mkono na watu wa chini (umma) Visiwani. Alimwona pia kama dikteta mkimya, asiyeweza kushauriwa akashaurika na watu wa chini yake.

Nyerere aligundua pia kile pekee kilichomsukuma “ang’are” kwake na kwa Wabara: kiu ya kurithi nafasi ya Rais baada ya Nyerere.

Baya zaidi lililomuudhi Mwalimu ni kwa Jumbe kugeuka mhafidhina wa kidini na mpambanaji wa Kiislamu katika Taifa lisilo na dini. Jumbe alizuru nchi nzima akitoa mihadhara kwenye misikiti hata Serikali ikalazimika kutoa waraka mkali wa Rais (presidential circular), kuwakumbusha viongozi wa kitaifa kutojitambulisha na mambo ya kidini. Hata hivyo, Jumbe alipuuza waraka huo, akaendelea kivyake.

Habari zikamfikia Jumbe juu ya kuanza kupoteza upendeleo wa Nyerere na kuchuja; zikauma, zikamvunja moyo; uhasama kati ya Jumbe na Nyerere ukazuka. Katika hali hiyo Muungano ukaanza kutikiswa.

Hatua ya kwanza iliyoanza kutikisa Muungano ilikuwa ni kumrejesha Tanzania Bara, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Damian Lubuva; badala yake akamteua raia wa Ghana, Alhaj Bashir K. Swanzy na kumpa uraia.

Kuanzia hapo, madai ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya Katiba, kupitia mihadhara, magazeti na redio, yalipamba moto. Wengi watakumbuka matangazo ya redio ya mafichoni, maarufu kama “Kiroboto tapes”, ya kudai Wazanzibari warejeshewe visiwa vyao, yalivyopamba moto hadi ilipogunduliwa msituni na wanajeshi kutoka Bara na kuzimwa.

Kwa kupitia Jaji Bashir Swanzy, iliandaliwa hati ya mashtaka kuhoji muundo na uhalali wa Muungano kwenye Mahakama Maalumu ya Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo kazi yake pekee, kwa mujibu wa ibara ya 126 ya Katiba ya Muungano ya 1977, “ni kusikiliza shauri lililoletwa mbele yake na kutoa usuluhishi juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba, iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar”.

Hati hiyo ya mashitaka ilipotea mezani kwa Jumbe katika mazingira ya kutatanisha, na hatimaye kuibukia mikononi mwa Mwalimu Nyerere. Taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa waliofanikisha kazi hiyo ni pamoja na wakubwa wa sasa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wakati ule wakiwa SMZ.

Haraka haraka na hima, kikaitishwa kikao cha NEC ya CCM mjini Dodoma, Januari 1984 na Jumbe akawekwa kiti moto kwa dhambi ya kujaribu kutua mahali malaika wanapopaogopa kutua, kwa maana ya kuhoji Muungano; kisha ikatangazwa “kuchafuka kwa hali ya siasa Zanzibar”.

Bila kumeza maneno, Jumbe alikiri kuandaa hati hiyo kama moja ya haki zake za kikatiba.

Mbali na hati ya mashitaka, Jumbe aliandaa pia barua ndefu kumkumbusha Nyerere jinsi Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano zilivyokuwa zikikiukwa. Alihoji pamoja na mambo mengine, mantiki ya kuunganishwa kwa TANU na ASP kuunda CCM na mamlaka chama hicho kiliyojipa, ya kutunga Katiba ya kudumu ya 1977.

Kwa msaada wa Mwanasheria Mkuu Swanzy, Jumbe alifanya rejea Sheria ya kuahirisha na kusogeza mbele muda wa kuitisha Bunge la Katiba, Namba 18 ya 1965, Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano ya 1965, na ubatili wa Katiba ya kudumu ya 1977 kwa namna ilivyobuniwa na kutungwa.

Kwa kuwa barua hiyo ndefu ilikuwa imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, alimtaka Waziri Kiongozi, Ramadhan Haji, ahakikishe imetafsiriwa kwa Kiswahili iweze kujadiliwa na Baraza la Mapinduzi.

