Saturday 31 December 2011

SMZ macho kuimarisha huduma za jamii- 2012

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), mwaka huu imeahidi kuendelea kuimarisha miundombinu na ubora wa huduma za jamii zikiwemo elimu, afya na maji safi na salama.
Hayo yalisemwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein katika risala yake ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2012, aliyoitoa Ikulu,
mjini hapa.
Aidha katika risala yake, Dk. Shein alieleza kuwa katika mwaka 2012, Serikali itaongeza
ushirikiano na sekta binafsi ili kwa pamoja kufikia lengo la kukuza uchumi na kupunguza
umasikini.
Katika kukabiliana na athari za uchumi wa dunia hususan ongezeko la bei ya chakula alisema
serikali itaimarisha sekta ya kilimo.
Akieleza mipango ya kiuchumi kwa mwaka 2012 Dk. Shein alisema kuwa Serikali inaazimia
kuzidi kuongeza ukusanyaji wa kodi na kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Dk. Shein alisisitiza kuwa katika kuelekea mwaka 2012 kuna mambo muhimu ya
kuyazingatia na kuyatekeleza ipasavyo kwa ustawi wa maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na
kuimarisha amani na utulivu
Chanzo: Habari leo

Thursday 29 December 2011

Zanzibar iwe na Benki kuu yake: Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.  

Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.  

Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar.  

“Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwiano huo ni mbaya katika suala la utoaji vipaumbele kwa maendeleo ya visiwani,” alisema Maalim Seif.  

Alisema umuhimu kwa Zanzibar kuwa na benki kuu yake sio jambo jipya, kwani hata awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweka wazi madai ya aina hiyo ikitaka kila upande uwe na mambo yake katika masuala ya kibalozi, shughuli za polisi, uraia na sarafu.  

Alisema wakati wa kutoa maoni juu ya Katiba mpya, pamoja na kudai haki ya kuwa na benki kuu, wananchi waungane ili maoni yao yaweze kusaidia upatikanaji wa katiba itakayoondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.  

Maalim Seif alisema ukosefu wa umoja miongoni mwa wananchi katika suala la kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Katiba mpya ni hatari kwa utaifa wao.  

“Utakapofika wakati wa kutoa maoni tusahau itikadi zetu, tuungane kulinda maslahi ya Zanzibar, vyama vya siasa ni taasisi za kupita, ASP haipo, Tanu haipo na ZNP haipo, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo,” alisema.  

Maalim Seif pia alisisitiza msimamo wa kutaka Katiba mpya itakayoundwa iweke utaratibu unaoruhusu mzunguko wa madaraka ya nafasi ya rais wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.  

“Mwandishi mmoja wa habari juzi alitaka nieleze maslahi ya Zanzibar ninayowahimiza wananchi kudai yawekwe ndani ya Katiba mpya, nikamwambia mfumo wa sasa wa uchaguzi umesbabisha nafasi ya rais wa muungano kubaki bara kwa muda mrefu,” alisema Maalim Seif akiwa anarejea jibu alilotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari baaya kuulizwa swali hilo na Muhibu Said, Mwandishi wa habari mwandamizi wa NIPASHE.  

Akifafanua zaidi haja ya kuwepo utaratibu wa kikatiba unaoruhusu nafasi hiyo kutolewa kwa mzunguko, Maalim Seif alisema chini ya mfumo wa uchaguzi uliopo Zanzibar imeshika nafasi hiyo kwa miaka 10 tu wakati Tanzania bara imehodhi wadhifa huo kwa miaka 35. 

Alisema hiyo ni kasoro katika uendeshaji wa serikali ya muungano iliyoundwa na mataifa mawili ambayo ni nchi.
Chanzo: Nipashe

Wednesday 28 December 2011

Muungano Sasa uwe wa mkataba, sio katiba

Na Ahmed Rajab
KUNA sababu moja kuu inayowafanya Watanzania waukaribishe kwa msisimko mwaka mpya wa 2012. Nayo ni kwamba, mwakani ndipo suala la Katiba mpya ya nchi hiyo litapoanza hasa kutokota. Hatuhitaji wapiga ramli kutwambia kwamba mwaka ujao hilo ndilo litalokuwa suala kubwa la kisiasa nchini Tanzania.
Kwanza kuna wenye kuupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 kama ulivyo hivi sasa. Wanahoji kwamba muswada huo una taksiri kadha wa kadha ambazo zitazuia isipatikane Katiba iliyo halali na itayotungwa kwa kuwashirikisha vilivyo wadau wote wanaostahiki kushirikishwa.
Miongoni mwa wapinzani hao ni asasi za kiraia ambazo zitaendelea kuupinga muswada huo kwa hamasa kuu na wataishtaki Serikali mahakamani katika jaribio la kuuzuia. Wakishinda mahakamani watakuwa wamepata mradi wao.
Wakishindwa wataendelea kuwa nguvu ya kutosha itayoweza kuwashawishi wananchi waikatae Katiba itayoibuka baada ya kumalizika kwa mchakato wake.
Hata hivyo, wakati wa mchakato wa kuipitia upya Katiba wanasiasa wa Tanganyika na viongozi wao watakabiliwa na hali wasiowahi kukutana nayo kabla.
Kwa mara ya kwanza huko Zanzibar, kuna mjadala mkubwa unaoendelea ndani na nje ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuhusu mustakabali wa visiwa hivyo.
Hilo ni jipya kwani hapajawahi kutokea hali kama hiyo kabla. Tena majadiliano hayo si ya kulazimishwa bali ni ya hiari na Wazanzibari wanatoa maoni yao kwa uhuru kamili.  Wanafanya hivyo wakitambua kwamba fursa waliyonayo sasa huenda wasiipate tena.
Wanaelewa vyema umuhimu wa kuwa na msimamo mmoja ili waweze kuigomboa nchi yao. La sivyo, wakichezacheza na wasipoungana kifikra basi fursa hiyo inaweza ikawaponyoka, wakajikuta wamekwenda kape.
Katika hayo majadiliano kuhusu mustakabali wa Zanzibar suala la Muungano ndo jambo kubwa linalozungumzwa Visiwani.  Muungano unajadiliwa mijini, vijijini na kwenye vitongoji Unguja na Pemba.  Ukiwasikiliza wananchi wa huko utawasikia wanataka irejee Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ikiwa ni dola kamili iliyo huru ikiwa na funganisho na Tanganyika pamoja na nchi nyingine za eneo hili. Tofauti ya mahusiano yaliyopo sasa na hayo wayatakayo ni kwamba wangependelea huo mfumo mpya wa mahusiano ya kufungamana uwe wa mikataba na si wa Katiba.
Msimamo huo ni sehemu ya ile iitwayo Ajenda ya Zanzibar niliyowahi kuizungumzia miezi kadhaa iliyopita.  Ni ajenda inayopigiwa debe na wengi wa Wazanzibari wakiwa pamoja na viongozi wao kutoka vyama tofauti vya kisiasa.
Wengi wao wanaamini kwamba kutokana na Hati za Muungano na mambo mengine yaliyoingizwa kuwa ni ya Muungano rais wao amepungukiwa na madaraka. Na si yeye tu bali pia na baraza lao la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi) na Mahakama yao.  Mamlaka ya taasisi zote hizo tatu za Zanzibar, ambazo ni mihimili mikuu ya dola, yamepunguzwa katika kipindi cha miaka 47 ya Muungano.
Kilichotokea ni kwamba kwa muda wote huo unaokaribia nusu karne mamlaka au madaraka yote ya Zanzibar yaliyo muhimu yamehaulishwa Tanganyika. 
Ujanja ulitumika kulifanya Bunge la Tanganyika liwe Bunge la Muungano na kuigeuza Katiba ya Tanganyika iwe Katiba ya Muungano. Ujanja vilevile ulitumika kuifanya Serikali ya Muungano iwe ndiyo Serikali ya Tanganyika na ya Tanganyika iwe ya Muungano. Shughuli za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na za Jamhuri ya Tanganyika zimekuwa zikiendeshwa na Serikali moja. 
Kwa upande mwingine, Zanzibar na Serikali yake hazina jukumu kubwa au la maana katika utawala na uongozi wa Muungano.
Ingawa kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa na kwa mujibu wa Hati za Muungano, Zanzibar na Tanganyika ni washirika wenye hadhi sawa ndani ya Muungano, mambo yanavyokwenda ni kwamba Zanzibar imewekwa kando. 
Zanzibar imetoweka hata kutoka kwenye ramani ya dunia na haina jukumu lolote la maana katika shughuli za eneo letu la Afrika Mashariki au la Afrika au ulimwenguni kwa jumla.  Wala Zanzibar haipati manufaa yoyote inayopata nchi yenye kushiriki katika uchumi wa dunia; isitoshe, hairuhusiwi kujihusisha na taasisi za kimataifa.
Hii leo wanasiasa wa Tanzania Bara hawawezi tena kuyapuuza manung’uniko na matakwa ya Wazanzibari kwa sababu wamekwishatanabahi kwamba Muungano kwa namna ulivyo sasa, uko kwenye njia panda na wakati umefika wa kufanya uamuzi muhimu kuhusu mustakabali wake.
Kwa sasa hakuna anayeweza kutabiri nini yatakuwa matokeo ya mchakato wa kuiandika upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.  Ingawa hakuna jedwali rasmi lililowekwa, inavyoonyesha ni  kwamba kabla ya Juni 2012 Wazanzibari watapata fursa ya kutoa maoni yao pale Tume ya Kuichunguza Katiba au wawakilishi wake watapozitembela shehia za Unguja na Pemba.
Hii si mara ya awali kutungwa Katiba ya Muungano wa Tanzania. Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba safari zilizopita Wazanzibari na wawakilishi wao ama hawakushauriwa ipasavyo au walijikuta wanayakubali bila ya upinzani wowote, matakwa ya Tanzania Bara.
Mnamo miaka ya 1990 palitolewa pendekezo la kutaka pawepo na mfumo wa serikali tatu, yaani Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano. Waliopendekeza hivyo waliamini kwamba mfumo huo wa serikali tatu ndio ulio bora na utaokubaliwa na washirika wote wawili, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Kwa hakika, baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa Tanganyika nao walifanya jaribio la kuifanya nchi yao iwe na serikali yake ndani ya Muungano. Jaribio hilo halikufika mbali kwani Mwalimu Julius Nyerere alitumia nguvu zake za turufu na kulizima suala hilo.
Pendekezo hilo liliibuka tena lilipotolewa kwa mara nyingine na Tume ya Muungano iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Robert Kisanga. Rais wa Muungano wa wakati huo, Benjamin Mkapa naye alilipinga.
Hatujui ikiwa huo ndio mwisho wa pendekezo hilo au iwapo Serikali ya Muungano italikubali kuwa njia murua ya kuunusuru Muungano usiporomoke. Iwapo Serikali ya Muungano hatimaye italikubali pendekezo hilo hatujui kama Wazanzibari nao wataliridhia kwa vile pendekezo hilo ukiliangalia kwa undani haliipi nchi yao uhuru wake kamili bali linauwekea mipaka. Muungano huo wa serikali tatu utakuwa Muungano utaojengwa juu ya misingi ya Katiba na si mkataba.
Ndio maana siku hizi huko Zanzibar mazungumzo kuhusu Muungano ni ya kutaka serikali mbili. Wazanzibari wengi wanahisi kwamba ule mfumo wa serikali tatu za Muungano umekwishapitwa na wakati. Wanapotoa hoja zao wanasema kwamba mfumo huo labda ungekubalika katika miongo iliyopita lakini si mnamo mwaka 2015.
Hata wale wenye kuunga mkono mfumo wa serikali tatu sasa wanasema kwamba ile serikali ya tatu, yaani ya Muungano, isiwe na mamlaka mengi kwani wanachotaka ni Zanzibar kuwa na uhuru zaidi ndani ya mfumo mpya wa Muungano.
Hao Wazanzibari wenye kutaka Muungano utaoundwa juu ya misingi ya Mkataba na sio Katiba wanahoji kwamba mfumo wa Muungano wa Mkataba ndio ufaao kwa mataifa yaliyo huru. Wanaendelea kuhoji kwamba hakuna haja ya kuwepo Serikali ya Tanzania. Badala yake, wanasema, pawepo Tume Maalumu ya Muungano itayokuwa na nguvu hafifu au mamlaka machache na itayosimamia vifungu vya Mkataba wa Muungano.
Mfano wanaoutaja mara kwa mara ni ule wa Tume ya Muungano wa Ulaya. Wanataka Muungano wao uwe mithili ya ule wa Ulaya ambao umeundwa kwa mikataba ya kimataifa kati ya nchi 27 zilizo huru.
Majaribio ya kutaka pawepo Katiba moja ya Muungano huo yalikataliwa pale palipofanywa kura za maoni katika baadhi ya nchi wanachama.  Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Muungano huo kila nchi ina kura ya turufu, na inaweza kujivuta na kujitoa kutoka kwenye Muungano kwa vile maamuzi yote makuu hukatwa kwa nchi kukubaliana. 
Wazanzibari wenye kuupigania mfumo huo wanasema kwamba mfumo huo si kwamba unazifaa nchi za Zanzibar na Tanganyika tu bali pia ni mujarab kwa bara zima la Afrika. Bara hilo nalo linahitaji kuwa na chombo kitachoziunganisha nchi zake zote kwa maslahi ya nchi wanachama.
Kuna jambo moja tu lenye uhakika katika mchakato wa kuiangalia upya Katiba ya Muungano. Nalo ni kwamba hatima ya Muungano itategemea sana juu ya kura ya maoni.
Watanganyika na Wazanzibari wataulizwa iwapo wanaidhinisha na kuiunga mkono au wanaipinga Katiba mpya ya Muungano. Jibu litalopatikana ndilo litaloamua kama Muungano utadumu ama la na ikiwa utadumu utakuwa na umbo au sura gani.

Source: Raia Mwema

Pesa Yetu hiyo kabla ya Muungano

Pesa ya Zanzibar Kabla ya uhuru na pia kabla ya muungano








Mimi hapa nimegunduwa kitu ambacho ni muhimu sana, hebu tizameni hawa watu walivokuwa wanachuma karafuu hapa ni 1916, walikuwa wanatumia ngazi kama majukwaa ila hebu tutizameni leo hii watu wanachuma karafuu kwa kuupanda mkarafuu wenyewe, nawaulizeni tuu jee wao hamuoni walikuwa wako more advanced kuliko sisi? na hapa jee tatizo la vifo na majeruhi zitakuwepo?

Tuesday 27 December 2011

SERIKALI IMEJIZATITI KUONGEZA UZALISHAJI WA MITI MIPYA YA MIKARAFUU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Bw Ali Mchumo ambae Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa pamoja na masuala ya bidhaa {cfc }   ulio chini ya Shirika la kimataifa la Unctad hapo afisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimueleza mipango ya Smz katika kukusudia kuimarisha zao la karafuu Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa {cfc } uliochini ya Shirika la kimataifa la Unctad.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti kuongeza uzalishaji wa Miti mipya ya mikarafuu katika mfumo wa kitaalamu zaidi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo hapo ofisini kwake Vuga wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa { CFC } Balozi Ali Mchumo ulio chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la UNCTAD wenye makao makuu yake Mjini Amsterdam Nchini Uholanzi.
Balozi Seif alisema Serikali pia inaangalia uwezekano wa kuimarisha Miembe iliyopo ambayo embe zake zinaweza kurejea katika soko la kimataifa iwapo zitashughulikiwa Kitaalamu.
Makamu wa Pili wa Rais alieleza kwamba kumekuwa na upungufu mkubwa wa Zao la karafuu kutokana na mingi kuzeeka wakati mengine ilikuwa ikikatwa ovyo kwa ajili ya kuni na Mkaa.
Balozi Seif alimuomba Balozi Mchumo kupitia Taasisi yake kuangalia uwezekano wa kusaidia Elimu na Fedha kwa Wakulima ili kuwapa uwezo wa kuzalisha katika kiwango kinachokubalika Kimataifa.
“ Tumekuwa na maeneo mengi ya miti ya mikarafuu ambayo ina rutba ya kutosha. Hivyo tunalazimika kuyajaza lakini katika mfumo wa Kitaalamu zaidi ”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alimpongeza Balozi Ali Mchumo kwa kazi yake nzuri inayoleta tija kwa Taifa katika masuala ya Bidhaa na kumuomba aendelee kuitangaza Karafuu kama Zao la Taifa la Zanzibar Kimataifa.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa { CFC } Balozi Ali Mchumo alisema Taasisi yake imekuwa ikitoa Taaluma na kusaidia katika Mazao ya Katani, Pamba, Korosho pamoja na Miembe.
Balozi Mchumo alisema Taasisi hiyo imejipanga kusaidia Taaaluma na Harakati za Kilimo cha Umwagiliaji Maji ambapo inaangaliwa uwezekano wa kujumuisha pia Zanzibar.
Mkurugeni Mtendaji huyo wa CFC ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutekeleza majukumu yake katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Alisema Dunia imeshuhudia utulivu uliopo Zanzibar hivi sasa kutokana na mfumo huo. Hivyo amesisitiza haja ya kuendelezwa amani iliyopo ambayo ndio Sera ya Taifa la Tanzania.
Katika mazungunzo hayo Balozi Ali Mchumo amekabidhi ubani wa Shilingi milioni mbili kama mchango wake binafsi na Familia yake kusaidia mchango wa Maafa kutokana na ajali ya Meli ya M.V Spice Islanders iliyotokea mwezi Septemba mwaka huu.
Balozi Ali Mchumo anatarajiwa kumaliza utumishi wake wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa {CFC} ulio chini ya UNCTAD mwezi Agosti Mwaka 2012.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

27/12/2011

Monday 26 December 2011

Maalim Seif: Zanzibar iwe na Benki Kuu yake

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.  

Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.  

Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar.  

“Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwiano huo ni mbaya katika suala la utoaji vipaumbele kwa maendeleo ya visiwani,” alisema Maalim Seif.  

Alisema umuhimu kwa Zanzibar kuwa na benki kuu yake sio jambo jipya, kwani hata awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweka wazi madai ya aina hiyo ikitaka kila upande uwe na mambo yake katika masuala ya kibalozi, shughuli za polisi, uraia na sarafu.  

Alisema wakati wa kutoa maoni juu ya Katiba mpya, pamoja na kudai haki ya kuwa na benki kuu, wananchi waungane ili maoni yao yaweze kusaidia upatikanaji wa katiba itakayoondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.  

Maalim Seif alisema ukosefu wa umoja miongoni mwa wananchi katika suala la kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Katiba mpya ni hatari kwa utaifa wao.  

“Utakapofika wakati wa kutoa maoni tusahau itikadi zetu, tuungane kulinda maslahi ya Zanzibar, vyama vya siasa ni taasisi za kupita, ASP haipo, Tanu haipo na ZNP haipo, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo,” alisema.  

Maalim Seif pia alisisitiza msimamo wa kutaka Katiba mpya itakayoundwa iweke utaratibu unaoruhusu mzunguko wa madaraka ya nafasi ya rais wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.  

“Mwandishi mmoja wa habari juzi alitaka nieleze maslahi ya Zanzibar ninayowahimiza wananchi kudai yawekwe ndani ya Katiba mpya, nikamwambia mfumo wa sasa wa uchaguzi umesbabisha nafasi ya rais wa muungano kubaki bara kwa muda mrefu,” alisema Maalim Seif akiwa anarejea jibu alilotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari baaya kuulizwa swali hilo na Muhibu Said, Mwandishi wa habari mwandamizi wa NIPASHE.  

Akifafanua zaidi haja ya kuwepo utaratibu wa kikatiba unaoruhusu nafasi hiyo kutolewa kwa mzunguko, Maalim Seif alisema chini ya mfumo wa uchaguzi uliopo Zanzibar imeshika nafasi hiyo kwa miaka 10 tu wakati Tanzania bara imehodhi wadhifa huo kwa miaka 35. 

Alisema hiyo ni kasoro katika uendeshaji wa serikali ya muungano iliyoundwa na mataifa mawili ambayo ni nchi.  
Chanzo: Nipashe

Saturday 24 December 2011

Wazanzibari tuungane kwa sauti moja katiba mpya- Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amezungumzia tena baadhi ya mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kutoa maoni ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka viongozi na wananchi kuungana katika kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano.
Amesema iwapo Wazanzibari wataungana na kuwa na sauti moja juu ya jambo hilo, kauli yao itakuwa na nguvu na upande wa pili wa Muungano utalazimika kuheshimu maamuzi hayo ya wazanzibari.
“Viongozi na wananchi wote tushikamane na tuweni na kauli moja juu ya jambo hili, na kamwe tusikubali kugawanywa kwa maslahi ya nchi yetu”, alisema Maalim Seif.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameeleza hayo katika viwanja vya demokrasia Kibandamaiti mjini Zanzibar wakati akiwahutubia maelfu ya wanachama na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliotishwa na CUF.
Amebainisha baadhi ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa na kuingizwa katika katiba mpya kuwa ni haja ya Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa ni nia moja wapo ya kudhibiti uchumi wake.
Mambo mengine ni pamoja na Zanzibar kuweza kuwa na sauti huru juu ya sera zake za fedha na uchumi ikizingatiwa kuwa suala la uchumi si katika mambo ya Muungano,sambamba na serikali kuendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka suala la mafuta liondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano.
Maalim Seif amefahamisha kuwa Zanzibar inastahiki pia kuwa na uwezo wa kuweka viwango vyake vya kodi, pamoja na kuwa na mitaala yake ya elimu inayoendana na mazingira ya Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibari.
Wiki iliyopita Maalim Seif alielezea umuhimu wa kuwepo utaratibu maalum wa kikatiba utakaoruhusu nafasi ya Urais wa Muungano kutumikiwa kwa awamu kati ya Tanzania bara na Zanzibar, tofauti na utaratibu uliopo sasa ambao hautoi fursa kwa Wazanzibari kuitumikia nafasi hiyo kubwa kabisa ya uongozi nchini.
Aidha Makamu wa Kwanza wa Rais alitumia fursa hiyo kutoa mkono wa pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na baadhi ya wananchi hasa wa mkoa wa Dar es Salaam kupoteza maisha yao, hali iliyosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa.
Amesema mwisho mwa mwezi huu chama chake kimepanga kuzitembelea kambi wanazoishi watu walioathirika na kupoteza makaazi kutokana na mafuriko hayo kwa lengo la kutoa pole na mchango wake kwa waathirika hao.
Wakati huo huo Naibu Katibu mkuu wa CUF Zanzibar Mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu amewataka wanachama wa chama hicho kupuuza uvumi juu ya mgogoro ndani ya Chama hicho, na kwamba chama hakina mgogoro na kiko imara wala hakitumbi.
Amesema uvumi huo unaosambazwa kupitia vyombo vya habari umekuwa ukitolewa kwa malengo maalum ya kukivuruga chama, malengo ambayo amesema hayatofanikiwa.
Nae mkurugenzi wa haki za binadamu, habari na mawasiliano ya umma wa chama hicho Bwana Salim Bimani amesema bado serikali ya Muungano haijatoa fursa zinazostahiki kwa Zanzibar katika masuala ya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuinyima nafasi za kibalozi nchi za nje.
 