Kama ilivyotokea kwa hati ya mashitaka, barua hiyo nayo ilitoweka mezani kwa Jumbe katika mazingira ya kutatanisha na kumfikia Nyerere. Kwa kuwa alikuwa hajaitia sahihi ilibidi kikao cha NEC kimtake Jumbe aseme kama hayo ndiyo yalikuwa mawazo yake; naye kwa mara nyingine, na bila ya kutafuna maneno, alikiri, na hivyo mvua ya mawe ikazidi kumnyea.

Awali, Januari 12, 1984, Jumbe alihutubia wananchi kwenye kilele cha sherehe za Mapinduzi, siku chache tu kabla ya kuitwa Dodoma. Katika hotuba hiyo, hakuficha kukerwa kwa Serikali yake namna Muungano ulivyotekelezwa kinyume na matakwa asilia. Aliwataka wananchi wawe wavumilivu na wenye subira wakati tatizo hili likiendelea kushughulikiwa.

Bila kumeza maneno, na Mwalimu Nyerere akisikia; Jumbe alisema, kama pasingepatikana mwafaka na maridhiano kati ya Zanzibar na Serikali ya Muungano juu ya jambo hilo, angelipeleka kwenye Mahakama Maalumu ya Katiba kupata ufumbuzi kwa yote haya.

Katika kikao cha NEC cha Dodoma, Jumbe alielezewa kama “kiongozi dhaifu na msaliti wa Muungano”. Alipinduliwa sawia na kupoteza nafasi zote, kisha akasindikizwa nyumbani kwake na kuwekwa chini ya ulinzi wakati harakati za kusafisha hewa ya kisiasa zikiendelea.

Tetemeko likawakumba wasaidizi wake wakuu, wakiwamo Waziri Kiongozi, Ramadhan Haji, Waziri wa Nchi, Aboud Talib, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Wolfango Dourado wakati Swanzy alirejeshwa kwao Ghana.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ulinzi wa Muungano na Mjumbe wa NEC, Kanali Seif Bakari, alipigana kiume kikaoni kujaribu kumwokoa Jumbe, lakini aliishia kuwekwa chini ya ulinzi wa nyumba yake na hatimaye kizuizini Tanzania Bara.

Nafasi ya Jumbe ilichukuliwa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi, na Seif Sharrif Hamad akaukwaa Uwaziri Kiongozi.

Je, hayo yalikuwa Mapinduzi dhidi ya Jumbe, kutekwa nyara au zilikuwa hatua za kinidhamu za chama?.

Jumbe alikuwa Rais wa “nchi” ya Zanzibar kwa mujibu na kwa misingi ya Katiba ya Zanzibar ya 1979. Na kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano [Articles of Union] wa 1964, ambao ndio unaosimamia na kutawala Katiba zote mbili – Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar, suala la Vyama vya Siasa halikuwa, halijawa na halipashwi kuwa jambo la Muungano.

Kwa mantiki hii, kitendo cha chama cha siasa kumwondoa madarakani Rais wa “nchi” yenye Katiba yake, yenye Serikali yake na Bunge lisilotawaliwa na Katiba ya Muungano, ni dhahiri kilikuwa kimevuka mipaka ya uwezo wake. Kwa sababu hii, hayo yalikuwa Mapinduzi ya kutumia nguvu ya kisiasa).

Baada ya kazi ya kumpindua Jumbe kukamilika, na ili kuhakikisha “vituko” vya kuhoji Muungano vimedhibitiwa Visiwani, suala la Usalama wa Taifa, ambalo kabla ya hapo halikuwa jambo la Muungano (ilikuwa ni Ulinzi tu), liliingizwa kwenye Muungano kusomeka “Ulinzi na Usalama”.

Kitendo cha Mwalimu Nyerere cha kusimamia na kufanikisha mapinduzi dhidi ya Jumbe kupitia NEC ya CCM, chama pekee kilichoshika hatamu za uongozi wa nchi; na kitendo cha kutiwa kizuizini kwa Kanali Seif Bakari, si tu kilichochea chuki miongoni mwa Wazanzibari kwa Muungano, bali pia kilizua mgawanyiko wa makundi mawili miongoni mwa viongozi waandamizi Visiwani na hatimaye kuenea Bara.