Dr Shein asifu invyofua walimu

DHAMIRA ya kuwa na walimu waliofuzu katika kiwango cha Shahada katika shule za sekondari
hapa Zanzibar itafikiwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali kwa sasa.

Hayo yalisema na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika Mahafali ya saba ya chuo hicho yaliyofanyika Kampasi ya Vuga.

Chuo hicho kilianzishwa miaka 10 iliyopita kwa lengo la kuinua taaluma ya ualimu.

Katika mahafali hayo ambapo pia, aliwatunukia Shahada za Heshima za Uzamivu za Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dk. Salmin Amour Juma na Dk. Amani Abeid Karume kutokana na juhudi zao katika uanzishwaji wa chuo hicho pamoja na juhudi zao katika kuiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa Zanzibar.

Dk.Shein katika hotuba yake wakati akiwapa wahitimu 139 Shahada zao za Sanaa na Elimu
na 63 Shahada ya Sayansi na Elimu, alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wake katika
kuhakikisha chuo hicho kinatoa fani nyinginezo kama vile utalii, kilimo na udaktari na kueleza furaha yake kwa chuo kuanza kutoa wataalamu wa Fani ya Teknohama (IT).

Katika maelezo yake, Dk. Shein pia alishauri kwamba Shule ya Kiswahili na Lugha za Kigeni katika chuo kikuu hicho ikuzwe ili iwe mashuhuri kwa lugha hiyo duniani kama ilivyo kwa chuo kikuu cha Oxford, Uingereza kilivyo mashuhuri kwa lugha ya Kiingereza.

Mapema Makamu Mkuu wa Chuo cha SUZA, Profesa Idrisa Ahmada Rai alieleza kuwa dhamira kuu ya chuo wakati kinaanzishwa ilikuwa ni kutayarisha walimu wenye sifa ili kukuza elimu ya msingi na sekondari Zanzibar, na baadaye kukitanua na kusomesha masomo mengine tofauti chuoni hapo.

Alisema kuwa ndani ya miaka 10 ya SUZA hilo limefanikiwa asilimia 100.

Chanzo: Habari leo

Thursday 22 December 2011

Viongozi wanachochea uvunjaji sheria Zanzibar - Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema uvunjaji wa sheria unachochewa na baadhi ya viongozi kuwabeba wawekezaji kujenga vitenga uchumi katika maeneo yasiyoruhusiwa kimazingira.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Novemba, mwaka jana.

Akitoa mfano Maalim Seif alisema Hoteli ya Zanzibar Ocean View, imejengwa katika eneo ambalo kwa mujibu wa wataalamu wa mazingira, haliruhusiwi kuanzishwa kwa ajili ya mradi huo.

Alisema anashangaa kwamba hata baada wataalamu kuzuia eneo hilo kwa mradi huo, hoteli hiyo ilijengwa baada ya wamiliki kubebwa na viongozi wazito serikalini.

Mfano mwingine wa uvunjaji wa sheria za mazingira alisema ni ujenzi wa hoteli ya kitalii ya Misali ambayo imejengwa kinyume na Sheria za Uhifadhi wa mazingira kisiwani Pemba.

Alisema hoteli hiyo imejengwa karibu na kituo cha kuhifadhi mafuta ya aina mbalimbali pia karibu na Kituo cha umeme cha Wesha ambacho hupokea nishati hiyo kutoka gridi ya taifa kupitia waya uliotandikwa chini ya bahari kuanzia mkoani Tanga.

Maalim Seif alisema hata wataalamu wa mazingira wanaposhauri miradi inayokiuka uhifadhi wa mazingira ivunjwe maamuzi yao yamekuwa hayazingatiwi kutokana na wawekezaji hao kulindwa na vigogo serikalini.

Alisema kitendo hicho ni cha hatari kwa sababu kina hatarisha usalama wa wananchi na mpango mzima wa uhifadhi wa mazingira pamoja na kwenda kinyume na misingi ya utawala wa sheria.

Alisema wapo wawekezaji ambao wamediriki kujenga ndani ya fukwe za bahari tofauti na maelekezo ya kisheria kwamba miradi kama hiyo ijengwe umbali wa mita 30 kutoka ufukwe wa bahari.

Alisema kitendo cha baadhi ya viongozi kuwaruhusu wawekezaji kuvunja sheria hatimaye kitakuwa na madhara katika suala la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema licha ya kuhatarisha uhifadhi wa mazingira, ujenzi vitenga uchumi fukweni pia umeibua migogoro mikubwa kati ya wavuvi wadogo wadogo na na wawekezaji walioanzisha miradi yao katika fukwe.

Aidham alisema wakati umefika kwa wananchi wa kuongeza uwajibikaji katika kulinda na kuhifadhi mazingira hasa kwa kujiepusha na vitendo vya ukataji miti ya mikoko, uchimbaji wa mchanga na matumizi mabaya ya fukwe za bahari.

Alisema katika kupambana na tatizo la uchafuzi wa mazingira ikiwemo kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki, serikali imeunda kamati maalum ya kuwasaka wanaoingiza mifuko hiyo kutoka nje ya nchi na wanauza kwa wananchi kwa rejareja.

Hata hivyo, alisema adhabu ya faini ya Sh. milioni 10 kwa mtu anayepatikana na kosa la kuwa na mfuko mmoja wa plastiki na Sh. milioni 10 kwa mtu anayetiwa hatiani kwa kuwa na shehena ya mifuko hiyo inahitaji kuangaliwa upya utekelezaji wake.

Alisema kwa msingi huo serikali imeamua kuiangalia upya sheria hiyo kabla ya kuanza kuwakamata wananchi wanaotumia mifuko hiyo na kuwafikisha mahakamani kutokana na kuwa tayari imepigwa marufuku matumizi yake

Chanzo: Nipashe

Kwa nini tunashindwa kuwapandisha wakubwa kizimbani?

Ahmed Rajab
UKWELI, ingawa ni adhimu, una tabia mbaya.  Una tabia ya kuudhi na hata ya kuuma. Ndiyo maana haishangazi tunapojikuta tunaukwepa.
Alhamisi iliyopita nilikuwa Bush House, jijini London, kwenye studio za BBC Focus on Africa, kusajili kipindi cha mwisho wa mwaka niliposikia kwamba mahakama moja nchini Ufaransa imemhukumu rais wa zamani wa nchi hiyo Jacques Chirac, baada ya kumpata na hatia ya ufisadi. Nilishtuka nilipojisikia nikijiambia: ‘Ndiyo maana wazungu wanatushinda.’
Halafu mbiombio nikajilaumu kwa dhana potovu kwamba kila cha mzungu ni chema.  Nilichelea yasije mawazo yangu yakateleza mithili ya yale ya mshairi maarufu wa lugha ya Kifaransa, Léopold Sédar Senghor. 
Senghor aliyezaliwa Senegal na aliyekuwa mmoja wa wahubiri wakuu wa falsafa ya négritude (uweusi) aliwahi safari moja kuhoji kwamba wazungu ndio wenye kutumia akili na watu weusi tumejaa jazba tu. Hatuna letu ila mihemko, mahamasa na hisia nzitonzito.  Kinyume na wazungu, alisema, sisi hatuyapimi mambo na kuyachanganua.
Wengi walimlaumu Senghor kwa dhana hiyo.  Pamoja na kuwa mshairi na msomi mkubwa, Senghor alikuwa mwanasiasa mahiri.  Alikuwa rais wa mwanzo wa Senegal kwa muda wa miaka 21 na anaheshimika kwa kuwa wa kwanza barani Afrika kuuacha urais kwa hiyari yake alipomkabidhi wadhifa huo waziri mkuu Abdou Diouf tarehe mosi Januari mwaka 1981.
Senghor alikosea pakubwa alipohoji kwamba ni wazungu peke yao wenye uwezo wa kuchambua mambo kwa kutumia akili.  Hata hivyo, sidhani kama ninakosea nisemapo kwamba wazungu wametushinda na wangali wanatushinda kwa mengi. 
Bila ya shaka si yao yote yaliyo mema au yanayopaswa kupigiwa mfano.  Lakini ukweli, na ukweli unauma, ni kwamba, kwa jumla, wanatushinda.
Wanatushinda, kwa mfano, katika kuziheshimu sheria. Ushahidi ni kama huo uamuzi wa mahakama iliyokuwa ikiyasikiliza mashtaka dhidi ya Chirac. 
Juu ya kuwa baadhi ya wakuu Wakifaransa walijaribu kuzuia Chirac asishtakiwe, hakimu alikataa.  Hatimaye haki ilitendeka, ilionekana ikitendeka na Chirac akapata alichostahiki: hukumu ya kifungo cha nje cha miaka miwili.
Hukumu hiyo imethibitisha jinsi demokrasia nchini humo ilivyopevuka.  Kuna mengi yasiyo sawa katika demokrasia hiyo lakini kwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya Chirac, Ufaransa ina haki ya kujigamba kwamba imeonyesha mfano mwema.
Kwa wasiomjua, Chirac ni kipenzi cha wengi na mkakamavu katika siasa za Ufaransa. Ni mwanasiasa aliyekuwa na ustadi wa kuyapangua makundi ya mahasimu zake ndani ya kambi yake na hata kuyagonganisha vichwa. Wengi wakimuona kuwa ni kiongozi wa siasa za ‘shujaa wa Ufaransa’, rais wa zamani Jenerali Charles de Gaulle.
De Gaulle alijiuzulu tarehe 28 Aprili 1969 baada ya kushindwa kwenye kura ya maoni. Alikwishakusema kwamba atajiuzulu endapo atashindwa kwenye kura hiyo iliyohusu mageuzi aliyotaka kuyafanya katika baraza la senate la bunge na katika mfumo wa serikali za kienyeji. 
De Gaulle alifariki ghafla mwaka 1970.  Alipofariki rais aliyemrithi Georges Pompidou alitangaza kuwa ‘Jenerali de Gaulle amefariki. Ufaransa ni kizuka’. Kwa kusema hivyo Pompidou alimaanisha kwamba de Gaulle alikuwa bwana wa Ufaransa.
Wakati huo Chirac alikuwa waziri na akijulikana kwa lakabu ya ‘buldoza’.  Baadaye akachaguliwa Meya wa Paris, wadhifa alioushika kwa muda wa miaka 18. Aliwahi pia kuwa waziri mkuu mara mbili. Mwishowe akawa Rais kuanzia 1995 hadi 2007.
Kumbe katika muda wote huo ‘buldoza’ Chirac alikuwa akijipakaza tope za ufisadi. Miongoni mwa shutuma zilizomuandama ni ile kashfa iliyomhusisha na ulipaji mishahara ya watumishi wa kubuni, yaani ‘wafanya kazi hewa’, wakati alipokuwa meya wa Paris na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa maslahi yake binafsi. 
Wengine wakaongeza mengine wakisema, kwa mfano, kwamba familia ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon marehemu Rafiq Hariri ilisaidia kulipia jumba la kifahari la Chirac linaloukabili mnara wa Eiffel, jijini Paris.
Shtuma nyingine ni kuwa marais kadhaa wa Kiafrika walimpa yeye na waziri wake mkuu Dominique de Villepin dola milioni 20 za Marekani ziwasaidie kwenye kampeni za uchaguzi.
Kwenye kampeni ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2002 inasemekana Chirac alipokea dola za Marekani milioni sita na laki mbili kutoka kwa marais wafuatao: Blaise Compaoré wa Burkina Faso; Abdoulaye Wade wa Senegal; Laurent Gbagbo wa Côte d’Ivoire; Denis Sassou Nguesso wa Congo and marehemu Omar Bongo wa Gabon pamoja na Obiang N’guema wa Equatorial Guinea.
Ingawa sheria ilimstahi alipokuwa rais baada ya kuacha madaraka ilimuonyesha kwamba hakuna anayeweza kuikwepa.
Yaliyomfika Chirac ndio yaliyonifanya nitafakari na kujiuliza kwa nini ikawa wazungu wanatushinda. Kwa nini hakuna kampeni Afrika ya kutaka hao marais waliotajwa washughulikiwe kisheria kwa kutumia fedha za umma kumhonga Chirac? 
Bila ya shaka wazungu hawakutushinda katika kila kitu, lakini hatuwezi kukataa kwamba wametupiku kwa kuwafanya viongozi wao wawajibike.
Sisemi kama wamekamilika.  Wapo wakorofi miongoni mwao wanaozipinda sheria lakini kwa jumla mwelekeo wao ni wa kuheshimu katiba na sheria zao.
Inasikitisha kuona kwamba nchini Tanzania mtindo wa wakubwa kung’ang’ania madaraka umekuwa sehemu ya utamaduni wa kiutawala. Ni nadra kwa wakubwa kuwajibika na hakuna anayethubutu kuwashurutisha wafanye hivyo.
Sana sana pakizuka kadhia ya ufisadi bunge ndilo huijadili kadhia hiyo.  Mara nyingi huo huwa ndio mwisho wake. Huonekana jambo kubwa pale wakubwa wanapojiuzulu kama walivyofanya mawaziri watatu pamoja na aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa.
Ikiwa wakubwa wanafikishwa mahakamani kama walivyofikishwa mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona basi kesi hupigwa danadana. Huendeshwa kivarangevarange wakati umma umekaa macho ukitaka kujuwa iwapo washtakiwa kweli wana hatia au wanasingiziwa.
Inavyodaiwa ni kwamba Yona, akiwa waziri wa fedha, pamoja na Ben Mkapa, akiwa rais wa awamu ya tatu, walijinunulia mgodi wa makaa wa Kiwira bila ya kufuata taratibu. Kwa hilo, Mkapa naye aliikiuka katiba ya nchi kwa kuigeuza Ikulu kuwa pahali pa kufanyia biashara.
Msomaji mmoja wa Raia Mwema alinikumbusha hivi karibuni kuwa Mkapa naye anastahiki apelekwe kwenye Korti ya Kimataifa ya Jinai huko Hague kwa mauaji yaliyotokea Visiwani Januari 2001. Raia waliuawa kwa sababu waliandamana na mauaji hayo yaliwapeleka mamia ya wananchi wengine waikimbie nchi yao. Isitoshe Mkapa aliwasifu askari waliohusika na kuwapandisha vyeo.
Tabu yetu Afrika ni kwamba tumezoea kuiga lakini tunapoiga hatuigi sawasawa.  Tunasema tunafuata mfumo wa utawala wa kibunge wa Westminster lakini tunaufuata mfumo huo kijuujuu tu.  Hatuviheshimu vyombo vya kisheria wala hatuvipi uhuru na mamlaka kamili. Badala yake tunaligeuza suala zima la demokrasia na utawala bora liwe mazingaombwe.
Ukweli ni kwamba sheria katika nchi nyingi za Kiafrika zinawalinda viongozi na wapambe wao. Wanapofikishwa mahakamani kesi zao huwa ni za kiini macho.
Nchini Zambia, kwa mfano, serikali ya Rais Levy Mwanawasa ilimfungulia mashtaka rais aliyemtangulia Frederick Chiluba kwa makosa 100 ya ufisadi na kuhaulisha fedha za umma na kuziingiza kwenye akaunti zake binafsi katika mabenki ya London.
Kesi ya Chiluba ilisotasota kwa miaka sita hadi baada ya kufariki Mwanawasa mwaka 2008 na urais kushikwa na Rupiah Banda, aliyekuwa rafiki wa Chiluba. Mwaka 2009 mahakama ya Zambia ikasema Chiluba hana hatia.
Wakati kesi ilipokuwa inaendelea nchini Zambia mahakama moja ya London ilimpata Chiluba na hatia ya kuchota takriban dola milioni 58 za Marekani na mahakama ikamtaka azirudishe fedha hizo.  Mahakama ya Lusaka ikamlinda.  Ilikataa kumpeleka Uingereza ikihoji kwamba ya Uingereza ni ya Uingereza na ya Zambia ni ya Zambia.
Huo ni mfano mmoja wa namna viongozi Wakiafrika wanavyolindana. Sikusudii kuwa kila kiongozi anayeshtumiwa kwa ufisadi au kwa makosa mengine lazima apatikane na hatia. La hasha.  Ninachokusudia ni kwamba lazima mahakama iachiwe ifuate mchakato wake.
Tukumbuke tu kwamba yaliyomfika Chirac hayana mmoja, yanaweza kuwafika viongozi Wakiafrika na wala wakati haugandi bali unakwenda na kubadilika. Viongozi wetu watakuwa wanajidanganya wakidhania kwamba yaliyomfika Chirac ama Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia ama Hosni Mubarak wa Misri hayatoweza kuwatokea.
Upepo wa mabadiliko wa miaka ya 1990 haukuzikumba nchi za Kikoministi za Ulaya ya Mashariki tu bali ulivuma barani Afrika pia.  Huko ulisaidia kuleta mabadiliko ya kuachana na mfumo wa chama kimoja cha kisiasa.  Waliokuwa na dukuduku hawakuwa na hila ila nao waliridhia ingawa kwa shingo upande.
Mwanzoni mwa mwaka huu pakavuma dhoruba ya mageuzi Afrika ya Kaskazini.  Matokeo yake tumeyaona.  Na hii hatua ya kuhakikisha kwamba hakuna anayeweza kuuhepa mkono wa kisheria ni upepo utaogeuka kimbuga barani Afrika wakati utapofika.  Mwenye macho haambiwi tazama.

Chanzo: Raia mwema

Tuesday 20 December 2011

Maalim aitaka COSTECH kufanya tafiti Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalimu Seif Shariff Hamad ameielekeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuisaidia Zanzibar kufanya utafiti ili iweze kuzitumia tafiti hizo kuboresha maisha ya wananchi.
Maalim Hamad alitoa maelekezo hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa tume hiyo kufuatia ziara aliyoifanya kwenye ofisi za jengo hilo, ambapo aliielekeza ifanye utafiti katika maeneo manne visiwani humo.
Eneo la kwanza ambalo ninawaomba muliiangazie ni la mazingira.Kama munavyojua Zanzibar ni visiwa na mabadaliko ya tabia nchi yanaviathiri sana visiwa vyetu na kwa hiyo utafiti wenu utatusaidia tujue hatua za kuchukua,” alisema.
Maeneo mengine ambayo aliiomba COSTECH isaidie ni katika upande wa masuala ya ukimwi, ulemavu na mihadarati ambapo alisema tafiti hizo zitasaidia kuelewa matatizo halisi yalivyo na njia za kutumia ili kuyaondoa.
Aidha, aliiasa COSTECH kuzitangaza huduma zake kwa wananchi ili waweze kuzielewa na hatimaye kuzitumia katika maendeleo yao kwa kuwa wananchi walio wengi nchini bado hawajui kuhusiana na huduma zinazotolewa na tume hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Hassan Mshinda, alisema tume imeweza kugharamia mafunzo kwa wataalamu wapatao 295 katika ngazi za shahada za uzamili na uzamivu baada ya serikali kuongeza kiwango cha fedha za utafiti kwa tume hiyo toka Sh. bilioni moja hadi bilioni 16 kwa mwaka huu.
Alisema wataalamu hao wamepelekwa kwenye vyuo vikuu vitano vya umma nchini vya Dar es Salaam, Sokoine, Muhimbili, Ardhi na Nelson Mandela kilichoko Arusha ambapo katika ngazi ya uzamili, tume imewagharamia wataalamu 195 na katika ngazi ya uzamivu inawalipia wataalamu 100
Chanzo: nipashe

Sunday 18 December 2011

Maalim Seif anogewa serikali ya mseto

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema anaridhishwa na mafanikio ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Amesema kutokana na hali hiyo, hafikirii kwamba Zanzibar inapaswa kurejea katika mfumo tenganishi ambao ulisababisha mgawanyiko mkubwa visiwani.

Maalim Seif aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kuzungumzia mafanikio na changamoto za mwaka mmoja wa Serikali hiyo inayoundwa na vyama vya CCM na CUF.

“Naam, ninaridhika sana na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali hii, sio mafanikio madogo, ni ya kuridhisha,” alisema Seif na kuongeza kuwa kila jambo lina changamoto zake.

Alisema kutokana na hilo, changamoto zilizopo hazina budi kurekebishwa ili kuiwezesha Serikali hiyo iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, kupata mafanikio makubwa zaidi.

Alisema ukilinganisha na Serikali kama hizo zilizopo Zimbabwe na Kenya, ya Zanzibar imeonesha kwenda vizuri licha ya kuwepo kwa upungufu kadhaa.

Alisema katika kuendesha Serikali hiyo wanatumia sera za chama anachotoka Rais, lakini kwa busara za Rais Dk. Ali Mohammed Shein, Serikali hiyo inatekeleza sera zote zenye manufaa wa ustawi wa Zanzibar hata kama zinatoka kwa chama kingine.

Alisema licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza katika mwaka mmoja wa Serikali hiyo, yapo mafanikio katika uboreshaji wa kilimo katika mazao ya chakula na biashara, kuimarisha sekta ya uvuvi, kuboresha hali za maisha za wafanyakazi na kukuza teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Katika kilimo, alisema zao la karafuu limepanda ambapo mwaka huu, kilo moja inanunuliwa kwa Sh 15,000, na inatarajiwa kuwa ifikapo Mei mwakani, kwa kisiwa cha Pemba pekee, wakulima watapata Sh bilioni 50 kutokana na mauzo ya karafuu.

Katika uvuvi, Maalim Seif alisema Serikali imechukua hatua kuifanya rasilimali ya bahari kuwanufaisha wananchi, na hivi sasa wawekezaji wengi wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo.

“Katika kuendeleza sekta ya uvuvi, tayari Serikali imewapeleka wananchi 30 huko China kujifunza mbinu za kufuga samaki,” alieleza Maalim Seif.

Maalim Seif alisema mbali ya mafanikio hayo, zipo changamoto kadhaa zikiwemo za baadhi ya watendaji wa Serikali kutofahamu malengo ya kuanzishwa kwa mfumo wa Serikali shirikishi, badala yake kuendelea na mfumo tenganishi.

“Badala yake wanaendesha shughuli za umma kwa taratibu zile zile ambazo hazisaidii sana kuimarisha umoja wetu,” alieleza Seif na kuongeza kuwa baadhi ya watendaji hao wanafanya kazi kwa mazoea.