Kundi moja ambalo halikufurahishwa na kupinduliwa kwa Jumbe na ambalo lilitaka kudumisha mapinduzi na fikra za Karume lilijiita “Wakombozi” (Liberators), na la pili lililotaka mabadiliko haraka na Zanzibar mpya, lilijiita “Wanamstari wa mbele” (Frontliners). Makundi haya yalipogongana, moto uliwaka kwa kishindo cha radi.

Kundi la “Wakombozi”, huku limesheheni chuki na hasira ya kulipa kisasi kwa Nyerere, lilisubiri nafasi na wakati mwafaka kwa tukio zito kutokea ili limpe kibano na kumdhalilisha, yeye na Muungano kwa ujumla. Jambo zito hilo lilikuwa nini? Je, kundi hilo liliweza kutekeleza azima yake?.
Chanzo: Raia Mwema

Monday 13 February 2012

Prof. Sheriff and Form 4 exam scandal

Dear Salma and the others

I think we are dealing with this question without consideringsome essential issues of rights and responsibilities, and proportionality ofcrime and punishment, and indeed even the Union question comes in.
Salma is trying to convince us that there are some terriblethings that the students have been doing – and I do not doubt it –but obviously there is a distinction between being involved in stealing aquestion paper, and one who does not know the answer who writes Bongo Fleva, orone who uses the opportunity to engage in dirty language. I can see at least 3different issues, and we cannot have a single punishment for all 3.
When I was in Form 2 a classmate of mine used the occasion tohit at British imperialism in 1957 rather than answering questions on Englishliterature, and he was failed; but he was allowed to repeat and passed the followingyear. If this could be done by our British colonial masters, why are we morebrutal than they?
Secondly, even those who did engage in stealing the paper, is athree-year punishment reasonable? To all practical purposes, a student who hasto remain out in the wild for 3 years is finished educationally. It is aneducational death sentence. Why do we want to treat so brutally our ownchildren who made a big mistake, but hopefully will learn the lesson if theyhave to repeat one year.
There is also the question about who is responsible for the examleakage – only the students? not the teachers who are supposed to supervisethe exams? how did the leaked exam papers reach all the way to far-awayvillages in Pemba where children could probably hardly afford to pay the heavy pricefor the leaked papers? Indeed, is not the Baraza la Mitihanio itself the mainculprit for allowing the exams to leak in the first place? Would it not be morejust to send the Baraza la Mitihani packing for 3 years, or even permanentlybecause they are adults who have been given an important responsibility, andfailed?
But then there is the wider question of Zanzibar in the Union. Barazala Mitihani for some reason was made a Union matter among many that were illegitimatelyadded to Union list; but education is not a Union matter. The job of the Barazais to set the exam and mark them, honorably if they can. How did they acquirethe power to determine how the Ministry of Education in Zanzibar wants to dealwith its students who made mistakes and engaged in an unruly way? They are ourchildren, and we have to take care of them in or outside the classroom. Do wein Zanzibar want to increase the gangs of malcontents who will resort to theft,drugs, etc. I say no. Let the mainland deal with the issue their way, but letus not surrender our responsibility to our children’s education or allow thepower of the Zanzibar Government to further diminish. Let this not be yetanother of the never-ending kero za Muungano.