Alisema pia yapo malalamiko mengi kuhusu suala la ardhi, ambayo hata hivyo, alibainisha kuwa Serikali inayafanyia kazi na tayari inapitia upya sera ya ardhi na sheria zote zinazohusu masuala ya ardhi.

“Kuna malalamiko makubwa ya kuwa wanafunzi wengi hawajafaidika na mikopo ya kuwawezesha kupata elimu ya juu. Hili linatokana na uwezo mdogo wa Serikali,” alisema na kuongeza: “Wanafunzi wanaohitaji mikopo ni zaidi ya 1,500.

Uwezo uliopo kwa mwaka huu wa fedha ni kuwapatia huduma hii muhimu wanafunzi 191 tu. Serikali itakuwa ikiongeza fungu la mikopo hii kila mwaka ili wanafunzi wanaofaidika waweze kuongezeka kila mwaka.”

Aidha, alisema baadhi ya wananchi wanalalamikia kuwa wananyimwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, na kuona kuwa hiyo ni haki ya kila mtu na Rais Shein alishatoa maelezo kwamba kila mtu apatiwe, hivyo ofisa asiyetekeleza hivyo, anafanya utovu wa nidhamu.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliwataka Wazanzibari kushirikiana kwa pamoja kuinua ustawi wa nchi yao.
Chanzo: Habari leo

Zanzibar sasa wataka zamu urais Tanzania

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inataka kuwepo kwa muundo ambao utagawa zamu ya nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika katiba.

Maalim alisema Zanzibar haifurahishwi na mfumo wa sasa ambapo Rais anatoka sehemu moja tu ya muungano ambayo ni Tanzania Bara.

“Kipaumbele chetu katika marekebisho ya katiba tunataka kuwepo kwa muundo utakaoonesha na kutamka wazi wazi muda wa zamu ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Zanzibar ni sehemu inayounda muungano huo,” alisema.

Seif alisema hayo katika mahojiano na waandishi wa habari hapo katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani ambapo alizungumzia mafanikio ya serikali ya umoja wa kitaifa tangu kuundwa mwaka jana.

Alisema kuwepo kwa utaratibu unaotambuliwa kisheria kwa kiasi kikubwa utasaidia kujua kipindi hichi rais anatoka kutoka katika upande upi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maalim alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa haifurahishwi na utaratibu uliopo sasa ambapo rais wa Jamhuri ya Muungano anatoka Tanzania Bara tu na Zanzibar kubaki na nafasi ya Makamu wa Rais.

Kwa mara ya mwisho, Zanzibar ilitoa Rais wa serikali ya Muungano, Mzee Ali Hassan Mwinyi mwaka 1985 aliyekaa madarakani hadi mwaka 1995 alipompisha Benjamin Mkapa.

Hata hivyo, Maalim aliwataka wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi wakati muda utakapofika wa kutoa maoni ya marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa ujumla alisema Zanzibar imejizatiti katika marekebisho hayo kuona kwamba maslahi ya Zanzibar katika mchakato huo yanazingatiwa kwa umakini mkubwa.

Alitoa mfano wa visiwa vya Comoro ambapo katika katiba yake vimeweka bayana kwamba mwaka huu raia anatoka kisiwa kimoja na katika uchaguzi unaofuata, raia anatoka kisiwa kingine.

“Utaratibu kama huo ndiyo unaokubalika ambao unataja wazi wazi mwaka huu rais anatoka wapi hatua ambayo ni nzuri kwani inasaidia kuondosha malalamiko ya muungano,” alisema Maalim.
Chanzo: Habari leo

Monday 12 December 2011

SPEECH BY THE PRESIDENT OF ZANZIBAR, DR. ALI MOHAMED SHEIN, AT THE OPENING OF “THE FIRST INTERNATIONAL SYMPOSIUM ON IMPACTS, VULNERABILITY, AND ADAPTATION TO CLIMATE CHANGE IN SMALL ISLAND DEVELOPING STATES” AT ZANZIBAR

First and foremost, I would like to take this opportunity to thank the Almighty God for availing us good health to be able to attend this important symposium. I understand that some of you have travelled from different countries and therefore let me take this opportunity on the behalf of the people of Zanzibar and Tanzania in general to welcome you all to this spice and historical Island. Please feel at home. “Karibuni sana.” My deep appreciation goes to the organizers for their enthusiasm and giving me this privilege to officiate at the opening of the first symposium of its kind.

I am told that the purpose of this three-day symposium is to present, discuss, share experiences and mutually resolve on evolving approaches, tools, methods and philosophies pertaining to impacts and vulnerabilities caused by climate change with specific focus on small island communities. As such, we in Zanzibar feel privileged to host this symposium. Many, if not all the matters under discussion touch us directly and our survival depends on them. The fact that you will discuss the impacts, vulnerability and adaptation to climate change, gives us much hope and raise our spirit for survival.

Distinguished Participants,
Ever since the declaration of the United Nations Conference on the Human Environment in Stockholm in 1972 that defined the common principles to the people of the world in the preservation and enhancement of human environment, the challenges concerning environment and development have become an almost insurmountable obstacle. Millions of people around the world continue to live far below human levels required for their decent existence. Population growth, food insecurity, challenges over shelter and education, health and sanitation and industrial pollution have continued to affect the pace of development in many countries.

Based on the challenges that we have been facing, it is very clear that the road to our common future cannot be realized without having common understanding and agreements in reaching agreed fundamental goals of environment protection, peace, economic and social equity, for the worldwide development.

Distinguished Participants,
The Rio Conference of 1992 established the implementation of the principles of sustainable development under Agenda 21. Central to this concept of development was the environmental and social justice with respect to the use of resources which included fair access to all without compromising the options of future generations. The interdependent and mutually reinforcing pillars of sustainable development are economic development, social development and environmental protection.

Today, when we look into the scope of sustainable development, we have to ask ourselves how far we have succeeded in optimizing these three pillars of economy, society and environment. The current state of environment concerning our atmosphere, water, natural resources and biodiversity is not so promising; the application of science and technology for productive economic outputs continues to be an expensive tool beyond the reach of poor nations; and the fundamental rights to education, adequate standard of living, food security, health, labour and shelter – all these pose a fundamental question on how far or close we are from achieving the desired goal of sustainable development.
Distinguished Participants,
The world has just completed another round of talks in Durban concerning whether or not to continue with the Kyoto Protocol of the United Nations Framework Convention on Climate Change. For some, the Protocol may just be another round of endless negotiations in the Multilateral Environment Agreements, but for many people around the world, and especially those who live in the small island developing states, this race is about our own human survival.

No countries are more susceptible to the effects and impacts of climate change than small island states. In many cases, these islands share unique biophysical characteristics, the urgency of these small nations coming together under one strong voice has never been more clearer. Small Island Communities are very vulnerable to climate change and have limited capacity to respond to the impacts caused by environment disasters. The problems we face such as rising sea level, failing monsoons, food insecurity, recurring droughts, depleted fisheries and the increased coastal erosion have been unbearable.

As a matter of fact, since 2003 East Africa has had the eight warmed years on record which in no doubt have contributed to the famine that now afflicts 13 million people in the Horn of Africa. The UN Environment Programme’s just published report, “Bridging the Emission Gap” shows that over the course of this century, warming will likely rise to four degrees.

Distinguished Participants,
It is not yet certain what exact impacts will these factors contribute to the economy and livelihoods of our people, but at least what we know for sure is that the coastal dynamics of our shorelines have already begun to be affected. With land becoming a scarce commodity under the forces of beach erosion, and the recorded cases of salt water intrusion in all the districts of the islands of Unguja and Pemba becoming conspicuous, the hazards of coastal flooding have already been rated very high in six out of ten districts of the islands of Zanzibar. Nowhere is that risk extremely high than on the western coastal fringes of the main island of Zanzibar where population density in some areas reach more than 2000 people per square kilometer. The risk is extremely high in some coastal fringes of the main island of Zanzibar. In addition, we have seen graves been inundated by salt water and arable land being made hopelessly useless.

Our limited capacity to measure accurately the projected impacts on our ecosystems and economy warrants an immediate and urgent plea for technical support in developing a reliable system of climate change models specific to the small island states with high resolution and level of accuracy. This could improve our early environmental and climate change warning system and be able to save lives and avoid environmental disasters and collapse of our small economies which are dependant on the oceans and forests.

It is high time for Governments and international organizations to do whatever they can to mitigate the impacts of climate change. In our case, my Government has already established Steering and Technical Climate Change Committees and the process of developing the Zanzibar Climate Change Strategy has begun. Moreover, the Revolutionary Government of Zanzibar with the support of development partners such as the Government of Finland (through Sustainable Management of Lands and Environment project) has already prepared a road map towards its national adaptation goal.

To strengthen our commitment towards implementation of the climate change adaptation programs in Zanzibar, my Government is also working on the African Adaptation Program (AAP) for provision of clean water supply to the communities of the northern locality of Nungwi whose water sources have been affected by salt water intrusion. These initiatives are being carried out under UNDP Project which is supported by the Government of Japan.

Distinguished Participants,
It is true that international efforts are under way to allocate enough resources to deal with adaptation and mitigation interventions, but this is not always enough. Debates are ongoing about the mechanism of the climate funding and how to allocate funds meant for Reduced Emissions for Deforestation and Degradation projects in poor countries. The Kyoto Protocol was supposed to help small countries under the Clean Development Mechanism (CDM) projects, but statistics show that only a handful of countries are expected to generate 80% of the total CDM credits by 2012, leaving the vast majority of small states in greater environment and climate change uncertainty.

The United Nations Framework Convention on Climate Change has tried to come up with alternative programmes under the National Adaptation Programme of Action (NAPA) and more recently, the piloting of Reduced Emissions from Deforestation and Degradation (REDD), but it is far from certain as to whether these interventions could by themselves be the viable solutions to our rapidly changing climate.

The community of nations must accept the fact that climate change is a global problem. It needs universal support to confront it. Let me quote Nobel-Laureate, Archbishop Desmond Tutu and Mrs. Mary Robinson, a former President of Ireland and currently President of the Mary Robinson Foundation, who jointly declared in a statement to the Durban conference supporting the assertion I have just made. They said, If countries are not confident that others are addressing it (the problem) they will not feel an imperative to act themselves.”

They added: “Climate change is a matter of justice. The richest countries caused the problem but it is the world’s poorest who are already suffering from its effects.”

Distinguished Participants,
At this juncture, let me again join the calls that propose for the setting up of the new global mechanism within the United Nations that will provide the necessary support to environment, climate change and sustainable development issues for small island states around the world. This new mechanism will facilitate in mainstreaming sustainable development issues for green economy in development planning, allocation of financial resources specific to small island states – and dedicated towards the climate funding.

The proposed mechanism will support the provision of appropriate technologies which are affordable and cost effective specific for addressing climate change impacts for small island communities; facilitate exchange and sharing of experiences and which will also assist in capacity building and capabilities of all small island developing states. We need to develop practicable means of dealing with the changes. We need to restore forests, encourage communities to change their mode of earning a living away from charcoal burning; collecting and use of rain water and developing better breed of seeds that can withstand the climate change, especially drought.

Distinguished Guests,
I believe that the upcoming Rio +20 conference that will take place next year will be a golden opportunity for the small island states and should be the delivery point for the new framework on integrated approach to address the problems facing our communities pertaining to environment, climate change and sustainable development. This will help to address the development needs of small island states while promoting a transition to green, low emission and climate resilient development and growth.