Yours sincerely

Abdul Sheriff

Saturday 11 February 2012

Iacheni Zanzibar na bahari yake

BAHARI Kuu si suala la Muungano, na kwa hivyo bahari inayoizunguka Zanzibar na rasilimali zake isiingiliwe na watu wasio husika.
Hivyo ndivyo anavyosema Profesa Abdul Sheriff katika jawabu lake kwa Waziri Profesa Anna Tibaijuka. Kwa upande mwingine Prof. Sheriff anasema kuwa, kwa bahati mbaya kumekuwa na tabia ya kudharau na kupuuza ushiriki wa watu wa Zanzibar katika masuala nyeti na mazito yanayowagusa Wazanzibari. Prof. Sheriff anatolea mfano kitendo cha Mheshimiwa Samuel Sitta kudai kuwa Zanzibar ilishirikishwa
katika kuandaa muswada wa mabadiliko ya katiba kumbe kushirikishwa kwenyewe ni danganya toto.
Akifafanua alisema, katika suala hilo muhimu sana, Zanzibar haikushirikishwa katika vikao, lakini ilitakiwa tu kupeleka maoni yake. Waliotakiwa kufanya hivyo Waziri anayehuiska na Utawala Bora pamoja na Mwanasheria Mkuu. Kwa mujibu wa barua ya Prof. Abdul Sheriff, viongozi hao katika SMZ walitoa mapendekezo 13, lakini yakachukuliwa mawili tu huku menguine 9 yakitupwa katika pipa la taka. “Former Speaker Samuel Sita claimed that Zanzibaris were consulted, naming the Zanzibar Minister of Good Governance and the AG, but it turned out that they were asked to submit their recommendations, but adopted only two out of 13, and threw the rest in the dustbin, and then went on to add many more without consulting even the Zanzibar Government.”
Haya ndiyo anayosema Sheriff akisema kuwa ‘dharau’ hii imerejewa tena katika suala la kuongeza eneo la Bahari la Tanzania ambapo Prof. Tibaijuka anasema kuwa Zanzibar iliwakilishwa wakati si kweli. Akasema, kilichofanyika ni kumchukua Waziri Shamhuna lakini Shamhuna mwenyewe anakiri kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijui jambo hilo.
“It seems that mainland leaders feel that if you have a few Zanzibaris in your gang, then Zanzibaris are represented – and it is never difficult to get a few vibaraka, as we know all too well from our history. The question is whether the people in Zanzibar even knew this business was cooking.” Anasema Prof. Sheriff
akimaanisha kuwa katika dharau zake, Tanzania Bara inadhani kuwapata vibaraka wachache, ambao sitabu kuwapata, basi inaweza kuwaburuza Wazanzibari. Anasema, katika suala hili la Tanzania (Bara) kujiongezea mipaka ya baharini, Zanzibar haina hata habari kwamba kuna jambo hilo. Katika nasaha zake Profesa Sheriff anakumbusha kuwa katika yale mambo 11 ya muungano, bahari haimo. Lakini anaongeza kwa kusema kuwa japo hata katika hii ‘jinai’ ambayo imefanywa ya kuongeza mambo ya muungano na kuwa 22 bila kufuata utaratibu, bado bahari kuu na rasilimali zake haipo katika hayo 22. Katika hali hiyo, Prof. Sheriff anamtaka Waziri Tibaijuka kuwaomba radhi Wazanzibari, kwanza kwa kutaka kuwaburuza katika jambo muhimu kama hili, na pili kwa kujaribu kuwagawa kwa kulifanya jambo hili kwamba ni la Jussa wakati ni la Wazanzibari wote. Lakini kama neno l a ziada, Waziri Tibaijuka
akatakiwa kuzingatia busara ya mkongwe wa siasa nchini Mzee Nassoro Moyo pale alipomwambia Samuel Sita kwamba asidhanie kizazi cha vijana wa sasa ni wale wa kale wa “hewala bwana.”
Chanzo: Annur

Friday 10 February 2012

Matokeo ya mitihani F4 ni janga la Taifa Zanzibar

Kwa kweli hili ni janga kwa mustakbali wa elimu ya Zanzibar, Nahisi tatizo ni kuwa kuna mtiririko mrefu wa masuali ya kujiuliza na pia wahusika ambao wanahitajika watiwe hatiani kabla ya hao watoto kufutiwa matokeo.

1. Baraza la mitihani lenyewe inakuwaje mitihani ivuje, definitely wao ndio ambao wanavujisha mitihani
2. kama mitihani imefutwa kwa wanafunzi, mfano Haile salasie hakuna wasiwasi kwa mazingira ya Zanzibar lazima Ben bela nao watapata, so kama kufutiwa wafutiwe wote.
3. Ndalichako anajitetea tuu ila madudu yote yako huko baraza la mitihani ambako wanavujisha mitihani kwani haiwezekani pia mitihani ivuje Zanzibar wakati baraza la mitihani liko Dar.
4. Hapa mitihani inahitajika irudiwe kwani mbona wao mitihani ya darasa la saba wameirudia kwa sababu walifkiria mustakbali wa watoto wao so na sisi pia kwa kuzingatia maslahi ya vijana wetu mitihani irudiwe. 


Then Serikali ya Zanzibar ishikie bango baraza la mitihani libebe jukumu lote la madudu yaliyotokea badala ya kuunda tume zisizokuwa na maana wala hatuoni result zake au tujipange tutengeneze baraza letu hilo linawezekana pia.

Wednesday 8 February 2012

Jinsi Nyerere alivomtia hofu Karume

Na Ahmed Rajab
KUFIKIA mwanzoni mwa mwezi wa Aprili mwaka 1964, kama miezi mitatu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, mambo Visiwani humo yalikuwa shwari. Hali ya kisiasa ilikuwa thabiti na hivyo mazingira ya kijamii nayo yalikuwa mazuri.

Mandhari ya kisiasa ya wakati huo yalikuwa ya kimapinduzi.  Hata steshini ya Redio ya Serikali iliacha kupiga nyimbo za taarab zilizokuwa na maudhui ya kimapenzi.  Badala yake ikipiga nyimbo kuwaenzi wakwezi na wakulima na nyingine kuhusu Mapinduzi ya Januari 12, 1963.

Serikali ya Mapinduzi, ikiongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume, ilikuwa Serikali iliyokuwa na umoja. Wakati huo ilikwishaanza kuchukua hatua mbalimbali zilizokuwa na lengo la kuleta usawa katika jamii. 

Hatua hizo, zikiwa pamoja na kutoa huduma bure za afya na elimu bure kwa watoto wote na kutaifisha ardhi, ziliwavutia wananchi wengi wa kawaida katika nchi nyingine za Afrika ya Mashariki. 

Iwapo kuna wataosema kwamba hatua hizo hazikufanikiwa, ni swali jingine. Ukweli ni kwamba hatua hizo zilizitia homa serikali fulani.  Haikustaajabisha kwamba mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12 wanajeshi waliasi nchini Tanganyika (Januari 20), Uganda (Januari 23) na Kenya (Januari 24).  Uasi huo haukushangaza kwa vile serikali za nchi hizo hazikuonyesha ari ya kuchukua hatua kama zile za Zanzibar ambazo zingewanyanyua watu wao. 

Lakini labda waliotishika zaidi walikuwa wakubwa wa serikali za Kimagharibi.  Pamoja na mengine walitishika na jina jipya la ‘Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.’  Nchi hiyo haikuwa Jamhuri tu ya kawaida baada ya kuondoshwa usultani lakini ilijitambulisha rasmi kuwa ni ‘Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.’ 

Kulikuwa tofauti kubwa kiitikadi kati ya nchi iliyokuwa ikijiita ‘Jamhuri’ na ile iliyokuwa ikijinata kuwa ni ‘Jamhuri ya Watu.’

Isimu hiyo ya pili ikitumiwa na serikali zilizokuwa zikijigamba kwamba zinatawala kwa maslahi ya wengi wa watu wao. Kinyume na Zanzibar lakini nyingi ya serikali hizo zikifuata itikadi ya kisiasa ya Kimarx na Kilenin au ya Kikomunisti.

Kufikia mwanzoni mwa Aprili 1964 wengi wa Wazanzibari walikuwa wamekwishayakubali Mapinduzi kuwa ni kudura ya Mungu. Watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida. 

Vituko vya watu kufukuzwa kazini kwa sababu za kikabila au za kisiasa vilizuka baadaye pamoja na visa vya kamatakamata na misiba ya mauaji.

Serikali ikiwapeleka nchi za nje kwa masomo ya juu wanafunzi wa kila kabila na ikiendesha shughuli zake kwa nidhamu. Hakukuwa na segemnege katika uendeshaji wa vyombo vya dola.

Ingawa mazingara yalikuwa tofauti na yale ya serikali iliyopinduliwa, watumishi wakuu wa serikali waliiendesha nchi kwa mujibu wa sheria zilizokuwapo na mpya zilizotungwa na Baraza la Mapinduzi. 

Hali hiyo iliyodumu kwa muda mfupi iliwafanya wengi wawe na matumaini na mustakbali wa taifa lao jipya. Leo tukikaa na kuipima hali ya mambo ilivyokuwa hatuoni ushahidi kwamba utawala wa Karume ulikabiliwa na kitisho kikubwa cha kutaka kuuangusha. 

Sisemi kwamba hakujakuwako watu waliokuwa wakiiapiza serikali yake na waliokuwa wakiomba isambaratike au ipinduliwe moja kwa moja.  Walikuwepo. Lakini nguvu zao za kuandaa mapinduzi ya kuyapinga Mapinduzi ya Januari 12 zilikuwa dhaifu. Hakuna mpinga Mapinduzi aliyethubutu kufurukuta wakati huo. 