Failure to act now would give the small island communities less time to adapt to the impacts of climate change and the consequences would be more costly especially if mitigation efforts and adaptation measures are postponed through lack of finance, technology or human skills. We must act now for our common future. It is said that if climate change is expensive, failure to act universally against is even costlier. Our efforts towards poverty reduction will be curtailed and held back.

I pledge that my Government will continue to work together with all friends and partners at the national, regional and international level to ensure the long-term goal of sustainable development as we are heading for the age of the Green Economy.

Let me conclude by wishing you a very fruitful and successful programme and I believe that you will also spare some time in your busy schedules to enjoy the exotic sites and sandy beaches of our islands, taste its delicious cuisines, smell the fragrance of its spices, appreciate the cultural diversity of its people and become our cultural ambassadors overseas. KARIBUNI ZANZIBAR and feel at home among brothers and sisters.

I am now pleased and honoured to declare the “First International Symposium on Impacts, Vulnerability and Adaptation to Climate Change in Small Island Developing States; implications to poverty reduction” is officially opened.
Thank you and wish you good luck

Sunday 11 December 2011

Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Z`bar yapora mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania

Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini, January Msoffe amesema marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar yemepora Mamlaka ya kikatiba ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ya kusikiliza kesi za haki za binadamu nchini.

Tamko hilo alilitoa jana alipokuwa akifungua maadhimisho ya siku ya haki za binadamu Duniani katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).

Alisema kwa mujibu wa marekebisho hayo ya katiba wananchi wa Zanzibar sasa hawana haki tena ya kikatiba ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania dhidi ya kesi za uvunjwaji wa haki za binadamu zitakazokuwa zikifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Msoffe, alisema katika mabadiliko hayo kuna tatizo kutokana na kifungu cha 24(3) cha katiba ya Zanzibar kufuta mamlaka ya kikatiba ya Mahakama ya rufaa Tanzania kupokea na kusikiliza rufaa za kesi za haki za binadamu zilizofunguliwa Zanzibar na kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

“Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imenyang’anywa uwezo wa kusikiliza kesi za haki za binadamu kutoka Mahakama kuu ya Zanzibar,” Alisema Jaji Msoffe.

Alisema kwamba kifungu hicho kinahitaji kuangaliwa upya kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa sababu kina wanyima haki ya kikatiba wananchi ya kutumia Mahakama ya rufaa Tanzania iwapo watakuwa hawakuridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Msoffe, alisema kwamba katiba ya Zanzibar na marekebisho yake yamebadilisha yaliyomo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977 ambayo ilikuwa ikitoa fursa kwa kila mwananchi wa Zanzibar kufuatilia haki zake Mahakama ya rufaa kama ikitokea hakuridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Alisema kwamba marekebisho hayo ya katiba yamempa uwezo Jaji Mkuu wa Zanzibar kuteua majaji watatu wa kusikiliza rufaa na uamuzi wao utakuwa wa mwisho kama mlalamikaji hatakuwa hakuridhika na uamuzi wa awali wa Mahakama hiyo.

Kuhusu katiba mpya ya Tanzania, Jaji Msoffe alisema mambo ya haki za binadamu lazima yaangaliwe upya katika katiba ya Muungano na ya Zanzibar ili yaendane na wakati katika mabadiliko hayo.

Alisema kwamba mabadiliko hayo ya katiba juu ya haki za binadamu vizuri kuangalia mifano ya Katiba za Kenya, Afrika Kusini na Uganda kwa vile katiba za mataifa hayo zimezingatia kwa kiwango kikubwa juu ya masuala ya haki za binadamu na utawala bora.

Jaji Msoffe alisema mabadiliko ya katiba ya Tanzania lazima yazingatie haki za binadamu za kiraia, kisiasa haki za kiuchumi na kiutamaduni katika pande zote mbili za muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema kwamba wakati umefika kwa wananchi na viongozi kufundishwa juu ya haki za binadamu kwa sababu wapo ambao hawafahamu juu ya haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Siyo viongozi wengi wanaofahamu haki za binadamu. Huu ni mtihani mkubwa kwa sababu wanatakiwa watende haki na haki zenyewe hawazijui,”alisema Jaji Msoffe huku akipingwa makofi na washiriki wa Kongamano hilo.

Alisema kutokana na tatizo hilo wananchi wengi Tanzania wamejigeuza wao kuwa Polisi na Mahakama kwa kuwakamata watu na kuwaadhibu na wakati mwingine kukatisha maisha yao jambo ambalo ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria. Alisema kwamba tatizo la wananchi kuchukua sheria mkononi lilianzia huko Tanzania bara na sasa limeingia kwa kishindo Zanzibar.

Alisema kwamba katika kuadhimisha miaka 63 ya tamko la umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu duniani ni vizuri kwa serikali kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wake ili wafahamu haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao na kujiepusha kuchukua sheria mkononi.

Kongamano hilo limetayarishwa na Kituo cha huduma za sheria (ZLSC) chini ya Mwenyekiti wake Profesa Chris Maina Peter, ambapo Mwanasheria mwanadamizi kutoka Ofisi ya Mwendesha mashitaka Safia Masoud Khamis, aliwasilisha katika kongamano hilo mada juu ya serikali katika kuheshimu haki za Binadamu Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

Thursday 8 December 2011

Dk. Salim: Chonde, chonde na Katiba

8th December 2011
Zanzibar wana madukuduku yao, Tanzania Bara wana madukuduku yao juu ya muungano ni muhimu wakubaliane kikatiba,” alisema Dk. Salim katika mahojiano na NIPASHE yaliyofanyika Kiwengwa, mjini Zanzibar juzi.
Alisema jambo la msingi kwa sasa ni wananchi kupewa nafasi ya kutafuta ufumbuzi wa dukuduku hizo kwa njia ya mjadala utakaoendeshwa kupitia mchakato wa kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba mpya.
Alisema itakuwa ni vizuri kwa vyama vya siasa kujiweka kando ili kuachia wananchi nafasi kubwa zaidi kwa sababu katiba kimsingi inatakiwa iandikwe kwa kuzingatia maoni yao na matakwa yao.
Dk. Salim alisema sehemu kubwa ya kizazi kilichopo kinaundwa na kizazi kipya hivyo ni vizuri wakapewa nafasi ya kushiriki na kuamua aina ya katiba ambayo wanaamini itakidhi matarajio yao.
Akizungumzia mambo ambayo anaamini ni hatari kwa taifa, Dk. Salim alisema ni pamoja kuingiza udini na ukabila katika masuala ya siasa.
Alionya kwamba wakati Tanzania inaendelea na mchakato wa kuandika katiba mpya, haitakuwa jambo zuri kwa taasisi za nje kuingilia shughuli za upatikaji wa katiba mpya.
Watanzania sio roboti, kila mmoja ana akili na fikira zake, muhimu kulinda umoja wetu, na wananchi hasa wa vijijini kupewa nafasi zaidi ya kutoa maoni juu ya katiba yao,” alisema Dk. Salim.
Hata hivyo, Dk. Salim alisema hashagazwi na kitendo cha kuingilia mambo ya ndani ya mchakato wa katiba kwa sababu Tanzania ni sehemu ya ulimwengu na haiwezi kujitenga kuwa peke yake.
Kuhusu miaka 50 ya uhuru, alisema Tanzania imefanikiwa kuwa na katiba yenye misingi mizuri ya viongozi kubadilishana madaraka na hivyo kudumisha amani.
Dk. Salim alishauri kuwa itakuwa ni kosa kubwa kwa Watanzania kujaribu kuwa na katiba inayoondoa ukomo wa viongozi kukaa madarakani, kwani jambo hilo linaweza kuipeleka Tanzania kwenye migogoro ya kisiasa.
Aidha, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa kwa wananchi wake ikiwemo kujenga misingi ya umoja wa kitaifa tangu mwaka 1964.
Alisema kwamba jambo la msingi hivi sasa ni wananchi kupewa nafasi ya kujadili kero za muungano na kutoa maoni yatakayosaidia kuimarisha muungano huo.
Kuhusu sera ya mambo ya nje ya Tanzania, Dk. Salim alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uhusiano wake kimataifa.
Hata hivyo alisema sifa hiyo haikuja yenyewe bali ilitokana na mabalozi waliokuwa wakiteuliwa kufanyakazi kwa kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi binafsi.
Alisema Watanzania wanaopewa nafasi za ubalozi ni vizuri wakafanyakazi kwa kuzingatia uadilifu na kujituma ili kujenga heshima kwa taifa lao.
Huwezi kujifundisha diplomasia kwa kukaa nyumbani na kupiga soga vijiweni, pia uaminifu kwa nchi, jambo la msingi ukiwa nje ya nchi ukipata kashfa hiyo ni kashfa ya nchi yako.” alisema Dk. Salim ambaye ni mwanadiplomasia mkongwe nchini.
Alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru mataifa mengi barani Afrika na Ulaya yanatambua mafanikio ya Tanzania katika kupingania ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na misingi ya haki za binadamu na ubaguzi wa rangi.
Hata hivyo, alisema kwamba vyama vya siasa bado vina mchango mkubwa katika kulinda na kutetea misingi ya umoja wa kitaifa katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
CHANZO: NIPASHE

Tuesday 6 December 2011

HOTUBA YA JUMUIYA YA WAFANYA BIASHARA, WENYE VIWANDA NA WAKULIMA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI.

TAREHE 06/12/2011

Mheshimiwa, Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Afisi Ya Rais Fedha Uchumi, na Mipango Ya Maendeleo.
Naibu Kamishna TRA,
Waheshimiwa, Wafanyabiashara wa Zanzibar,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.

Assalaamu Alaykum.


1)Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwingi wa Rehema kwa viumbe vyake vyote, kwa kutujaliia kuwa na afya njema katika siku hii adhimu ya Mlipa Kodi katika mwaka huu wa 2011.

2)Napenda vile vile kueleza shukurani zetu za dhati kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) Zanzibar kwa kutupatia nafasi ya kueleza mawazo ya wafanyabiashara katika hafla hii. Tutajaribu kueleza yale ambayo tunaamini yanaweza kuletea ufanisi katika kutekeleza jukumu kubwa walilopewa wenzetu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Zanzibar. Jukumu hilo ni lile la kukusanya kodi kwa lengo la kukuza uchumi wa Zanzibar na kuendeleza huduma za kijamii kwa wananchi wake. Kwa ujumla maudhui yangu ni kuwa kodi inayokusanywa Zanzibar ni kwa maendeleo ya huduma za kijamii na za kiuchumi za Zanzibar.


3)Kwa ujumla kodi ni makusanyo ya sehemu ya mapato yanayofanywa na utawala wa nchi kutoka wenye kipato kulingana na sheria ili mapato hayo yaweze kutumika kutoa huduma za jumla ambazo ni za lazima na haziwezi kutolewa na mtu mmoja mmoja, katika jamii nzima. Mfano wa hayo ni usalama wa raia, barabara, elimu na hata ulinzi wa nchi. Orodha wa yale ambayo yanaweza kuhudumiwa kwa kutumia kodi ni mrefu wala sina madhumuni ya kuelezea zaidi upande huo, isipokuwa tu kuongeza kuwa kwa ujumla madhumuni yake ni kuleta maendeleo ya nchi.

Zaidi ya yote hamasa na hiari ya ulipaji kodi usio wa kushurutishwa unachangiwa sana pale mlipa kodi anapoona kuwa kodi yake inatumika ipasavyo na kwa uangalifu na kwamba mwisho ya yote inamrudia mwenyewe kwa kupata huduma stahiki kama vile matibabu bora, elimu , huduma za maji nk. Hivyo ni jambo la msingi serikali iwe na uangalizi mkubwa katika suala la matumizi ili ipige vita aina zote za ubadhirifu ili mlipa kodi aone matunda ya kodi yake.