Tarehe Aprili 13 Karume alimwambia Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Salim Rashid, kwamba Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Tanganyika, alimpigia simu akimtaka ende Dar es Salaam. Siku ya pili yake Karume na Salim Rashid wakafunga safari kwenda kwa Mwalimu.

Walipofika Ikulu, Dar es Salaam, Mwalimu huku akimuangalia Salim Rashid aliwaambia wasaidizi wake: ‘Mpeni gari (Salim) akanyoe ndevu.’

Ni wazi kuwa Nyerere hakutaka Katibu wa Baraza la Mapinduzi asikie aliyokuwa amepanga kumwambia Karume. Ndipo Salim Rashid akashika njia kwenda kwa kinyozi akimuacha Karume na Mwalimu.  Mbali ya Marais hao wawili hakuna mtu anayejuwa kwa uhakika nini hasa kilijiri kati yao sebleni Ikulu.

Kuna wanaoshikilia kwamba Nyerere alimtisha Karume kwa kumwambia kulikuwa na njama za kumpindua na kwamba muungano wa nchi zao utampa himaya.

Na kuna wasemao kwamba wakati huohuo Nyerere alisema atawarejesha kwao askari polisi 300 Wakitanganyika waliokuwa na silaha na waliopelekwa Zanzibar kusaidia kuzuia fujo.

Miaka michache kabla ya hapo Karume aliwahi kutaja  nia yake ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika na kuifanya iwe jamhuri.  Kauli hiyo, aliyoitoa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na iliyoripotiwa kwenye gazeti la Mwongozo la chama cha Zanzibar Nationalist Party (maarufu kwa jina la Hizbu), ilimchongea baadaye amuangukie na kumtaka radhi sultani wa wakati huo Seyyid Khalifa bin Haroub.

Ingawa tangu hapo Karume alikuwa na ndoto ya Muungano wa Zanzibar na Tangayika hatujui akitaka uundwe kwa masharti gani au uwe wa aina gani.  Tunachoweza kufikiria ni kwamba matamshi ya Nyerere ya Aprili 14 yalimtia hawafu kubwa Karume kiasi cha kumfanya ampe mwenzake aliyemzidi akili uhuru kamili wa kuziunganisha nchi zao. 

Aliporejea Zanzibar Karume aliwaficha memba wenzake wa Baraza la Mapinduzi alichokubaliana na Nyerere.  Siri ya Muungano ilikuwa yake peke yake Zanzibar.  Hakulishauri Baraza la Mapinduzi, hakuishauri serikali wala hajakishauri chama cha Afro-Shirazi Party (ASP).

Wadadisi na wataalamu wengi wenye kuitalii kwa kina historia ya Muungano wanaamini kwamba ingawa Nyerere alikuwa mtetezi wa umoja wa Afrika na ingawa Karume alikwishadokeza kwamba angependelea Zanzibar na Tanganyika ziungane, Muungano ulioundwa Aprili 26 mwaka 1964 uliandaliwa ili kuliridhia matakwa ya dharura ya Marekani.

Wakati huo Marekani kwa kweli ilikuwa hamnazo, majununi kabisa, kuifikiria Zanzibar kuwa ngome ya ukomunisti upande wa Afrika ya Mashariki na kitisho kwa maslahi yake. Marekani ikawa mbioni kutafuta njia au mamba wa kuyameza Mapinduzi ya Zanzibar.

Siku tatu au nne baada ya huo mkutano wa siri wa Marais wawili Karume alipelekewa Hati za Muungano kutoka Dar es Salaam.  Hati hizo alikabidhiwa Ikulu ya Zanzibar na aliyekuwa waziri mdogo wa mambo ya kigeni wa Tanganyika.

Hii leo mustakbali wa Zanzibar uko njia panda kama ulivyokuwa pale Karume na Nyerere walipoziunganisha nchi zao. Lakini hali halisi za Aprili 1964 na za leo zimebadilika sana.   Hii ni kwa sababu kwanza hali ya ndani ya Zanzibar kwenyewe imebadilika; pili, mahusiano yake na nchi zilizo ngeni kwake yamebadilika na tatu, mazingara ya ulimwengu pia yamebadilika.

Mnamo Aprili 1964 mustakbali wa Zanzibar uliamuliwa kwa njama zilizoandaliwa na Marekani pamoja na madola mengine ya Kimagharibi, ambayo tunaweza kuyabandika lakabu ya ‘wapishi wa kimataifa’.  Mpishi mwengine alikuwa jirani Tanganyika.

Kama inavyokumbushwa mara kwa mara Muungano uliopo leo sio ule ulioelezwa na Hati za Muungano, zilizokuwa na mambo 11 tu ya Muungano. Kwa muda wa miongo kadhaa Zanzibar ikiachiwa ijiendeshe yenyewe.

Kwa mfano, ilikuwa na uhuru kamili wa kisiasa toka 1964 hadi 1972 alipouliwa Sheikh Karume.

Kwa upande wa uchumi serikali za Zanzibar ziliendelea kuwa na uhuru kamili mpaka ilipoingia ile ya awamu ya tano ya Rais (Mstaafu) Salmin Amour. Serikali hiyo ilishindwa nguvu na shinikizo za Bara. Ikabidi isalimu amri na kuchanganya sera yake ya fedha pamoja na kodi na ushuru na ile ya Bara (yaani ya serikali ya Muungano).

Tukiuzingatia umoja walio nao Wazanzibari na matarajio yao kwa Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa, halitokuwa la ajabu iwapo mchakato utaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania utayathibitisha matakwa yao.

Matakwa hayo yatabainika watapotoa maoni yao kwenye Tume ya Katiba na yataonyesha kuwa wengi wao watataka pawepo Muungano wa Mkataba na si wa Katiba.

Ushahidi kwamba hali ya mahusiano ya Zanzibar na Muungano ni tofauti na ilivyokuwa zamani ni ile migogoro isiyokwisha kati ya pande hizo mbili. Shtuma zilizoko Visiwani ni kuwa Serikali ya Muungano yenyewe ndiyo inayoianzisha migogoro hiyo, kama kwa mfano kwa kuandikiana mikataba na jumuiya za kimataifa kwa niaba ya Zanzibar au kwa kuwa na makubaliano ya kibalozi kwa niaba ya Zanzibar na madola ya nje, mfano Norway.

Serikali ya Tanzania haina haki ya kufanya hivyo hata ikiwa sekta zote zinazohusika za utawala ziko chini ya mamlaka yake. Na hivyo sivyo ilivyo. Tena haina haki hiyo kwa sababu mfumo wa Muungano uliopo sasa si wa kudumu kwa vile kuna huu mchakato wa kuamua kuhusu majaaliwa ya Muungano wenyewe pamoja na mfumo wake na katiba yake.

Wakuu wa Bara watapata taabu Zanzibar na huenda hata wakahatarisha usalama endapo watajaribu kushikilia kwamba mfumo uliopo sasa wa Muungano uendelezwe kama ulivyo.

Hatimaye tukumbuke kuwa ulimwengu nao pia umebadilika. Tujuavyo, tena kwa uhakika,  ni kuwa kinyume na mwanzoni mwa 1964 hii leo nchi kadhaa za Kimagharibi ziko tayari kuiunga mkono Zanzibar ikiwa itadai mamlaka yake kamili kutoka Serikali ya Muungano. Tumeyadaka haya faraghani yakidondoka kutoka ndimi za wanabalozi wa nchi fulani wasiotaka kutajwa.
Chanzo: Raia Mwema

Tuesday 7 February 2012

Chongowe avuliwa Pakistan

Nyangumi akipandishwa kwa Crane kutoka kwenye maji

Fishermen in the Pakistani port of Karachi got more than they bargained for Tuesday as they reeled in one of the biggest fish in the sea: a whale shark.
The Express Tribune, a Pakistani newspaper, reported that the 40-foot fish was first spotted ten days ago in seas about 150 km (93 miles) from the city. Mehmood Khan, the owner of a local fishery, said the shark was unconscious at that time and other reports said that it was found dead Tuesday.
A large crowd gathered as a succession of cranes were brought in to lift the shark on to the pier. After several hours and a number of failed attempts, the leviathan was finally brought ashore and promptly sold for 1.7m Rupees ($18,750).
The whale shark was added to the World Conservation Union's list of threatened species in 2008.