4)Kwa hapa Zanzibar vyombo vinavyokusanya kodi mbali na TRA, ni pamoja na Zanzibar Revenue Board, Mabaraza ya Manispaa, Halmashauri, na Vitengo vyengine vya Idara za serikali, ambavyo hukusanya “kodi” kwa majina mbalimbali.

5)Kwa upande wetu wafanyabiashara, tunahisi ingekuwa vyema kama shughuli hii ya leo ingelijumuisha pia na Bodi ya Mapato Zanzibar, na vyombo vyote vya ukusanyaji “mapato” kwani kwa mtazamo wetu Bodi hii, pamoja na vitengo vyengine vya serikali, vinawajibika moja kwa moja kwa Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na muhimu zaidi vinakusanya kodi kutoka mlipa kodi mmoja huyo huyo. Mkusanyiko wa vyombo vya ukusanyaji hapa leo ungeipa serikali picha halisi ya mzigo wa kodi na mzigo wa kuwajibika kulipa kodi (cost of compliance) kwa mlipa kodi. Katika mipango yake ya kutaka kodi kutoka kwa wafanyabiashara tunaiomba serikali isisahau kwamba kuna gharama za kuwajibika na kulipa kodi, mbali na kodi yenyewe. Serikali ina wajibu wa kupunguza gharama hizo na ikiwezekana kuziondosha kabisa.

6)Mheshimiwa Mgeni Rasmi, kitendo cha kuiweka siku maalum ya mlipa kodi ni kitendo cha kimaendeleo. Si mara nyingi watu, hata viongozi wanaoelewa yakua walipa kodi ndio “engine’ ya shughuli zote za Serikali. Mara nyingi watu huhisi yakua Serikali inazo tu fedha lakini hawajui zinatoka wapi. Kwa hivyo kitendo
cha kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kulipa kodi ni kitendo muwafaka kabisa. Ni katika kuiendeleza dhana hii ndio serikali inapata fursa ya kuanzisha ushirikiano na walipa kodi katika mfumo wa PPP wenye lengo la kuleta maendeleo ya wote kwa jumla.

7) Kitendo cha kuwapa tunzo walipaji kodi wazuri ni kitendo cha kiungwana na chenye kuleta faraja, kwani wahenga wanasema “mcheza kwao hutunzwa”, hata kama kitakuwa kidogo lakini hufarijika na kuwashajiisha wengine kuiga mfano mwema na hatimaye kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari. (Voluntary Tax Compliance). Haitakuwa vibaya kama katika hafla kama hii siku za mbele serikali au TRA ikavitambulisha vigezo vilivvyotumiwa kupata walipa kodi wazuri. Jambo hilo yumkin huenda likawashajiisha na wengine kujaribu kuvifikia. Kwani wafanyabiashara wakijaribu, hata kama hawakuvifikia watakua wamechangia katika makusanyo ya kodi.

8) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Labda tuulizane hii mbinu ya kuwazawadia walipa kodi wazuri inatosha kuongeza kodi kwa serikali? Sisi tunadhani mbinu hii inachangia sana lakini haitoshi pekee, na kwa hivyo mbinu nyengine kutoka upande wa sera itabidi ziangaliwe. Itabidi tuliangalie suala hili katika daraja ya sera na si ile daraja ya ukusanyaji pekee. Katika daraja ya sera kama tunataka kuongeza makusanyo hapana budi mbinu nyengine za ziada zitumiwe ili wigo utanuke, au biashara na uzalishaji utanuke zaidi.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

9) Katika uwanja wa biashara ni vipi tutaweza kuongeza makusanyo wakati soko la Zanzibar la watu milioni moja ni lile lile? Sisi wafanyabiashara tunadhani biashara inaweza kutanuka kama Zanzibar itajipatia soko kubwa zaidi ya lile la visiwa hivi viwili. Uanzishwaji wa Jumuia ya Africa Mashariki, pamoja na Zanzibar kuwa ni sehemu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ni nafasi ambazo zinaweza kutumiwa kisera kuipatia Zanzibar soko kubwa la bidhaa ambalo litaweza kutoa kodi ya kutosha kwa maendeleo ya Zanzibar. Kwa mantiki hii mbinu za kulifikia soko la Jumuia ya Africa Mashariki ndio kazi kubwa ya kuangaliwa watunga sera wetu.

10) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Naomba kutoa mfano mdogo kihesabu na uzoefu kuhusu namna ya kuitumia kodi kama nyenzo ya kuongeza mapato. Mfano Zanzibar inatoza wastani wa kodi ya 30% kwa bidhaa fulani bandarini, na mizigo 1,000 ya bidhaa hizo ikaingizwa nchini kwa kipindi fulani. Zanzibar itapata kodi sawa na mizigo 300. Lakini ikiwa itapunguza kodi hadi 5% tu (badala ya 30%) na mizigo ikapungua bei na ikaingizwa 50,000 (badala ya 1,000) basi Zanzibar itapata kodi ya wastani wa mizigo (5%x50,000 = 2,500). Ongezeko la hapa ni kutoka Zanzibar kupata wastani wa kodi wa mizigo 300 hadi kufikia mizigo 2,500. Papo hapo ieleweke hakuna namna ya mizigo kuongezeka kutoka 1,000 hadi kufikia 50,000 bila ya kazi hiyo kuongeza ajira nchini. Na vile vile tujiulize, Jee ni lazima mizigo iongezeke hadi kufikia 50,000 kutoka 1,000. La, hasha. Hata kama mizigo ingeongezeka kufikia 7,000 (kutoka 3,000) tu basi tayari wastani wa mizigo 300 umeshapitwa. Ninalojaribu kusema ni kuwa uko uwezekano kuongeza mapato ya kodi na ajira hata katika kupunguza viwango. Tunavyoiona TRA sisi wafanyabiashara wa Zanzibar ni kuwa ina sera maalum ya kuidhibiti Zanzibar isitumie fursa zilizomo ndani ya Muungano huu, na mbaya zaidi inaonekana ina mamlaka makubwa ya kutojali maamuzi ya viongozi wa Jamhuri Ya Muungano. TRA inaonekana ina sera ya kuitumia kodi kama kidhibiti Zanzibar!
11) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Wafanya Biashara sote hatuwezi kuwa walipa kodi bora, lakini sote tunaweza kuwa walipa kodi wazuri na kukaribiana katika ulipaji kodi kwa mujibu wa biashara zetu zilivyo. Aidha mchango wa kodi katika makusanyo unaweza kuongezeka kutokana na sera tunazoziomba kuwapa mwanya zaidi wafanyabiashara wetu kupata uhuru wa kufanya biashara wakiwa hapa Zanzibar, na kulipa kodi zao hapa Zanzibar bila ya kushurutishwa kuhamishia biashara zao Tanzania Bara au sehemu nyengine za Africa Mahariki. Katika mkakati wa kuendeleza Tanzania TRA nao waelimishwe yakua Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri hii na maendeleo au mafanikio ya Zanzibar ni maendeleo ya Tanzania na wao wawe watekekezaji wa sera za kuendeleza Tanzania yote.

12) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, hivi sasa tunaona wafanyabiashara wetu wengi wakihamisha sehemu kubwa ya biashara zao na kuzipeleka Tanzania Bara na huku wakituambia yakua vikwazo vya kodi hasa ya bandarini vimewaondokea katika biashara zao za huko bara. Jee kuna sera mbili za kuendeleza Tanzania. Jee kuna manufaa yeyote kwa Tanzania kama upande wake mmoja utadumaa. Sisi wafanyabiashara wa Zanzibar na ambao tunalipa kodi hapa Zanzibar, tunadhani kuna upotofu katika muelekeo huu wa TRA kuhusu biashara za Zanzibar; na kwa vile kijiografia Dar-es-salaam ndio njia ya bidhaa za Zanzibar kuingia katika soko la Africa Mashariki kwenda Uganda, Rwanda Burundi na Kenya suala hili lina umuhimu wake na tunaomba lisidharauliwe.

13) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Hapa naomba kutoa mfano hai wa yanayofanywa na TRA kuhusu biashara za Zanzibar ziendazo bara na zipitiazo bara kwenda nchi za nje. Super Shine ni kiwanda kipo eneo la Viwando Vidovidogo Amani kwa sheria za ZIPA EPZ kama mwekezaji tokea 1996. Kinazalisha audio cassettes, video cassttes, CDs, DVDs na bidhaa za plastic kwa kuuza 20% ndani ya nchi na 80% nje ya nchi.
Kinyume na makubaliano ya nyuma na sheria za EPZ kuanzia Aug 2011 wameanza kulazimishwa kulipa VAT na Import Duty kwa bidhaa zinazoingizwa Tanzania bara. Kwa maana hii bidhaa zinazozalishwa Zanzibar ni bidhaa za kigeni zinapoingizwa Bara. Wakati huo huo bidhaa zote za viwanda vya bara km saruji hailipishwi kodi hizi zinapoingizwa Zanzibar.
14) Jengine ni kuwa kuanzia Aug 2011 wamelazimishwa kulipa VAT na Import Duty kwa zile bidhaa wanazosafirisha nje ya nchi. Haya ni maajabu, bidhaa zinapita tu Tanzania bara na zinatozwa VAT ambayo ni kodi ya mlaji (wa Zambia) na Import duty wakati bidha hizi ni Exports zinapita njia tu. (maelezo kamili yapo kwenye pamphlet ambayo tutaomba tukupe Mheshimiwa Mgeni Rasmi.), pamoja na hotuba yetu hii.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

15) Sisi wafanyabiashara tunashukuru kuwa mwaka 2009 tulipatiwa fursa ya kutoa maoni yetu ingawa ufumbuzi bado umekuwa hafifu, hata hivyo tunathamini umuhimu wa siku hii ya mlipa kodi, kwa matumaini yakua maoni yetu yatasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi na mengine kuendelea kufanyiwa kazi kwa manufaa ya Zanzibar. Wakati huo huo kuna masuala mengine yamejitokeza na tunahisi kuwa ni muhimu kuangaliwa ili kumfanya mlipa kodi wa Zanzibar awe na shauku ya kulipa kodi na vile vile kuwashawishi wafanyabiashara wetu waendeleze biashara zao Tanzania nzima pamoja na Africa Mashariki huku wakiishi na kulipa kodi Zanzibar. Hii ni kwa dhamira ya kuona yakua si lazima kwa wafanyabiashara wahamie bara ili waendeleze biashara zao huko. Sasa naomba nieleze, kwa muhtasari yale ambayo tuliyasema mwaka 2009 na ambayo hayakuchukuliwa hatua pamoja na mepya ambayo ni muhimu kushughulikiwa.

16) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, ingawa ni vyema kwa walipa kodi kulipa kodi, ni vyema vilivile wapewe uhuru wa kupata mapato ili walipe kodi.

17) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, leo hii tunazungumzia walipa kodi na mchango wao katika maendeleo. Si vibaya tukazungumzia wakusanyaji kodi nao mchango wao katika kuhakikisha yakua kodi inakuwa nyingi hapa Zanzibar ili ikusanywe na kuwasilishwa serikalini.

18) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, hapo juu nilitoa mfano wa kimahesabu kuhusiana na kodi na mienendo yake. Mfano ulikuwa wa kuongeza makusanyo ya kodi kwa kupunguza viwango vya kodi. Sasa naomba kutoa uzoefu tuliouona hapa Zanzibar kutokana na bidhaa kuongezewa kodi. Itakumbukwa yakua kulikuwa na kodi hapa Zanzibar zilizowaruhusu wafanyabiashara kuuza kwa bei za chini kulingana na kwengineko Africa Mashariki katika miaka ya 1990s na mapema ya 2000s. Matokeo ya bei hizo ni kuwa wafanya biashara wengi kutoka nje kama vile Comoro, Malawi, Burundi, Rwanda, Zambia, Kenya n.k walikuja kwa wingi kununua bidhaa, na kuzichukua makwao. Mbali na kukuza mfuko wa kodi walikuwa wakiishi kwenye mahoteli na kutumia huduma za mikahawa, taxi, mikokoteni nk. Yote hayo yalipotezwa kwa uamuzi wa TRA kuwatoza kodi za ziada bandarini Dsm hata kama wikuwa wakipita tu njia Dar es salaam. Katika hili Zanzibar imekosa kila kitu na wafanyabiashara pia wamekosa kila kitu. Hakuna tena wafanyabiashara kutoka nchi za jirani wanaokuja Zanzibar kununua bidhaa zao. Bila shaka kodi kwa Zanzibar nayo imepotea.

19) Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Ipo haja ya kujiuliza kama matokeo ya aina hii yanasaidia kujenga moyo wa ulipaji kodi katika wafanyabiashara wetu. Ni jambo la uhakika kwamba kila mlipa kodi atalipa kodi kwa furaha bila kinyongo kwa kiwango chochote pindipo tu akiona kwamba kodi anayoilipa inarudi kwake kwa jinsi inavyotumika kweli kweli katika kuleta maendeleo na kutoa huduma za jamii – afya ,elimu, miundombini n.k. Mifano hii inaonekana wazi katika nchi za wenzetu zilizoendelea.

20) Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Naomba kueleza kidogo kuhusu ukubwa wa kodi za Zanzibar kulingana na zile za bara. Ingawa Corporate tax hapa ni 30% kwa Tanzania yote kodi halisi yaani “effective tax rate”ni 40% hapa Zanzibar kulingana na uchambuzi uliofanywa na “Doing Business in Zanzibar. Viwango vya walipa kodi binafsi (Individual tax rates) pia vile vya Zanzibar ni vikubwa sana kulinganisha na vya Tanzania bara ingawaje hali ya kipato cha Wanzanzibari ni kidogo zaidi. Kodi ya Ujuzi wa Maendeleo – Skills Development Levy (SDL) abayo ni asilimia tano (5%) ya mapato ya mishahara ya wafanyakazi pia ni kubwa mno na tuna wasi wasi kwamba haitumiki kwa malengo khasa yaliyokusudiwa. Kulingana na ukubwa wa uchumi wa Zanzibar viwango hivi vya kodi ni vikubwa na vinadumaza juhudi ya kujipatia kipato na vivyo hivyo juhudi za kuongeza makusanyo ya kodi. Kwa upande wa sera naomba ieleweke kua kodi iliyo kubwa ina punguza shauku ya wawekezaji kuweka mitaji yao katika uchumi husika. Katika hali ya Zanzibar kodi kubwa na soko dogo ni mchanganyiko maalum wa kuwatisha wawekezaji na hivyo kupunguza mapato ya kodi, ajira na mengineyo. Kama washauri tunaomba viwango vya kodi viangaliwe ili vyenyewe viwe ni vivutio kwa wawekezaji

21) Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Muundo wa uongozi wa TRA Zanzibar (Organization Structure) bado hautoi mamlaka ya maamuzi kwa mujibu wa taratibu za TRA, hivyo tunaishauri Serikali iliangalie suala hili kwa undani zaidi ili maamuzi yanayotolewa na TRA Zanzibar yaheshimike na yaonekane kuwa ni maamuzi sahihi kama yalivyo kwa maamuzi ya TRA ya Tanzania Bara. Atawezaje kuisaidia Zanzibar kupata kodi zaidi ikiwa maamuzi yake hayathaminiwi. Jambo hili nalo linahitaji ufumbuzi.

22. Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Mwisho, kwa vile leo ni siku yetu walipa kodi tunapenda kutoa kilio chetu juu ya haki yetu ya msingi tunayonyimwa ndani ya sheria ya Rufaa za Kodi (Zanzibar Tax Appeals Act (2006). Sheria hii ilianzishwa kwa misingi ya kutoa haki kwa mlipa kodi pindi asiporidhika na maamuzi ya vyombo vinavyokusanya kodi. Tuna hakika kwamba toka ilipoanzishwa bodi hiyo ya rufaa mwaka 2006 hakuna kesi hata moja waliyoipokea na sisi kama walipa kodi hatutegemei kupeleka kesi yoyote huko kutokana na ukandamizaji wa sheria hiyo na jinsi isivyompa haki mlipa kodi. Sheria ina masharti mawili makubwa kwanza- ni Lazima ikiwa mlipa kodi hakuridhika na kodi aliyoamriwa kulipa na Kamishna, basi afanye Objection kwa Kamishna wa chombo cha kodi kinachohusika (TRA/ZRB). Tatizo hapa ni kwamba kama tokea mwanzo mlipa kodi na Kamishna wameshindwa kukubaliana vipi mlipa kodi anatakiwa arudi tena kukata rufaa ya awali kwa huyo huyo kamishna waliyekwisha kukosana na atendewe haki? Pili, sheria inamtaka mlipa kodi alipe kwanza kodi aliyoamriwa na kamishna kiwango cha asilimia hamsini (50%), ili kesi yake iweze kusikilizwa. Yupo mlipa kodi ambae tayari amekisiwa na ameamriwa kulipa jumla ya kodi ya Tshs bilioni sita, maana yake ni kwamba anatakiwa alipe kwanza bilioni tatu ili asikilizwe, jambo ambalo milele haliwezekani. Mambo haya mawili yanamnyima uhuru na haki mlipa kodi, na tunapendekeza yaondolewe mara moja katika sheria ikiwa kweli tunataka ulipaji kodi wa hiari, (Voluntary compliance) wenye uwajibikaji (accountability) na usafi (transparency).
23) Umuhimu wa elimu ya kodi kwa walipaji na wakusanyaji hauhitaji kusisitizwa zaidi. Lililo muhimu ni uadilifu katika utendaji wa kazi zetu.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
ZNCCIA
Siku ya Mlipa Kodi
Zanzibar.
06/12/2011
Chanzo: Zanzinews

Tanzania yakataa ushirikiano ulinzi, siasa EAC

Keneth  Goliama
TANZANIA imekataa Shirikisho la  Ulinzi, Siasa  pamoja na Kinga za Viongozi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na   kutaka mambo hayo  kujadiliwa   kwa upana zaidi  kuhusu uundwaji wake ili wananchi waweze kushirikishwa kutoa maoni yao.

Hata hivyo Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, wamekubaliana kwa pamoja kuunda Sekretarieti maalum ya Watalaam  wa kufuatilia mchakato mzima wa maoni ya watu ili waweze kuyawasilisha katika mkutano ujao.

Katika mkutano huo pia kumependekezwa  kuanzishwa kwa Benki Kuu  Umoja wa Jumuiya ya  fedha, Bunge la Jumuiya lenye uwakilishi wa Kisiasa , Mamlaka ya Uangalizi, mahakama ya Jumuiya Afrika mashariki itakayosimamia na kuhakiki  mikataba .

Akizungumza na waandishi wa habari , Katibu Mkuu  Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Dk Stergomena Tax alisema Tanzania  haijakubaliana na Uundwaji wa Shirikisho la kisiasa , Ulinzi na Ardhi kwa madai kuwa masuala  hayo  yanahitaji muda zaidi wa kujadiliwa na wadau husika wa Jumuiya.

Aliyataja mambo mengine yaliyokubaliwa  katika  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Baraza la Mawaziri  kuwa ni pamoja na  Sera ya mkakati wa uendelezaji wa viwanda, Kuimarisha Huduma ya Forodha, Itifaki ya kuzuia na kupambana  Rushwa  sambamba na Itifaki ya kinga na hadhi ya jumuiya zilizopo chini ya Jumuiya.

Dk .Tax Alisema  suala la Ulinzi Shirikishi na siasa katika mkutano huo liliibua mjadala mzito na kuonekana kuwa changamoto inayohitaji kufikiriwa kwa makini ili kuepusha nchi husika kuingia katika migogoro baina ya nchi na nchi pale zitakapo pingana .

 “Nikitolea mfano mambo ya vita katika kushirikiana na kusaidiana na nchi inayopigwa ndani ya Jumuia ya Afrika mashariki linatakiwa kujadiliwa kwa  kina na kufanyiwa marekebisho ili kujua mambo gani muhimu yatakayohusika katika Ulinzi ili kuweza kujulikana  na kukubaliana” alisema Dk Tax.
Katika Mkutano huo  Tanzania imeteuliwa  kuwa Mwenyeji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika mashariki ambaye Makao Makuu yake yatakuwa Zanzibar huku Rwanda ikichaguliwa kuongoza Kamisheni ya Sayansi naTeknolojia  na Burundi ikiongoza Kamisheni ya Utafiti wa Afya.
Alisema upataji wa wenyeji huo unatokana na Tanzania kuwa mwombaji pekee sambamba na kuomba  nafasi zingine  za Afya na Sayansi na Teknolojia  ambazo haikufanikiwa badala  yake ilionekana kuwa na sifa katika Kamisheni ya  Kiswahili.

 Alisema kwa kupata nafasi hiyo  Tanzania itanufaika kwa kiasi kikubwa katika kuinua Uchumi wake kutokana na kuwepo kwa  soko huria  katika sekta za biashara ,viwanda na uwekezaji katika kupunguza vikwazo vya uchumi.

Katika kongamano la Jumuia ya Afrika mashariki kuhusu Maendeleo ya Bonde la ziwa Tanganyika, Katibu huyo alisema ,  walijadili nchi wanachama kuvutia biashara na kuongeza uwekezaji katika nchi wanachama ili kutumia maliasili nyingi zilizopo kwaajili ya  kuinua uchumi.

Dk Tax alisisitiza kuwa Tanzania haina budi kulipeleka  Suala la Ardhi, Ulinzi, Siasa kwa wananchi ili walijadili zaidi kwani matokeo ya awali yalionyesha kuwa  asilimia 75 ya Watanzania walikataa uharakishwaji wa uundwaji Shirikisho hilo .

Dk Tax alisema nchi wanachama zinatakiwa kupima Ardhi na kuanzisha vyombo vya msingi  vinavyotoa haki ya umiliki wa ardhi  kwa wananchi , Kusimamia  mgawo wa faida,  na gharama za mali asili kuwa sehemu ya majadiliano katika mkataba wa uundwaji wa shirikisho la kisiasa.
Kuhusu maombi ya uanachama wa Nchi za Sudan Kusini na Sudan Kaskazini , alisema majadiliano hayo yalifanyika na kwamba  Sudan Kaskazini ilikosa vigezo vya kujiunga  kutokana na umbali uliopo katika mipaka na nchi wanachama .

Alisema Sudan Kusini ilikidhi katika ibara ya tatu ya vigezo vya kujiunga lakini majadiliano zaidi yanaendelea ili kuhakikisha  wanapata mwafaka zaidi katika kuweza kujiunga
Chanzo: Mwananchi

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA UK


Uhuru wa Tanzani UK